Buriani Rashid Mbuguni, Mzalendo aliyedhulumiwa kiwanda amekufa hajaona haki

Sasa si bora huyo fisadi anayetoa visent kwa walala hoi... hao ambao si mafisadi wamewafanyia nini walala hoi?
Tufanye mfano pm Majliwa si fisadi, hadi sasa kawafanyia nini walala hoi??
Tatizo la Masikini wengi huwa hawapendi kujua upande wa giza wa tajiri,hata Kama anauuza viuungo vya Binaadamu wao hawajali,na wanacho angalia wao ni ule msaada wanaopata kutoka kwa Mafisadi!!
 
Daah umeongea kwa uchungu sana Mkuu pana watu walikufa wale waliopokonywa hela za kwenye maduka ya kubadilishia fedha wengine walikopa nilishangaa eti pana kikosi kinalazimisha kuchukua hela zote zilipo kwenye hilo duka mpaka wale walioacha fedha kwenda kuchukua nao walikuatana na huo mziki nadhani pana wale wakamataji nao walipata kitu kwa dhuluma ni vile hii Nchi vitu vinaisha tuu wangeunda Tume kuchunguza ule unyang'anyi tungepata kitu...
 
Mkuu, namnukuu mtu mmoja hapa.

Anasema kuna mfanyabiashara mmoja alikuwa na deals zake ku supply nyama kwenye mahoteli. Alikuwa na shilingi bilioni 4 benki. Magufuli akazikomba zote. Jamaa mpaka leo kachanganyikiwa anaongea mwenyewe njiani, karudi kuajiriwa.

Kuna wafanyabiashara kibao wamefanya biashara za mazao miaka na miaka, Magufuli kaja kakomba hela zao zote.

Halafu, hizo hela na zile za plea bargaining, zimeingia katika akaunti binafsi, si akaunti za serikali. Hili hata Samia kalisema.

Sasa mpaka hapa hatuoni U Mafia wa Magufuli tu?

Mpaka leo, Magufuli ameangusha sana imani kwenye banking system ya Tanzania.

Halafu watu wanajitoa akili kumsifia?
 
Kuna watu wakifa roho zao huwa zinatangatanga,zinahangaika maana huwa zinashindwa kupokelewa na aliyeziumba kutokana na mabaya walio wafanyia wenzao
 
Luqman ni lichawa, halijabalance stori
 
Hakuna cha ushetani mijizi mikubwa nyie.

Magufuli hajawahi kumwandama mtu bila sababu, huyo Luqman hana ajualo upande wa pili

Wapuuzi wakubwa
 
Likaunganishwe na bandari...Maana Mama anasema ana mitihani migumu sana
Huyo mama mtansingizia kila kitu, watoto wa singo mother" ndivyo mlivyo.

Mama mwema hakimbii lawama, huzitatuwa ajuwavyo kama mama.

Hata "kama" alisema hivyo, Ma Shaa Allah huo ndiyo Uislam.
 
Kwa ufupi, Mengi, E. Massawe, Mbuguni na Nyaulawa walikua National Auditing kwa wakat mmoja na inasemekana utajiri wao waliutoa huko haswa kipindi cha maandalizi ya zoezi la ubinafsishaji.
 

Usitumie nguvu unajua mtu hawezi from no where achukue pesa ya mtu bila sababu, mi mwemyewe kuna nyumba yetu ilipitiwa na hayati kipindi cha upanuzi wa barabara ya morogoro, niliumia sana ila hua simlaumu maana kiuhalisia mzee wetu alikula sehem hifadh ya barabara ili kujenga shule siku za usoni so kuna hisia na hualisia wa jambo.

Mi nafikiri mnapokua mnasema vitu vibaya alivyofanya kuweni waungwana mseme na sababu zilizomfanya kufanya vile ziwe nzuri ama mbaya, naamini hakua chizi kuzichukua izo fedha labda kama ni wasadizi wake ndani ya serikali yake na sio yeye.
 
Ungesema sababu ningekuelewa ila kwa vile una chuki na hayati na hata ulichoandika hapa ni upuuzi mtupu dogo...

Kwani hayati alikula ule mtandao damu moja na zantel?
 
Unatetea vitu usivyovijua kwa logical non sequitur na mahaba uliyo nayo kwa Magufuli.

Kama nyie mmebomolewa nyumba iliyokuwa kwenye hifadhi ya barabara kwa uzembe wenu, hilo halina maana kwamba hakuna watu waliofanyiwa u Mafia bila sababu za msingi.

Magufuli alikuwa na sababu gani za kutaifisha mitambo ya Business Times zaidi ya kutaka kuminya uhuru wa habari tu?

Alikuwa na sababu gani?

Na kwa nini hela alizokuwa anachukua, kama za okea bargaining na za Bureaus, alikuwa anaweka katika akaunti binafsi ambazo hata serikalini hazijulikani?
 
Acha kutetea upumbavu. Kama hukuwa na hela wakati wa Magu huwezi kuelewa kinachozungumzwa. Huyo mzee hakuwa na urafiki akiona akaunti imenona. Ubaya ni kuwa alikuwa haangalii sura CCM sijui CHADEMA akiona mpunga tu anakomba. Ilifika wakati kama unadaiwa kodi na akaunti ina hata 20m wanaikomba bila hata kukujulisha. Maskini peke yao ndo hawaujui muziki wa roho mbaya iliyokuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…