Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
View: https://youtu.be/GxN6WSDDIF8?si=6EyFTUpKptlgFoEm
Huko ni Burkina Faso.
Kutokana na fedha alizoziokoa, Capt. Ibrahima amenunua matrekta 5,000 na kuyagawa kwenye vijiji vya Burkina Faso. Ameweka lengo la kutonunua chakula kutoka nje katika miaka mitano ijayo, pia kutengeneza asilimia 60% ya nguo zote nchini (Tujilishe na tujivishe wenyewe).
Na kwa vile nchi hiyo inakabiliwa na uasi uliopangwa na Ufaransa kwa sababu ya kuchukua rasilmali za nchi hiyo (kumbuka Congo), Cap. Ibrahim aliwafukuza wanajeshi wote wa Ufaransa nchini mwake na sasa vita vya kukomboa maeneo yanayoshikiliwa na waasi, wanapigana Waburkinabe wenyewe.
Baada ya majeshi ya Ufaransa kusua sua kwa miaka mingi wakidai waasi wana silaha kali, sasa jeshi la Burkinabe limeanza kurudisha ardhi yake.
Leo hii amekomboa eneo muhimu lenye machimbo makubwa ya dhahabu lililokuwa linashikiliwa na waasi.
Amefanikiwa kufanya hivyo baada ya kununua vyombo vya kisasa vya kijeshi, vifaru na magari ya deraya, zikiwemo drone 20 kutoka China, Iran...na drone zinazosifiwa zaidi kutoka Uturuki za Akinci ambazo zina uwezo wa kugundua na kuwaangamiza waasi hata saa nane za usiku, hata wakiwa wamejificha chini ardhini, kwa kutumia miali ya laser ya kuangaza (infra red).
Sidhani kama Bongo tuna zana hizo, ingawaje tuna uchumi almost maradufu ya BF. Ni uaminfu, uzalendo, akili na upangaji (vitu ambavyo hatuna).
Nikisoma hivi nalia kwa uchungu na hasira. Acha nisiendelee nisije nikatukana! Kweli matatizo yetu makubwa ni uongozi mbovu. Huyu kijana wa miaka 34 ameigeua nchi kabisa katika miaka miwili tu.
Dhahabu yote ya BF inachimbuliwa, kusafishwa na kuuzwa na Waburkinabe wenyewe. Hata baadhi ya mashine za kufanya hivyo zimebuniwa na kutengenezwa na Waburkinabe wenyewe! Amekwisha nunua mashine za kupanda, kuvuna, kuondoa mbegu na kusuka pamba...katika miaka hiyo.
Ukosefu wa kazi umepungua kwa asilimia 4 katika miaka hiyo miwili tu. Na sasa amepunguza mshahara wake na Mawaziri kulipia maendeleo.
Bado anatembelea Isuzu 2018!