TANZIA Buriani Mama Tumaini Kakuyu Mlewa, Mpambanaji hodari, mwasisi wa shughuli za usafi maofisini na upambaji wa kumbi za mikutano, sherehe nk

TANZIA Buriani Mama Tumaini Kakuyu Mlewa, Mpambanaji hodari, mwasisi wa shughuli za usafi maofisini na upambaji wa kumbi za mikutano, sherehe nk

Jemima Mrembo

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
2,864
Reaction score
8,328
Screenshot_20210808-233319.png


Tumaini Kakuyu Mlewa alikuwa ndiye mtu wa Kwanza kuwa na kampuni professional ya usafi akichukua tenda kwenye ofisi za makampuni mbalimbali, mahospitali viwanda nk kupitia kampuni yake ya Fame Consolidated Services LTD.

Pia aliasisi shughuli za upambaji wa kumbi za starehe, mikutano etc.

Huyu Mama hakuwa mwanasiasa, ila wajasiriamali tunamlilia sana.

Mungu mpokee
 
Safi sana. Duniani kila mtu ameletwa na mungu kwa sababu.

Unavyoondoka duniani huku umeacha legacy inapendeza sana.

Huyo mama kifo chake ni sherehe ya kweli. Maana hana deni na dunia
 
Aliyeuliza nazani anamaanisha labda kudhulumu wafanyakazi, malipo madogo huku yeye anaingiza parefu nk
Nimefanya kazi kwenye kampuni yake kwa zaidi ya miaka kumi, hatukuwa na mahusiano ya damu. Wala hakuwa ndugu yangu kabisa, lakini huyu Mama hakuwahi kumuacha mtu aangamie.

Mishahara haikuwa mikubwa, pia mishahara haikuwa kidogo, kampuni yake ilikuwa kioo kwa malipo mazuri kwa kampuni za usafi.
Nilianza kazi kwake nikiwa nimemaliza form four na div 4 ya point 26 mwaka 1998.

Akanishauri nijiendeleze kielimu, nikamwambia Mimi nasomesha wadogo zangu.

Akanipeleka Mwenge Mzumbe QT, kwa gharama zake nikarisiti na kupata div 2.

Kwangu ilikuwa nu furaha kubwa na huzuni pia, nikijiuliza wadogo zangu wawili watasomaje?

Huyu Mama hakuwajua ndugu zangu, lakini alitusomesha wote watatu.

Tunaposema huyu Mama ni mfano muwe mnaelewa.

Hajabadilisha maisha yangu tu, ila ya watu wengi pia.

Zaidi ya wamiliki 85% wa makampuni ya usafi amewasaidia kwa namna Moja ama nyingine
 
Umejuaje hana deni na Dunia maana sie binadam hakuna aliye mkamilifu..😭
Ukisoma ufunuo 14:13 unasema maana matendo yao yafuatana nao.

Ufu 14:13​

Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao
 
Nimefanya kazi kwenye kampuni yake kwa zaidi ya miaka kumi, hatukuwa na mahusiano ya damu. Wala hakuwa ndugu yangu kabisa, lakini huyu Mama hakuwahi kumuacha mtu aangamie...
Basi na wewe una deni!
 
Nimefanya kazi kwenye kampuni yake kwa zaidi ya miaka kumi, hatukuwa na mahusiano ya damu. Wala hakuwa ndugu yangu kabisa, lakini huyu Mama hakuwahi kumuacha mtu aangamie...
Mungu amlaze mahali anapostahili.. Such a beautiful soul
 
Back
Top Bottom