Bus kuwa VIP linatakiwa kuwaje maana kuna moja nimepanda hakuna tofauti kubwa na la kawaida

Nilipanda VVIP ya Ally's star bus, kutoka DAR to Mwanza nauli ni 170k
Aisee Ile bus Iko poa na unahudumia mambo mengi
Seat covers ziko poa
Choo safi
WiFi ina kasi
Azam tv
Unapewa bites za maana
Asbh tukiwa Shinyanga tulipiga break fast ya maana
Ally's star bus wako njema
 
1. Siti ya kukaa
2. Siti ya kukaa
3. Siti ya kukaa
4. Then blabla nyingine.

Muda mwingi kwenye basi tunaotumia Kwa kukaa. Sasa basi lina siti zaidi ya hamsini nalo kabisa linaitwa VVIP? Mtu unatakiwa Ukae Kwa uhuru unyooshe miguu ulale. Yaan siti iwe free
 
Sipingi mkuu wako vzr sana. Pamoja na hayo siwezi rudia panda VIP tena labda kama nasafiri na family ila kama ni mwenyewe tu siwezi
 
Mimi sijaona la maana kama umeamua kulificha hilo bus maana hujawasaidia wengine watakaohitaji huduma ya VIP alafu wakaingia mkenge. Ile JF ya kufichua ujinga na udharimu imepotea kwa baadhi ya members naona.
 
Halafu TV yenyewe, kuna bus moja nilipanda kutoka Dar kwenda MZA ni mambo ya mapigano tu, yaani kwangu ilikuwa kero. Imagine una watoto, na wahudumu wa bus hawajali kwamba kuna watoto au la, wanachukuliwa watoto kama watu wazima kuweka hayo madudu yao tu safari nzima. Kwa nini mfano wasionyeshe mambo ya utalii, kilimo, uvuvi ziwani na baharini, na pia mbunga za wanyama tulizonazo, etc? Hopeless kabisa!
 
Panda gari la kawaida ili mradi liwe na sehemu ya kuchajia simu! Tembea na portable wi-fi hutajutia safari yako.
Mengineyo ni udanganyifu.
Utapigwa bei bila sababu ya maana!
 
Walikupa na maji ya ya sh 500 yako kwenye kichupa laini. 🤣🤣🤣🤣
Wafanyakazi wa humo kwenye mabasi, huwa wanafikiri kila abiria ni mshamba mmoja kutoka Meatu ndani ndani huko, na wakikupa pipi, wanategemea ua-appreciate.
 
 
Aise VIP unapewa pipi nimecheka, maana nilipanda gari ya kwenda Utete ,nakumbuka nilipewa pipi.
Gari ndani ni km banda la kufugia njiwa ,lkn pipi walipewa wote.
 
Kutoa biskuti na maji ya 300/=
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…