Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
We Mbowe umetoa tuhuma nzito dhidi ya Jeshi la Polisi nchini, lakini hata nyie chama chenu kinao vijana waliopewa mafunzo ya kijeshi, wakati wa uchaguzi na hata sasa uchaguzi wa serikali za mitaa, vijana wenu mliowapa mafunzo wamesambazwa kwenye kila wilaya kutoa mafunzo ya namna ya kufanya vurugu wakati wa uchaguzi, sisi tunayasikia huku mitaani, kwa mfano juzi mlipeleka watu mikoani kwa ajili ya kufundisha vijana kufanya vurugu na mkifika mnakutana na madiwani na mnaeleza kuwa mmetumwa na chama chenu kwa ajili ya kutoa mafunzo ili wayatumie wakati wa uchaguzi, wale vijana wenu walikaa wiki nzima wakisubiri walipwe posho lakini madiwani walishindwana na vijana hao wakarudi, nyie ni watu wabaya sana.
Mwaka 2020 uchaguzi mkuu mlipeleka watu mkoa wa Lindi hasa Nachingwea na Liwale mkachoma gari moto mmoja wafuasi wenu aitwae Hawa alikamatwa na kukaa sana jela, mlichoma ofisi za serikali, kule Masasi, Tunduru, Mtama, Mara huko kwenu Arusha na Moshi kote, mna vijana wenu wa kutoa mafunzo kwa ajili ya kukabiliana na vyombo vya usalama.
Naishauri serikali iende Nachingwea, Masasi, Mtama ifuatilie yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa 2020 vurugu kubwa zilitokea maeneo hayo kwa sababu ya mafunzo waliyopewa vijana, wanawafundisha namna ya kuchoma magari moto, namna kuchoma moto nyumba, kwa hiyo Mbowe hata nyie mnafanya hujuma hizo.
Vurugu zinazotokea wakati wa uchaguzi mnakuwa nyie ndio mmesababisha, mnapeleka vijana wenu kwenda kutoa mafunzo huko mawilayani halafu leo unatokea mbele ya vyombo vya habari kujifanya una data, mbona husema chama chenu pia kinatoa mafunzo kufundisha vijana kufanya vurugu.Sasa kama unanisoma humu ama hunisomi, mimi ni mfanyabiashara nazunguka sana nchini na bahati nzuri nina mtandao mkubwa wa kupata habari, idara yenu mnayoitumia kwenda kufundisha vijana namna ya kufanya hujuma kwa serikali sasa hivi mmefika mwisho, bahati nzuri kila vijana wenu wanapotoka kwenda mikoani na wilayani ninajua, nitakuwa navijulisha vyombo vya usalama kuwa wilaya hii kuna watu wa chama kile wameleta watu wa kutoa mafunzo nendeni mkawadake, sasa usije kulia kulia.