Burundi yaongeza wanajeshi Kivu Kusini

Burundi yaongeza wanajeshi Kivu Kusini

Hapa nahisi harufu ya jeshi la nchi furani likizunguuka kupitia Kivu kusini na kuipa company RED-TABARA. Na Hapo mpaka Bujumbura pafupi sana
Tpdf ikitazama tu hili, itakua hatari kwa bandari ya dar,hivyo uchumi wa tz,ukizingatia kuna reli inataka jengwa mozambique-zambia
 
Ikiwa wazi hivyo basi mda si mrefu na wale wa upande mwingine watafanya waziwazi bila kificho kama sasa
je nan atakuwa kawaruhusu hao wanajeshi w bwana Slim ? Burundi wwna terms ba DRC
 
Rwanda haina uwezo wa kuipiga Burundi, hilo hata Rwanda wanajua.
Rwanda kwa ukanda huu huwezi kuibeza kwa sasa, mission zake huko Msumbiji ,CAR zinajieleza.

Japo hapo Drc imelipa gharama kuiteka Goma....ila kuiteka Goma katikati ya majeshi 20,000 kutoka UN na SADC sio kazi ndogo.

Burundi wana wanajeshi mpaka Somalia
Wakati mwingine wingi wa wanajeshi hauashilii ushindi wa vita. Japo huko walishatolewa.

Hujasikia Burundi ikilalamikia Somalia kupunguza idadi ya warundi na kuongeza waganda? Hii EAC ina unafiki mkubwa
 
Rwanda kwa ukanda huu huwezi kuibeza kwa sasa, mission zake huko Msumbiji ,CAR zinajieleza.

Japo hapo Drc imelipa gharama kuiteka Goma....ila kuiteka Goma katikati ya majeshi 20,000 kutoka UN na SADC sio kazi ndogo.

Hapo taarifa zikiwa za kweli ndo watu wanapigana mfumo wa hatuna la kupoteza, na hakuna cha mazungumzo wala nini, mpaka tufikie tunachokitaka.
 
Rwanda haina uwezo wa kuipiga Burundi, hilo hata Rwanda wanajua.
Aisee hili nililisema kuna jamaa lilibweka vibaya mno ,nikamwambia Mrundi ni mpiganaji mzuri sana na kona zote hizo nae anazijua lakini pia hana maadui wa ndani wa kivile kama ilivyo kwa Pk,

Ambapo kwa vyovyote vile Chigali ikianza kupigwa direct wataibuka watu wengine hatutajua wametoka wapi kumshindilia vizuri Pk
 
Burundi inajitahidi
Nchi ya Burundi, inayohusika na vita vinavyoendelea mashariki mwa Congo, kupitia makubaliano ya ushirikiano kwa mambo ya kisalama, kuanzia Septemba 2023, na hili jambo liliifanya Burundi kuwa mshirika mzuri kikanda. Burundi imeweza kupeleka nchini Congo wanajeshi wapatao elfu 10 kulisaidia jeshi la FARDC kukabiliana na M23, waasi wanaoungwa mkono na Rwanda.

Kwa siku mbili sasa, kikosi cha 22, kinakusanyika mpakani Gatumba, kwa maandalizi ya kuingia Kivu kusini. Hili litafanya vikosi 16 vya jeshi la Burundi kuwa nchini DRC,ambapo inakadiliwa watakuwa kati ya elfu 8 na elfu 10. Wanajeshi hao watakuwa na kazi ya kulinda barabara zinazoingia Bukavu mjini, lengo likiwa kuzuia M23 kuingia mjini humo.

Source RFI/Afrique

Hili linafanyika wakati nchi za SADC zinajiandaa kuondoa wanajeshi wake nchini humo, kuanzia Malawi iliokwishatoa Tangazo, Afrika kusini na yenyewe ilionesha nia ya kuwaondoa wanajeshi wake.
 
Hivi, kweli inawezekana raisi wa nchi apeleke wanajeshi elfu kumi vitani nchi nyingine? Hapa kuna watu wanaenda kupimana uwezo si bure.
Unapeleka. Wenzetu hao washazoea mikimiki hivyo Wana vikosi ready.

Nawaza hivi Rais wa Congo DRC alivyoingia madarakani alishindwa kweli kuunda Jeshi pale mwanzoni.

Wataalamu wapo humu. Inachukua muda Gani kumpika Mwanajeshi akaiva kabisa kabisa. Yaani kuanzia 0 anapovuliwa uraia Hadi awe let say commando.

Hivi alishindwa kweli???!!???

Unatakaje madaraka kwenye nchi kama DRC halafu huna plan na unajua hapo ni muda wowote wanakiwasha.

Namsapoti Tshisekedi kimawazo na kimatendo lakini namwona ana kasoro za viongozi wengi wa Afrika, Kung'ang'ania vitu usivyoviweza. Kama Mama Fulani anavyokazania kuongoza Boma.

Plan nzuri ilikuwa akiingia madarakani anaivuta Tanzania, South Africa, Zimbabwe and the like kisha anaomba wamsaidie kuunda kikosi kazi yaani special force ya kupigana na waasi tu wakati wanajeshi wengine wakilinda mipaka.

Angelipa nchi hizo hata kwa dhahabu. Sasa ivi angekuwa na Jeshi.

Anyway, vita sio nzuri tuiombee CONGO DRC.
 
Aisee hili nililisema kuna jamaa lilibweka vibaya mno ,nikamwambia Mrundi ni mpiganaji mzuri sana na kona zote hizo nae anazijua lakini pia hana maadui wa ndani wa kivile kama ilivyo kwa Pk,

Ambapo kwa vyovyote vile Chigali ikianza kupigwa direct wataibuka watu wengine hatutajua wametoka wapi kumshindilia vizuri Pk
Burundi ikiamua kuingia vitani na Rwanda inawaleta FDRL ambao huwa inawafundisha na kuwajumuisha vitani, na wao ni wengi na wana impact kubwa kuliko waasi wa Burundi watakaoungwa mkono na Rwanda.

Burundi ni wapiganaji wazuri, hata majambazi wao wamekubuhu achana na majambazi uchwara ya Tanzania yanayoishi Sinza. Jambazi mmoja wa Burundi anaendesha mji mzima unateseka kwa miezi kadhaa.

Hamna kitu Rwanda wanafanya alafu Burundi hawawezi pale DRC. Kupigana misituni ndio jadi yao. Tofauti yao ni silaha kidogo Rwanda wanazo nyingi ila vita ikitokea hamna mshindi pale. Na Rwanda haiwezi jichanganya.
 
Unapeleka. Wenzetu hao washazoea mikimiki hivyo Wana vikosi ready.

Nawaza hivi Rais wa Congo DRC alivyoingia madarakani alishindwa kweli kuunda Jeshi pale mwanzoni.

Wataalamu wapo humu. Inachukua muda Gani kumpika Mwanajeshi akaiva kabisa kabisa. Yaani kuanzia 0 anapovuliwa uraia Hadi awe let say commando.

Hivi alishindwa kweli???!!???

Unatakaje madaraka kwenye nchi kama DRC halafu huna plan na unajua hapo ni muda wowote wanakiwasha.

Namsapoti Tshisekedi kimawazo na kimatendo lakini namwona ana kasoro za viongozi wengi wa Afrika, Kung'ang'ania vitu usivyoviweza. Kama Mama Fulani anavyokazania kuongoza Boma.

Plan nzuri ilikuwa akiingia madarakani anaivuta Tanzania, South Africa, Zimbabwe and the like kisha anaomba wamsaidie kuunda kikosi kazi yaani special force ya kupigana na waasi tu wakati wanajeshi wengine wakilinda mipaka.

Angelipa nchi hizo hata kwa dhahabu. Sasa ivi angekuwa na Jeshi.

Anyway, vita sio nzuri tuiombee CONGO DRC.
Unajua lakini Tshisekedi ni mtoto wa nani? Huu uongozi wa kurithi nao shida.
Then, watu walishaisha mapolini miaka nenda rudi, washakuwa kama wanyama, unaanza kuwaelekeza cha kufanya.
 
Watu humu wanaichukulia poa burundi yenye backup ya TZ katika nyanja za kijeshi
Achana na backup ya Tanzania. Ikitokea Burundi na Rwanda zinapigana Tanzania itakuwa neutral.

Burundi inajua kupigana na wanapigana kimyakimya hawana mbwembwe na makelele. Na ubaya wa hizi nchi ni kwamba kuna chuki ya makabila mawili majority kwenye majeshi yao. Burundi wanajeshi wengi Wahutu, Rwanda wengi Watutsi. Hapo huhitaji kuwapa motisha morali wanayo wenyewe.

Pia Burundi inaongozwa na Jenerali mwenye baraka za kikatiba na population nzima (uchaguzi wake relatively ulikuwa wa haki na alishinda kwa wingi) Rwanda anangoza mwanajeshi ambaye anaishi kwa mkono wa chuma, rally na support wakati wa vita Ndayishimiye anayo kubwa kuliko Kagame.

Kwenye masuala ya vita, Rwanda wana RPF kama chama tawala kilichotokea msituni. Burundi wana CNDD-FDD chama tawala kilichotokea msituni na hawa kina Ndayishimiye walikuwa viongozi wa waasi. Kagame anawatishia mabwege wengine ila hana cha kuwatishia Burundi.
 
Rwanda kwa ukanda huu huwezi kuibeza kwa sasa, mission zake huko Msumbiji ,CAR zinajieleza.

Japo hapo Drc imelipa gharama kuiteka Goma....ila kuiteka Goma katikati ya majeshi 20,000 kutoka UN na SADC sio kazi ndogo.

Lini ulisikia M23 wamepigana na UN forces?
SADC umeona kuna vita wamepigana pale? JWTZ wameenda umesikia engagement yoyote au ni ambush za hapa na pale.

Majeshi mengi yanakuwepo DRC sio kwa ajili ya intervention bali kulinda amani na kupiga gwaride tu kupoteza muda. Wanaopigana ndio kama hawa Burundi wameenda.

SADC nchi wanachama wote 16 waliopeleka majeshi ni Malawi, Tanzania na South Africa na tena wamepeleka idadi chini ya kiwango.

Nilikuwa natamani South Africa wakasirike alafu wasielewane na Rwanda kidiplomasia wafanye reinforcement DRC ungeona jinsi Rwanda wana jeshi la kawaida.

Kati ya wote waliopo Eastern DRC, wenye sababu za kupigana ni DRC ambaye ni mchovu kijeshi, M23 ambao wanazo sababu na Rwanda. Usitarajie eti Malawi au Tanzania wapigane kwa motivation sawa na Rwanda.

Msumbiji kule Rwanda iliitwa na France kulinda invesment ya Total na ilipewa means za kwenda, na pia Msumbiji yenyewe iliilipa. Tanzania tulienda for securing our border na tulifanikiwa hilo. Wao wanapenda PR na propaganda, majeshi mengine hayapendi media attention.

Wanaweza, ila uwezo wao kiuhalisia ni wa kawaida. Hawana level za kuifanya Burundi ilale bila usingizi.
 
Back
Top Bottom