Burudani ya soka bila EPL

Burudani ya soka bila EPL

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
Kumbe unaweza kuburudika kwa kutazama futbol bila hata mechi za EPL.

Binafsi nilikuwa natamani sana EPL ingekuwemo kwenye king'amuzi cha Azam lakini ndiyo hivyo tena.

Pamoja na kukosekana kwa EPL ndani ya Azam, lakini kwa sisi wapenda soka, angalau nafsi inaridhika kwa kutazama mechi live ndani ya Azam-Serie A, Laliga, Bundesliga, Carabao Cup na baadhi ya mechi za EPL mfano leo ilioneshwa ya Leicester vs Aston Villa.

Aloo! Huko Italia mpira unapigwa jamani.

Azam tegueni mtego mliowekewa wa kuonesha EPL. Mkifanya hivyo tayari mtakuwa wafalme rasmi wa burudani ya soka Tanzania
 
Hashimu Ibwe una mbinu nyingi sana za kuitangaza azam.
Hapana. Ni mimi mdau mmoja fulani hivi. Soma post zangu za nyuma ndio utajua siyo Hashimu Ibwe.

Kiukweli nilihamia Azam kwa ajili ya ligi ya bongo. Sasa taratibu nazoea mbugi zinazopigwa huko Ujerumani, Spain na Italia.

Muda si mrefu imemalizika mechi kati ya Lazio na AC Milan. Yaani Lazio walipelekewa moto na kutanguliwa goli moja mpaka kipindi cha kwanza kinaisha. Nikajua tayari Lazio wamekubali unyonge.

Kipindi cha pili, Lazio wakaja moto na kusawazisha na kuongeza ikawa 2-1. AC Milani nao wakaongeza moto na kupata goli game ikaisha 2-2.

Mpira ni wa ushindani haswa huko Italia.
 
Ila azam waongeze chanel za mpira bad hazitoshi mechi nyingi hawazirushi
Ni kweli. Yaani kama wikendi ya jana wamerusha mpaka kupitia UTV, palikuwa pamechangamka haswa. Wao waongeze channel na wajitahidi waoneshe EPL hapo watakuwa wamemaliza kazi.
 
Barcelona itakuja kuwa tishio ulaya na Dunia nzima, Ina vijana wengi wadogo U20 na wanashambulia kama nyuki.
Nafurahi sana kwa sasa barca tumeanza kurudi kama mwanzo na bila uwepo wa messi tumekubali maisha

Hawa vijana watakuja kusumbua sana chamsingi tusibadili makocha hovyo

Kule Madrid wamejaza mastaa sana kiasi kwamba hakuna maelewano
 
Ni sawa lakini tunajivunia mpira duni sana. Wenzetu hata ukiwafunga 2 mpaka dakika za 80 unashangaa wana equalize na kuongeza la ushindi.

Hiyo ndiyo kandanda ya ushindani.
Tunajivunia tulicho nacho mkuu, ukienda ghana, nigeria huko wanatamani kuwa kama sisi. Maaana wao weekend mechi za ulaya watu wapo katika screen soka lao la ndani mashabiki wa kuhesabika
 
Nafurahi sana kwa sasa barca tumeanza kurudi kama mwanzo na bila uwepo wa messi tumekubali maisha

Hawa vijana watakuja kusumbua sana chamsingi tusibadili makocha hovyo

Kule Madrid wamejaza mastaa sana kiasi kwamba hakuna maelewano
Madrid kwa hizi mechi za mwanzo limecheza jina lao tu. Uwezo mdogo na hakuna muunganiko wa kitimu.

Moto wa Barcelona ni hatari Mzee! Hawakupi chance ya kuutumia mpango kazi wa kocha wako😂😂😂

High pressings na mashambulizi ya kutokea pande zote ( pembeni, na katikati)
 
Kwakweli Azam Tv Wamefanya la maana sana kuonyesha mechi za ligi 6 siyo kazi ndogo, sahivi mechi kali zote za Bundesliga, Laliga, serie A , ligi ya kina CR7, League 1 ya France na NBC zote unaziona jana nilikua naangali game kali ya Barcelona ila Tanesco wakakata umeme ulivyorudi mtu kashachapwa chuma 7 safi
 
aisee ni kwa kif7rushi cha tsh ngapi unacheki ligi zote
 
Back
Top Bottom