Buriani Hassan Chikusa msomi mkimya

Buriani Hassan Chikusa msomi mkimya

Waislamu weusi wajingas sana mtume Muarabu muuza watumwa hawatambui kamweee!...na hata hako ka yesu kazungu kakoloni hakawataki wakristo!!

weusi mmekimbia dini yenu ya kweli...pamoja na Biblia kuwafunuia mambo meeengi lkn Bado…….Torati ya Musa inasema '' Mtarudishwa Misri kwa mitumbwi na huko Mtaabudu msicho kijua''' na kweli Anglia mlivyoooo!
 
Hivi Dar es salaam kwa Mimi ambaye sijafika kumbe sijui vingi? Yaani hapo Dar es salaam kuna maeneo maalum ya Waislamu pekee kiasi kwamba ni kosa kisheria kujenga bucha ya nyama ya nguruwe, au Mimi ndo sijakuelewa uliposema yalijengwa kinyume cha sheria? Au tusaidie hiyo sheria iliyovunjwa ni ipi?
kama mabucha 🐷🐷yapo kati ya makazi ya waislamu wengi na yanauza nini tafsiri yake? Wateja walikuwepo, maana wasingekuwepo yangefilisika. Kama wakazi wengi ni waislamu na ngurue anaisha nani ananunua 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Daudi,
Nilikuwako katika shura pale msikitini lakini wasemaji walikuwa viongozi wetu.

Kutokana na sakata hii la mabucha nilialikwa Kenyatta University, Nairobi kuzungumza.

View attachment 2305337

Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma (1940 – 1994) And the Dar es Salaam Pork Riots of 1993​

Unknown December 25, 2013 0
Islam’s Encounter with the Challenges of the 21st Century
1ST – 4TH AUGUST 2006
Organised by
Department of Philosophy & Religious Studies
KENYATTA UNIVERSITY
Venue
Kenyatta University
NAIROBI
Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma
(1940 – 1994)
And the Dar es Salaam Pork Riots of 1993

Speaker

Mohamed Said​
Mzee ulikimbia aisee, haiwezekani uhudhurie shura pamoja na Hassan Halafu Hassani akamatwe we muda mchache usionekane eti umeitwa Nairobi, kumbuka kwenye stori ya kuna shehe mkuu alikamatiwaa njiani akitorokea Nairobi wakamrudisha Dar (ulidai alikuwa anaenda kwenye matibabu)
 
BURIANI HASSAN CHIKUSA MSOMI MKIMYA
Naamini si wengi wanamfahamu Hassan Chikusa na yote yaliyomsibu katika maisha yake.

Mimi nilimjua Hassan Chikusa kwa kuwa alikua jirani yangu akiishi kwa ndugu yake Masaki jirani na nyumba niliyokuwa naishi mimi na familia yangu.

Wakati ule alikuwa kijana mdogo ndiyo kwanza amemaliza masomo yake na anafanya kazi Makao Makuu National Bank of Commerce (NBC), Sokoine Drive.

Tulizoeana sana na wakati mwingine akija nyumbani kwa mazungumzo na akipenda mazungumzo yangu katika vitabu, historia na muziki kama ilivyo kawaida ya vijana.

Hassan alikuwa akiweka shajara yaani akiandika, ''diary.''

Hassan alikuwa kijana akiipenda dini yake sana kwa mapenzi makubwa.
Mwaka wa 1993 pakawa na sakata la uvunjaji mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe Wilaya ya Kinondoni baada ya sala ya Ijumaa.

Kilichotokea ni kuwa kijana alitumwa nyama na muuza nyama pengine kwa kutokujua akamuuzia huyu kijana nyama ya nguruwe.

Palikuwa na malalamiko kuhusu haya mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe lakini walioshika madaraka hawakujali wala kutia maanani malalamiko ya Waislam.

Mjini Dar es Salaam kulikuwa na mabucha 29 ya kuuza nyama ya nguruwe kwenye sehemu wanazoishi Waislam na hii ilikuwa kinyume cha sheria.

Tatizo hili Waislam wakalifikisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mustafa Nyang;anyi lakini hakuna kilichofanyika na likafikishwa pia kwa Waziri Mkuu, John Samuel Malacela.

Waswahili wanamsemo wanasema yale yalikuwa sawa na kutwanga maji katika kinu.

Hili tatizo la mabucha likashushwa chini hadi kwa Mkuu wa Wilaya, Wilson Mkama na yeye akawaita ofisini kwake maimamu wa misikiti mitano ya Wilaya ya Kinondoni kwa mazungumzo.

Serikali haikuwa tayari kufunga mabucha hayo kwa kile walichokiona ni shinikizo kutoka kwa Waislam wenye, ''siasa kali.''

Bwana Mkama akawaeleza maimam kuwa hayo mabucha yapo kihalali na wana leseni walizopewa na serikali kufanya biashara hiyo kwa ajili hii serikali ina dhima ya kuzilinda hizo bucha.

Mkutano ukamalizika na maimamu wakarejea misikitini kwao kuwaeleza Waislam kauli ya serikali kuhusu mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe.

Waingereza wana msemo, ''The straw which broke the camel's back,'' yaani ujani uliowekwa juu ya mgongo wa ngamia ukauvunja.

Waislam walighadhibika sana kwa uamuzi wa serikali kuwapuuza.
Siku ya pili ilikuwa Ijumaa Kuu.

Baada ya sala ya Ijumaa vijana wa Kiislam walipomaliza sala waliziendea zile bucha zilizokuwa Wilaya ya Kinondoni wakazivunja zote kwa mpigo.

Dar es Salaam ilizizima.
Haya hayakupata kutokea katika kipindi chote cha uhuru.

Rais Ali Hassan Mwinyi akiwa Zanzibar akasema katika kulani kuvunjwa mabucha ya nguruwe kuwa nguvu za dola ziwaangukie wale waliovunja mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe.

Jioni yake BBC hwakuchelewa wakafanya mahojiano na Waziri Mkuu John Samuel Malecela.

Malecela akasema kuwa waliovunja mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe ni wahuni wanotaka kuchukua serikali kupitia dini.

Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu Augustine Mrema yeye akasema mabucha yamevunjwa kutokana na nguvu kutoka nchi ya Kiislam ili kuivuruga Tanzania.

Katibu Mkuu wa CCM Horace Kolimba yeye akahitimisha kwa kusema kuwa waliovunja mabucha si Waislam ila ni wahuni wanaotaka kupindua serikali.

Kufika asubuhi siku ya Jumamosi masheikh 40 wakawa wamekamatwa usiku wa manane kwa taadhira kubwa majumbani kwao mfano wa majambazi na kutiwa korokoroni.

Wahariri wa magazeti asubuhi yake siku ya Jumamosi wakawa katika burdani kubwa ya kuandika kuvunjwa kwa mabucha ya kuuza nguruwe na kukamatwa kwa masheikh.

Asubuhi ile ya Jumamosi kundi dogo la Waislam wakaenda Kituo Cha Kati cha Polisi kufuatilia masheikh waliokamatwa usiku na kuwekwa korokoroni hapo.
Hawa nao wakakamatwa na kuwekwa ndani.

Haukupita muda baada ya habari kuenea kuwa Waislam waliokwenda kuwauliza masheikh na wao wamekamatwa Waislam wakaja kwa wingi kituoni siku ya pili yake Jumapili iliyokuwa Easter Sunday.

Siku hiyo Waislam wakakusanyika pale kituoni ikawa kama vile kituo kimezingirwa na sala ya L'Asr ilipoingia ikapigwa adhana pale nje ya ya kituo watu wakasali barabarani.

Polisi wakataka kuwapiga mabomu ya machozi lakini pakawa na kutokubaliana baina ya askari wenyewe.

Hawakupendezewa na kitendo kile.

Askari Waislam wakawaambia wenzao hilo haliwezi kufanyika kuwapiga mabomu Waislam wanaosali kwani ni kufuru kubwa Waislam hawajafanya fujo wamekuja kituoni kufuatilia masheikh wao walioko korokoroni.

Jua lilipotua Waislam wakaondoka pale kituoni wakaamua wakutane siku ya pili Msikiti wa Mtoro washauriane.

Siku hii ya Jumapili yaani Easter Sunday mimi ndiyo niliingia Dar es Salaam nikitokea Le Havre, Ufaransa nikaja Paris kwa muda wa siku mbili kisha nikaenda London kisha Cardiff na kurejea London kupanda ndege kurudi Dar es Salaam.

Nilipofika nyumbani ndipo nilipopata taarifa ya masheikh kukamatwa na kati ya masheikh hao alikuwa mjomba wangu Sheikh Pazi wa Manzese.

Sikusubiri nikaenda kwa Hassan Chikusa wakati huo akiishi Mwananyamala kwani nilijua pamoja na kupita kwa jamaa wengine yeye ndiye ataweza kunipa taarifa ya mkasa mzima pamoja na tathmini.

Hayo niliyoandika hapo juu ni baadhi ya mambo aliyonifahamisha kuwa yametokea kuanzia siku ile ya Ijumaa yalipovunjwa mabucha hadi siku ya pii yake Jumamosi.

Hili ninalosema sasa ni jambo ambalo kwa miaka yote kila nilipokutana na Hassan moyo uliniuma sana nikiishia kumuombea dua.

Hassan siku ile nilipokwenda kwake ilikuwa Jumapili usiku na hakuwa na taarifa kuwa siku ya Jumatatu, yaani Easter Monday Waislam wameamua kufanya shura ndani ya Msikiti wa Mtoro ambao Imam Mkuu, Sheikh Kassim Juma alikuwa kakamatwa Arusha akielekea Nairobi kwenye matibabu na kurudishwa Dar es Salaam na yuko rumande.

Mimi ndiye nliyemfahamisha kuwa kesho Easter Monday kuna shura ya Waislam wote wa Dar es Salaam kujadili kwa pamoja nini kifanyike kurejesha heshima ya masheikh wetu.

Hassan aliniuliza kama mimi nitakuwepo.
Nikamwambia In Shaa Allah nitakuwapo.

Hassan Chikusa na yeye akaniambia atakuwapo pia.

Kwa ufupi siku ile ndani ya Msikti wa Sheikh Mtoro Mwinyi Mangara iliamriwa baada ya mjadala mkali sana Waislam watoke kwa maandamano hadi Kituo Cha Kati Cha Polisi kwenda kuwatoa masheikh wao korokoroni.

Katika maandamano yale Waislam walipambana na polisi na mabomu ya machozi yalipigwa.

Mapambano haya yalifanyika kati ya kituo cha polisi na Clock Tower.
Haya ndiyo yalikuwa maandamano ya kwanza ya Waislam Tanzania Bara.

Zanzibar maandamano yao yalikuwa mwaka wa 1988.
Maandamano haya yote tatizo ni Uislam.

Hassan Chikusa akakamatwa pamoja na vijana wengi wa Kiislam.
Wakawekwa rumande wakashtakiwa na kuhukumiwa vifungo jela.

Hassan Chikusa akapoteza kazi yake NBC.

Huyu ndiye Hassan Chikusa msomi mkimya ambae baada ya kutoka jela akiwa hana kazi masahibu mengi ya maisha yalimfika.

Lakini siku zote akisema yaliyomfika ni madogo sana na yote ameyakadiria Allah na na yeye bado yu hai.

Kwangu mimi maadamano yale na wale walioshiriki katika yale maandamano kile kilikuwa kipimo.

Tunamuomba Allah amsamehe makosa yake mja wake huyu na amtie Firdaws.
Amin.

View attachment 2305229
Hassan Chikusa​
Mzee makala yako ni ndefu lakini haujatueleza "USOMI" wa Hassani Chikusa kwamba alikuwa na elimu gani ya juu? ya dini au secular, ila maelezo yako yameegemea kwenye harakari za waislamu kuvunja mabucha na kupambana na polisi.
 
Mwenyezi Mungu amlaze marehemu mahali pema peponi.

Back to the point. Mimi nimezaliwa katika familia ya kiislamu but i am regretting to tell all christians and muslims wherever they are that religion is an opium of poor people..

Mwenyezi Mungu hana dini wala hatambui dini yoyote.

Mambo ya dini ni ujinga wetu tu wa hapa duniani.

Ona kama hiyo ishu ya watu kupoteza maisha mwembechai mwaka 98.

People were killed over bullshit
 
Daah moyo wangu huumia sana napopata historia juu ya maonevu wanayoyapitia waislamu hapa nchini.Ndani ya Tanzania waislamu ndiyo jamii pekeee iliyoumizwa Mara nyingi zaidi huku wakiwa dhariri na hakuna wa kuwatetea.
 
Ndani ya Tanzania waislamu ndiyo jamii pekeee iliyoumizwa Mara nyingi zaidi huku wakiwa dhariri na hakuna wa kuwatetea.
Pole mkuu wakati mashehe wa uamsho wanakamatwa wafuatao walibariki na walikuwa waislam
1. Rais JK
2. IGP said Mwema
3. Mwanasheria mkuu wa serikali. Othman
4. Viongozi wote wa serikali wa Zanzibar
 
Alikuwa siasa kali ya kidini Answar Sunna

Kipindi kile si tu walivunja mabucha ya nguruwe lakini pia walileta migogoro mingi misikitini wakitaka kupora misikiti.ya Bakwata iwe ya Answar Sunna na uongozi iwe wa Answar Sunna

Serikali ikawadhibiti barabara ndipo wakatulia
shida sana waislam ndio mmesababisha hata Nigeria hapakaliki kwa itikadi zenu za kijinga..NB: SINA DINI
 
Kabla sijasoma maoni mzee wangu ningeomba msaada wa hicho kifungu kinacho sema "maeneo haya ni ya waislamu"

Je, ni waislamu tu ndio waliopatiwa maeneo au kumilikishwa?

Je, kama yapo ni utawala wa awamu ipi waligawa haya maeneo?

Je, dini zingine mfano kristo, hindu, dini za asili nao wanao mgao huo kama ndugu zao islamic?

Mwisho kwa mtazamo wako unaona jambo la kugawa hayo maeneo lina tija kwa taifa la sasa hususani kwenye kujenga mshikamano kitaifa?
Mtu hawezi fungua biashara sehemu ambayo anajua hawezi pata wateja automatically hayo maeneo wateja wapo haijalishi Imani yao. Kazi iendelee
 
BURIANI HASSAN CHIKUSA MSOMI MKIMYA
Naamini si wengi wanamfahamu Hassan Chikusa na yote yaliyomsibu katika maisha yake.

Mimi nilimjua Hassan Chikusa kwa kuwa alikua jirani yangu akiishi kwa ndugu yake Masaki jirani na nyumba niliyokuwa naishi mimi na familia yangu.

Wakati ule alikuwa kijana mdogo ndiyo kwanza amemaliza masomo yake na anafanya kazi Makao Makuu National Bank of Commerce (NBC), Sokoine Drive.

Tulizoeana sana na wakati mwingine akija nyumbani kwa mazungumzo na akipenda mazungumzo yangu katika vitabu, historia na muziki kama ilivyo kawaida ya vijana.

Hassan alikuwa akiweka shajara yaani akiandika, ''diary.''

Hassan alikuwa kijana akiipenda dini yake sana kwa mapenzi makubwa.
Mwaka wa 1993 pakawa na sakata la uvunjaji mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe Wilaya ya Kinondoni baada ya sala ya Ijumaa.

Kilichotokea ni kuwa kijana alitumwa nyama na muuza nyama pengine kwa kutokujua akamuuzia huyu kijana nyama ya nguruwe.

Palikuwa na malalamiko kuhusu haya mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe lakini walioshika madaraka hawakujali wala kutia maanani malalamiko ya Waislam.

Mjini Dar es Salaam kulikuwa na mabucha 29 ya kuuza nyama ya nguruwe kwenye sehemu wanazoishi Waislam na hii ilikuwa kinyume cha sheria.

Tatizo hili Waislam wakalifikisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mustafa Nyang;anyi lakini hakuna kilichofanyika na likafikishwa pia kwa Waziri Mkuu, John Samuel Malacela.

Waswahili wanamsemo wanasema yale yalikuwa sawa na kutwanga maji katika kinu.

Hili tatizo la mabucha likashushwa chini hadi kwa Mkuu wa Wilaya, Wilson Mkama na yeye akawaita ofisini kwake maimamu wa misikiti mitano ya Wilaya ya Kinondoni kwa mazungumzo.

Serikali haikuwa tayari kufunga mabucha hayo kwa kile walichokiona ni shinikizo kutoka kwa Waislam wenye, ''siasa kali.''

Bwana Mkama akawaeleza maimam kuwa hayo mabucha yapo kihalali na wana leseni walizopewa na serikali kufanya biashara hiyo kwa ajili hii serikali ina dhima ya kuzilinda hizo bucha.

Mkutano ukamalizika na maimamu wakarejea misikitini kwao kuwaeleza Waislam kauli ya serikali kuhusu mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe.

Waingereza wana msemo, ''The straw which broke the camel's back,'' yaani ujani uliowekwa juu ya mgongo wa ngamia ukauvunja.

Waislam walighadhibika sana kwa uamuzi wa serikali kuwapuuza.
Siku ya pili ilikuwa Ijumaa Kuu.

Baada ya sala ya Ijumaa vijana wa Kiislam walipomaliza sala waliziendea zile bucha zilizokuwa Wilaya ya Kinondoni wakazivunja zote kwa mpigo.

Dar es Salaam ilizizima.
Haya hayakupata kutokea katika kipindi chote cha uhuru.

Rais Ali Hassan Mwinyi akiwa Zanzibar akasema katika kulani kuvunjwa mabucha ya nguruwe kuwa nguvu za dola ziwaangukie wale waliovunja mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe.

Jioni yake BBC hwakuchelewa wakafanya mahojiano na Waziri Mkuu John Samuel Malecela.

Malecela akasema kuwa waliovunja mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe ni wahuni wanotaka kuchukua serikali kupitia dini.

Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu Augustine Mrema yeye akasema mabucha yamevunjwa kutokana na nguvu kutoka nchi ya Kiislam ili kuivuruga Tanzania.

Katibu Mkuu wa CCM Horace Kolimba yeye akahitimisha kwa kusema kuwa waliovunja mabucha si Waislam ila ni wahuni wanaotaka kupindua serikali.

Kufika asubuhi siku ya Jumamosi masheikh 40 wakawa wamekamatwa usiku wa manane kwa taadhira kubwa majumbani kwao mfano wa majambazi na kutiwa korokoroni.

Wahariri wa magazeti asubuhi yake siku ya Jumamosi wakawa katika burdani kubwa ya kuandika kuvunjwa kwa mabucha ya kuuza nguruwe na kukamatwa kwa masheikh.

Asubuhi ile ya Jumamosi kundi dogo la Waislam wakaenda Kituo Cha Kati cha Polisi kufuatilia masheikh waliokamatwa usiku na kuwekwa korokoroni hapo.
Hawa nao wakakamatwa na kuwekwa ndani.

Haukupita muda baada ya habari kuenea kuwa Waislam waliokwenda kuwauliza masheikh na wao wamekamatwa Waislam wakaja kwa wingi kituoni siku ya pili yake Jumapili iliyokuwa Easter Sunday.

Siku hiyo Waislam wakakusanyika pale kituoni ikawa kama vile kituo kimezingirwa na sala ya L'Asr ilipoingia ikapigwa adhana pale nje ya ya kituo watu wakasali barabarani.

Polisi wakataka kuwapiga mabomu ya machozi lakini pakawa na kutokubaliana baina ya askari wenyewe.

Hawakupendezewa na kitendo kile.

Askari Waislam wakawaambia wenzao hilo haliwezi kufanyika kuwapiga mabomu Waislam wanaosali kwani ni kufuru kubwa Waislam hawajafanya fujo wamekuja kituoni kufuatilia masheikh wao walioko korokoroni.

Jua lilipotua Waislam wakaondoka pale kituoni wakaamua wakutane siku ya pili Msikiti wa Mtoro washauriane.

Siku hii ya Jumapili yaani Easter Sunday mimi ndiyo niliingia Dar es Salaam nikitokea Le Havre, Ufaransa nikaja Paris kwa muda wa siku mbili kisha nikaenda London kisha Cardiff na kurejea London kupanda ndege kurudi Dar es Salaam.

Nilipofika nyumbani ndipo nilipopata taarifa ya masheikh kukamatwa na kati ya masheikh hao alikuwa mjomba wangu Sheikh Pazi wa Manzese.

Sikusubiri nikaenda kwa Hassan Chikusa wakati huo akiishi Mwananyamala kwani nilijua pamoja na kupita kwa jamaa wengine yeye ndiye ataweza kunipa taarifa ya mkasa mzima pamoja na tathmini.

Hayo niliyoandika hapo juu ni baadhi ya mambo aliyonifahamisha kuwa yametokea kuanzia siku ile ya Ijumaa yalipovunjwa mabucha hadi siku ya pii yake Jumamosi.

Hili ninalosema sasa ni jambo ambalo kwa miaka yote kila nilipokutana na Hassan moyo uliniuma sana nikiishia kumuombea dua.

Hassan siku ile nilipokwenda kwake ilikuwa Jumapili usiku na hakuwa na taarifa kuwa siku ya Jumatatu, yaani Easter Monday Waislam wameamua kufanya shura ndani ya Msikiti wa Mtoro ambao Imam Mkuu, Sheikh Kassim Juma alikuwa kakamatwa Arusha akielekea Nairobi kwenye matibabu na kurudishwa Dar es Salaam na yuko rumande.

Mimi ndiye nliyemfahamisha kuwa kesho Easter Monday kuna shura ya Waislam wote wa Dar es Salaam kujadili kwa pamoja nini kifanyike kurejesha heshima ya masheikh wetu.

Hassan aliniuliza kama mimi nitakuwepo.
Nikamwambia In Shaa Allah nitakuwapo.

Hassan Chikusa na yeye akaniambia atakuwapo pia.

Kwa ufupi siku ile ndani ya Msikti wa Sheikh Mtoro Mwinyi Mangara iliamriwa baada ya mjadala mkali sana Waislam watoke kwa maandamano hadi Kituo Cha Kati Cha Polisi kwenda kuwatoa masheikh wao korokoroni.

Katika maandamano yale Waislam walipambana na polisi na mabomu ya machozi yalipigwa.

Mapambano haya yalifanyika kati ya kituo cha polisi na Clock Tower.
Haya ndiyo yalikuwa maandamano ya kwanza ya Waislam Tanzania Bara.

Zanzibar maandamano yao yalikuwa mwaka wa 1988.
Maandamano haya yote tatizo ni Uislam.

Hassan Chikusa akakamatwa pamoja na vijana wengi wa Kiislam.
Wakawekwa rumande wakashtakiwa na kuhukumiwa vifungo jela.

Hassan Chikusa akapoteza kazi yake NBC.

Huyu ndiye Hassan Chikusa msomi mkimya ambae baada ya kutoka jela akiwa hana kazi masahibu mengi ya maisha yalimfika.

Lakini siku zote akisema yaliyomfika ni madogo sana na yote ameyakadiria Allah na na yeye bado yu hai.

Kwangu mimi maadamano yale na wale walioshiriki katika yale maandamano kile kilikuwa kipimo.

Tunamuomba Allah amsamehe makosa yake mja wake huyu na amtie Firdaws.
Amin.

View attachment 2305229
Hassan Chikusa​
We jamaa ni hazina
 
Back
Top Bottom