Usiseme kuwa mataifa jirani ndiyo yenye tatizo la Covid 19. Ukweli ni kuwa tatizo hili lipo nchini mwetu. Na kadiri siku zinavyoenda inaonekana linazidi kuongezeka.
Tunajua ni tatizo la Dunia. Tunajua si Rais, Serikali au mtu yeyote amelisababisha hili. Bali tunachomlaumu sana Rais ni kukataa kuwa hili tatizo lipo. Wapo watanzania wengi wanaoamini kuwa Rais akitamka jambo au Serikali, basi ndio ukweli wenyewe. Hawa hawawezi kuchukua hatua yoyote. Na wakifa kwa sababu hawakuchukua tahadhari kwa vile waliamini maneno ya Rais kuwa hakuna tatizo la corona nchini, Rais ana hatia na anakuwa amebeba dhambi kubwa kutokana na kupotea kwa maisha ya watu hao.
Kama sisi sote, tukakubali kuwa kuna hili tatizo, na Rais akatuongoza katika mapambano kwa kutoa elimu ya kutosha kwa umma, hata kama wapo watakaopoteza maisha, hakuna wa kubeba lawama.
Naungana na msimamo wa Rais wa kutowafungia watu ndani ya majumba yao. Lakini siungani naye katika kutowapima watu, kutoshirikiana na Dunia kwenye jitihada za kupambana na Covid 19, na katika kilutokiri kuwa tuna hili tatizo.
Ninavyoandika hivi, rariki yangu wa karibu yupo kwenye msiba wa ndugu wawili waliofariki kwa kupishana kwa siku moja, wote walipatwa na tatizo la kupumua, na wote kama siku 10 hivi walikuwa kwenye Sherehe.
Tumesikia huko Zimbabwe, mawaziri wawili waneondoka, na hivyo kufanya idadi ya mawaziri waliofariki kufikia 4. Na wengine wapo taabani hospitalini.
Tulikubali tatizo, tupime watu wetu ili kujua kiwango cha ukubwa wa tatizo, tutoe elimu ya kutosha kwa watu wote, na tuweke miongozo ya namna ya kufanya kazi zetu ili kupunguza maambukizi, tuimarishe hospitali zetu za wilaya, mikoa na rufaa ili kuweza kuwasaidia watakaokuwa wamekumbwa na ugonjwa huu hatari. Ni aheri baadhi ya miradi isimame ili fedha itumike kununulia vifaa vya kusaidia kuokoa maisha ya Watanzania.
Mungu amjalie hekima Mh. Rais ya kutambua kuwa hakuna kilicho mbadala wa maisha. Hatuwezi kuupata umaarufu wa kisiasa kwa kuyakana matatizo ambayo ni dhahiri.
Sent using
Jamii Forums mobile app