Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
CORONA inakusogelea kwenye lango lako kuu la makalioKwani wewe unasubiri serikali ikuambie jinsi ya kujikinga na corona? Mbona wanasaccos mnakuwa na akili za kuvukia barabara tu? Pia mwambie Mbowe akijifungie tena kule Dodoma na yule dada kama alivyofanya wakati ule mpaka Faru John akamdondosha chini kwenye ngazi!!
Wewe ni janga la dunia.
Janga la dunia!
Usuchanganye mambo jombaa, kuna tofauti kubwa kati ya taifa na serikali...Kuchakutwa mnaliombea taifa juuu ya mabayaa. Kumbukeni suala lakorona mpaka sasa hakuna mbinu sahihi ambayo kunataifa ulimwenguni kote wamefanikisha juu ya mapambano dhidi ya korona, kama si huruma ya Mungu kutunusuru.
Mbona hajaweka namba za simu?????Ameweka na jina lake akumbukwe kwenye teuzi. Bado wakuu wa wilaya.
😂😂Bora life ili ajira zitamalaki Kama kipindi Cha jk. Sasa hivi vijana tuanateseka. Hata zile ajira ambazo zilikuwa hzisumbui hazipo Tena. Ualimu na udaktari
ungebandika hapa hiyo tuita ingependezaSalaam Wana JF,
Kupitia ukurasa wa twitter Bwana Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo" CHADEMA" ametumia haki yake ya Kikatiba kushambulia serikali hasa kiongozi wa nchi juu ya hatua zinazochukuliwa dhidi ya Covid19, Ukweli ni kwamba Bwana Mbowe ameshindwa kuonyesha nia ya kushauri na badala yake "ametuhumu na kushambuli rais wa nchi na taasisi zake" huu ni udhaifu kwa Bwana Mbowe, Binafsi namheshimu sana Bwana Mbowe kwa sababu natambua mchango wake wa siasa za upinzani katika kuchochea maendeleo ya nchi na watu wake, Kwa nafasi yake anayo fursa ya kuongea na Rais wa nchi endapo anaona kuna jambo aliendi sawa kwa maslahi ya umma badala ya kutumia mitandao ya kijamii kuwasilisha mambo mazito yanayohusu maisha ya watu.
Aidha Bwana Mbowe, unaposema "Watu wasio na hatia wanakufa, na huu ni uharamia" una maana gani? Kwamba Serikali imeshindwa kuwajali watu wake dhidi ya janga hili la Covid 19, au ni uzembe wa nani huu? Kwa nafasi yako kama kiongozi wa kisiasa ulipaswa kutoa ushauri kwa viongozi waandamizi wa serikali juu ya hatua gani zichukuliwe dhidi ya tatizo hili la Corona ambalo kwa sasa ni Janga la dunia endapo tu umebaini uwepo wa tatizo hili nchini, hata hivyo Tanzania ni taifa linaloingiliana na mataifa mengine inawezekana kwa njia moja au nyingine kuna tatizo, Kwahiyo kutumia lugha za kejeli na vijembe kwa serikali na Rais kamwe si suluhisho la kupambana na Covid19, toeni ushauri utakao saidia kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu na si lawama hasi zenye mchango hasi kwa Watanzania.
Ukweli ni kwamba jambo hili linakuzwa na kuwa agenda pana mitandaoni pasipo na umuhimu mkubwa wa kufanya hivyo, kwa ufupi kuna" upotoshaji uliopitiliza" Rai yangu kwa Bwana Freeman Mbowe ni kujiepusha na mtego wa kuingia kwenye makundi ya wale watu wanaoshinda mtandaoni kuibua na kuzusha mambo mabaya yenye nia ovu dhidi ya serikali na watu wake kwa sababu wewe ni kiongozi mwenye dhamana kubwa katika taifa hili, Bwana Mbowe tunza heshima yako na angalia usije ukaangukia kwenye makundi haya "maovu"
Hata hivyo Kinga ni bora kuliko tiba, Kwa sababu Tanzania sio Kisiwa na tunaambiwa nchi majirani zetu bado Covid 19 inawasumbua sana, ni rai kwa Watanzania wenzangu kuchukua hatua za kutumia miti shamba kama sehemu ya maandalizi ya kinga, hoja ya kusubiri kiongozi mkuu wa nchi atoe kauli ya kutumia dawa dhidi ya corona ndo tuanze kutumia huo ni utumwa wa kifikra ndani ya maisha yetu.
Niwatakieni Jumapili njema.
Deogratias Mutungi
Sawa,tumekusikia Nabii Tito.Salaam Wana JF,