Bush stars na Born Town first eleven.....

Du kumbe kuna wanabodi wa zamani humu.Tukumbushane pia na mambo ya majeshi kwa waliopitia huko kwa mujibu wa sheria,Pamoja na burudani ya gazeti la sani tujikumbushe jinsi tulivyohenyeshwa jeshini pia:wink::wink:.
mimi so wa zamani nakumbuka hizi habari nilikuwa nkizisoma nkiwa darasa la tano.............namkumbuka sana rafiki yangu Chama alikuwa akiniletea shuleni maana mzee wake alikuwa mfuatiliaji sana wa haya mambo ila kwa shariti moja tu........kumpa daftari langu la hesabu aigilizie kazi tulopewa na mwalimu
 
kuna mwingine alikuwa anaitwa UDUVI..............
 
Mwingine aliitwa chonka na kaputo
 
Nakukumbusha kidogo

Mapung'o ilikuwa gazeti la Bongo na hawa Bush stars ilikuwa gazeti la sani

star wa Bush star alikuwa mzee Meko na katuni zilikuwa za Ibra radi washokera miaka hiyo


Mkuu asante sana kwa kunikumbusha hilo jina la Ibra radi washokera,wakati nipo Shule ya msingi nilikuwa napenda sana kuchora na nilikuwa eti nikijiita Ibra radi washokera 😆😂
 
Huu ni utajiri mkubwa tunaupoteza
kulikuwa na jarida lingine lenye bi kisebengo na kapelo...
kulikuwa na hadithi kama za 'mzungu halei mwana'

Haya magazeti ya Sani yalikuwa yakitolewa na kampuni iliyojiita WAMASA (Watoaji maandishi wa Sani) sijui hii kampuni kama ipo
 
kuna mtu anakumbuka first eleven....ya timu hizi...
mimi namkumbuka Madenge tu mzee meko wa bush stars
na mtangazaji sukununu...

Zamani ilikuwa raha sana mkuu,watu waliishi bila kubaguana Dini,Ukabila wala rangi,nakumbuka Sikukuu ya X-mass tulikuwa tukila kwa jirani,nao sikukuu ya Iddi wakija kula kwetu,ilikuwa raha sana!

Siku hizi watu wanabaguana sana kwa tofauti zao! Inasikitisha sana huko tunakoelekea
 
kuna mtu anakumbuka first eleven....ya timu hizi...
mimi namkumbuka Madenge tu mzee meko wa bush stars
na mtangazaji sukununu...
namkumbuka straika machachali wa bush stars goal getter Mapung'o him self, jamaa alikua kakomaa ile mbaya na yule konja wao nimemsahau jina alikua anawapa mazoezi ya kikomando badala ya mpira!
 
Maoni ya wengi naona wanachanganya majina ya wachezaji. Ikumbukwe Sani baba lao halafu yakafuata Bongo na Tabasamu.
 


Kweli CCM imeharibu uchumi sana tazama bei yake halafu leo tunauziwa gazeti shilingi 800/=@


Sasa wewe ulitaka toka mwaka 1987 mpaka leo bei ya Jarida iwe hiyo hiyo?!! Mkuu umenistaabisha sana na Complain yako!!
 

Kwa hiyo bifu la Wanaume wa Mkoani na wa Dar ni la kitambo sana.
 
Kuna mechi moja halftime mabush walipiga ugali wakashushia na togwa. Jamaa walikuwa watata sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…