Burna Boy ni zaidi ya Wizkid na Davido kwa sasa?

Zote achana nazo nenda Ghana kuna viumbe wawili wanajiita R2Breez walimpa Verse moja na Chorus apige ngoma inaitwa To Night. Bro ni nomaaaaaaa



Kama una sabufa sikilizia humo uone unyama wa Kidayo
Nilitaka nikutajie io ngoma kaanza verse na kaua chorus.....Tunatembea kwenye fikra sawa....Wiz kid ni moto
 
Naomba utupostie huo wimbo maana siuon YouTube
 
Nigeria's new generation music hii ya kuchezeka tu. wanaija Walikuwa wakiita hivyo wakati inaanza kuendesha music industry yao
Kwenye album nzima ya African giant nyimbo zinazochezeka Tu hazizidi nne .

Nyingine zote pure African
 
Kwenye album nzima ya African giant nyimbo zinazochezeka Tu hazizidi nne .

Nyingine zote pure African
Shukrani mkuu pamoja na waliopita. Ngoja niende kuzisikiliza maana hitz zote naona ni club banging. Ngoja nimuweke katika list
 
Hapo ndipo wabongo tunakosea ... Siko hapa kusema Nani Ni mkali zaidi ya mwingine... Niko hapa kutoa shout Out kwa Burna Boy...

Mindset hizi ndizo zinafanya mziki wa bongo hauendi beyond the limit.
Hapo Gud. Burna namuheshimu. Lkn Wiz na Davido Two Legends. Heshima kwao.
 
Matamasha mawili yaliyopangwa kumshirikisha mwanamuziki nyota wa Nigeria huko nchini Afrika Kusini Burna Boy yamefutwa kufuatia "kuongezeka kwa vitisho vya ghasia.

Burna Boy alitarajiwa kutumbuiza katika tamasha la Africa Unite na mpango ulikua pesa itakayopatikana isaidie waathirika wa #xenophobia Afrika Kusini, lakini waandaaji wanasema matishio ya kufanyika fujo yaliongezeka hivyo wamelazimika kufuta tamasha.

Taarifa zinasema kuwa simu nyingi zilipigwa na raia wa nchi hiyo wakitaka Burna Boy aombe radhi kwa kauli yake aliyoitoa wakati mashambulizi ya hivi karibuni ya #xenophobia yalipofanyika ambapo msanii huyo alisema hato tua mguu wake nchini Afrika Kusini na kutaka wanao shambuliwa toka mataifa mengine wajilinde.

Kuna haja ya waafrika kuvutana au kupigana wenyewe kwa wenyewe?
 
Baada ya Xenophobia Burna alikataa hataenda south ... Wao ndio walimfuata kwa kumpa dau kubwa ila alikataa hataomba msamaha hajafanya kosa lolote.. Yaani wao wawaue wanaijeria na aombe msamaha..Alikataa.
 
Angalieni Album Ya Burna ilivyosukwa ... Halafu mtu haogopi kwanini Jamaa katajwa Grammy... Mtu anadhani Grammy Ni Kilimanjaro music awards
 
Huyo mwamba mwimbo wake wa 'on the low' popote utakapopigwa lazima nipoteze concentration ya jambo nililokuwa nalifanya,jamaa anajua mno.

Ila Starboy,ni mtu mwingine kabisa,hakuna cha Davido wala tiwa and the likes
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…