Burundi yatuma kikosi cha waokoaji Uturuki, nimejifunza kutoa ni moyo

Tunambwela mbwela tu.

Hamna lolote la maana linafanyika awamu hii.

Maneno meengi fedha zinakopwa hakuna Kinachofanyika.
 
Hata ameweza kumaliza ugomvi na RWANDA pia ,wako vizuri na congo pia ,kiufupi yuko poa

USSR

Kabisa kwa Zamani isingewezekana Kagame aende Bujumbura, Burundi anajipambanua kivingine hasa kwenye demokrasia na kwa sasa Burundi ina uelekeo tofauti na zamani kabisa
 
Mkuu Burundi wamewekeza kwenye human resources kwa sana, wakifuata nyayo za Rwanda. Kuna idadi kubwa ya wataalamu waliosoma na kubobea kwenye fani walizozichagua makusudi. Mfano kuna idadi kubwa ya makocha wenye elimu inayotambulika kimataifa. Kutuna wataalamu wa uokozi ni moja ya hazina ya uwekezaji huo ikiwemo matumizi ya jeshi lao kwenye migogoro. Tanzania hatuna chuo wala maandalizi ya wataalamu wa uokozi, kumshambulia Stergomena Tax kwenye hili la warundi kutuma timu ya uokozi Uturuki ni kumuonea. Labda tungeanza kwa kunyesha mfano kwenye ile ajali ya Precision Air pale Bukoba, huenda tungeweza kujipima na watu waliokwisha wekeza kwenye nyanja hiyo.
 
Waokoaji walishindwa kuokoa raia kwenye Ndege ya Precision Air ndo wakaokoe wa Tetemeko,sisi Bado tunaupiga mwingi .

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Kabisa kwa Zamani isingewezekana Kagame aende Bujumbura, Burundi anajipambanua kivingine hasa kwenye demokrasia na kwa sasa Burundi ina uelekeo tofauti na zamani kabisa
Sana warundi sasa wameamua kujenga nchi

USSR
 
Nikajua una pointi, kumbe pumba tu. Uoakoaji sio siasa na sio UN General Assembly.
 
Watanzania ukiwapeleka huko,badala waende kuokoa watu,wataenda kuwasachi tu marehemu na kuwaibia.hiyo ndiyo tabia ya Mtanzania.
 
Waliokwisha kwenda huko wanatosha sio lazima na sisi twende!
 
Unataka serikali itumie pesa ya mkopo kupeleka waokoaji Uturuki?
 
Aiseee kwa hiyo shida yako kwa Tax ni Burundi kutuma waokoaji Uturuki? Kichwa chako kiko vizuri kweli? Tumeshindwa Bukoba, tutume Burundi?
 
Serikali ya bongo imewekeza zaidi kupambana na chadema,kwengine kote ni bora liende.
Sasa hivi kwenye serikali kuna watu wamejiandaa kupambana internet ya starlink isifike TZ kivyovyote vile kama walivyopambana kuiondoa paypal
 
Ni ngumu sana kwa ombaomba kutoa msaada, hata ule wa kutumia nguvu na akili tu hawezi.
 
Hakuna walichotuzidi wala cha kulilia. Acha wafu wazike wafu wenzao. Hawa jamaa unadhani yangetupata sisi wengejali? Burundi kinatafuta kiki tu
 


Sisi kama Tanzania tuna kitu cha kujifunza hapa. Picha chini Rais wa Burundi General Évariste Ndayishimiye

Mimi nimejifunza kifuatacho ongeza chako;

1. Kutoa ni moyo uzambe ni utajiri

======

Bujumbura. Kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lilioikumba nchi za Syria na Uturuki lililosababisha vifo vya watu zaidi ya 28,000 na uharibifu mkubwa, Serikali ya Burundi imeamua kutuma timu ya watu 10 kwenda kusaidia uokoaji.

Hii imekuja kama hatua ya mshikamano na watu wa Uturuki waliokumbwa na matetemeko makubwa ya ardhi tangu Jumatatu na kusababisha maelfu ya watu kupoteza maisha.

"Wakati wa kuwasili, timu itatumwa na mamlaka ya Uturuki katika maeneo ambayo wanaihitaji zaidi," amesema Albert Shingiro, waziri wa mambo ya nje wa Burundi ameliambia shirika la habari la BBC siku ya Jumapili.

Shingiro amesema,“hakuna raia wa Burundi aliyeathiriwa, na Sabria Samir Kaze ambaye alikuwa katika mji wa Gaziantep, uliokumbwa vibaya na tetemeko la kwanza alihamishwa hadi Ankara.”

Burundi haikutuma waokoaji Syria kwa sababu ni vigumu kufikia maeneo yaliyoathiriwa hata hivyo, serikali inasema inawahurumia watu wanaoteseka huko nchini Syria.

Mwananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…