Aliyeuliza nazani anamaanisha labda kudhulumu wafanyakazi, malipo madogo huku yeye anaingiza parefu nk
Nimefanya kazi kwenye kampuni yake kwa zaidi ya miaka kumi, hatukuwa na mahusiano ya damu. Wala hakuwa ndugu yangu kabisa, lakini huyu Mama hakuwahi kumuacha mtu aangamie.
Mishahara haikuwa mikubwa, pia mishahara haikuwa kidogo, kampuni yake ilikuwa kioo kwa malipo mazuri kwa kampuni za usafi.
Nilianza kazi kwake nikiwa nimemaliza form four na div 4 ya point 26 mwaka 1998.
Akanishauri nijiendeleze kielimu, nikamwambia Mimi nasomesha wadogo zangu.
Akanipeleka Mwenge Mzumbe QT, kwa gharama zake nikarisiti na kupata div 2.
Kwangu ilikuwa nu furaha kubwa na huzuni pia, nikijiuliza wadogo zangu wawili watasomaje?
Huyu Mama hakuwajua ndugu zangu, lakini alitusomesha wote watatu.
Tunaposema huyu Mama ni mfano muwe mnaelewa.
Hajabadilisha maisha yangu tu, ila ya watu wengi pia.
Zaidi ya wamiliki 85% wa makampuni ya usafi amewasaidia kwa namna Moja ama nyingine