Hii ni ishara tosha kwamba sasa TLS ni tawi la chadema, na lazima wakisema jambo lolote, tujue wametumwa na chadema, linatakiwa lichukuliwe kisiasa, na kujibiwa kisiasa, na ikibidi kukwamisha chochote kitakacholetwa na TLS kwa kuwa ni mdomo wa chadema
TLS kuwa tawi la Chadema ni hasara kwao mana chadema hawana mapesa na nafasi za kuteua majaji . Nadhani CCM na serikali yake wanapoteza uungwaji mkono kutoka kwa Wakulima na wafanyakazi .
Amni ,amni nakuambia hata majeshi yote yangepiga kura kwa siri kuwachagua wakuu wao hakika wale wanaoungwa mkono na CCM na serikali yake wasingepata nafasi za juu mana mateso na shida zao zinatokana na CCM kushirikiana na wezi lutengeneeza mitandao ya kifisadi bila kujali maisha ya watu wa Chini kama ilivyokuwa imeundwa kuwa chama cha wakulimma na wafanyakazi.
CCM sasa ni chama cha wezi na mafisadi.
Wanashera wengi ni watoto wa wakulilma na wafanyakazi.
Moto umewaka na hali hii iko nchi nzima watu wamefurahi sana ushindi wa Mwabukusi.
Natamani pangetokea chama kingine nje ya vilivyopo halafu Waungane wapigania haki ,usawa ,rasilimali za umma na Maendeleo ya Watu wote haki. Wawepo akina Mpina, Mwabukusi, Manamapinduzi, Mbariwa, Tundu Lisu , Heche n.k.
Vyama vilivyopo vinapigania maslahi ya watawala au viongozi wao na kupata fursa za kujitajirisha na kushika uchumi binafsi kwa kushindana na mabilionea waliopo duniani kupitia rasilimali za nchi.