Kuna bus moja huko kanda ya ziwa sitalitaja ila sipandi tena kutokana na kutuona abiria ni wajinga.
Baada ya kukuta kampuni niliyoizoea kujaa nikaenda kampuni nyingine nikaambiwa imebaki VIP na nikatajiwa nauli ambapo inaongezeka elfu 15 kutoka ile ya kawaida. Nikawauliza kuna huduma gani za ziada wakaniambia kuna choo, Azam TV, msosi na Internet basi nikaona hii nzuri, nikalipa .
Kufika muda wa kusafiri kuingia ndani nikaona seat ziko tu kama za kawaida, baada ya muda tukaunganishwa Wi-Fi speed ya kobe, hakuna cha choo wala nini na tukawa tunasimama kwenye kuchimba dawa mavyoo ya nje . Wakazidi kutuona abiria ni wajinga kwa kutugawia biskuti za sh.mia na pipi mbili.
Kwa nini msiwe wakweli yaani biskuti za sh mia, pipi na WiFi ndio mnaita bus VIP na kuongeza nauli?
Kuongezeka kwa elfu 15 sio kubwa sana lakini kwa nini muongope kwa kutaja huduma za uongo?
Abiria sio wajinga.