Bwana Jela Gereza asema hatawaruhusu viongozi wa CHADEMA kumuona Lissu sababu kesi iko mahakamani. Jaji amshangaa

Bwana Jela Gereza asema hatawaruhusu viongozi wa CHADEMA kumuona Lissu sababu kesi iko mahakamani. Jaji amshangaa

KITUKO KILICHOTOKEA MAHAKAMANI.
​
Wakati Mkuu wa Gereza yaani BWANA JELA ambae ni Andrew Shabani Ntamamilo alipohojiwa na Mhe. Tundu Lissu kuhusu Kuwazuia kabisa Mawakili kama Vile Deogratias Mahinyila, Dickson Matata lakini pia viongozi wakuu wa Chama akiwemo John Heche, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu wa Chama, John Mnyika na Amani Golugwa ambao ni mashahidi katika kesi ya Uhaini wamekataliwa kuingia Gerezani Ukonga.

Majibu ya Mkuu wa Gereza amesema yeye hajawazuia. Mhe. Lissu akasema basi watakuja kuanzia kesho. Akasema SITAWARUHUSU waingie kwasababu kesi bado iko mahakamani.

Jaji Amir Mruma ndio akaanza kumuhoji kuna amri yoyote ya Mahakama kuwa watu hawa hawapaswi kuja kumtembelea Tundu Lissu? Akasema kwa kiburi tena kuwa SITAWARUHUSU.

Jaji akavua miwani na kumuuliza unataka tufike huko. Uko serious kweli? Akiwa amekasirika sana. Maaskari Magereza walioko nyuma niliokaa nao karibu wamekimbilia nje kucheka.

Baada ya Jaji kukasirika Bwana Jela akaanza kuomba radhi kwa Jaji. Majaji wote watatu wametikisa vichwa vyao na kuonesha wanashangaa mambo haya yanawezekanaje kwenye Taifa lenye sheria na taratibu.

Kesi hii imeendelea tena kutuonesha watawala wa nchi hii wakoje. Ukisikia majibu ya Mkuu wa Gereza unajiuliza kiburi anakitoa wapi?

Ngoja tusubiri maamuzi ya Majaji mwisho wa kesi hii utakuwaje lakini naamini kila mtu anashuhudia uhalisia wa mambo ulivyo katika Taifa letu.

Tuendelee kusubiri lisaa likamilike turudi kuendelea.

Wanachama leo ni wengi mno. Mahakama imetapika. Yupo Makamu Mwenyekiti John Heche, Yupo Katibu Mkuu, Mnyika. Mama Suzan Lyimo, Mwenyekiti BAZECHA, Yupo Boniface Jacob Mwenyekiti Kanda ya Pwani, Dua Lyamzito, Katibu Mkuu BAVICHA, Pamela Massey, Katibu Mkuu Bawacha. Mzee Azaveli Lwaitama, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chama na wanachama wengine mbalimbali.

Tutaendelea kuwaleteeni live moja kwa moja mwenendo wa kesi hii kutokea Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es salaam...

Source: Hilda Newton X X-Twitter page

=======================
FUATILIA SEHEMU YA DODOSO YA TUNDU LISSU NA MAJIBU YA JEURI YA BWANA JELA. KIDOGO AGEUZIWE KIBAO NA JAJI, BAHATI NJEMA AKAGUNDUA KOSA LAKE, NA KUOMBA RADHI​

Mhe. Lissu: Je ni kweli kwamba baada ya matukio ya Oktoba 29 uliniita ofisini kwako?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli

Mhe. Lissu : Ulivyoniita ukaniambia kuanzia sasa ni marufuku viongozi wa Chadema na wanachama wa Chadema kuja kukutembelea.

Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli

Mhe. Lissu: Na pia ulisema ni ndugu zako wa karibu tu ndio watakutembelea?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli

Mhe.Lissu: Na ukasema mazungumzo yako na mawakili yatakuwa kwa mambo ya kisheria tu?

Ntamamiro (Bwana Jela): sio kweli.

Mhe. Lissu: Wakili Gaston Garubindi alikuwa anakuja kunitembelea Gerezani kabla ya Tar. 14/11/2025

Ntamamiro (Bwana Jela) : kweli

Mhe. Lissu: kuanzia hiyo tarehe hajawahi kuruhusiwa?

Ntamamiro (Bwana Jela): Simpangii.

Mhe. Lissu: Kuanzia niingie Gerezani Wakili Dickson Matata na Deogratias Mahinyila hujawahi kuwaruhusu waingie gerezani. Huyu Matata ni Mwenyekiti Kanda ya Magharibi na Mahinyila ni Mwneyekiti wa Vijana Taifa hawajawahi kuruhusiwa?

Ntamamiro (Bwana Jela): Siwalazimishi waje au wasije.

Mhe. Lissu: Kumbe ndio hivyo. Haya Mahinyila na Matata kesho njooni Ukonga.

Ntamamiro (Bwana Jela): Kesi iko Mahakamani sitawaruhusu

Mhe. Lissu: John Heche, Amani Gorugwa, Katibu Mkuu Mnyika wakiwa kama mashahidi wangu kwenye kesi ya uhaini wamezuiwa kuingia?

Ntamamiro (Bwana Jela): Hawawezi kuingia.

Jaji: Hilo la kwamba huwezi kuruhusu umelitoa wapi? Kuna amri yoyote ya Mahakama?

Ntamamiro (Bwana Jela): Siwezi kuwaruhusu.

Jaji Mruma: Tumefikia huko. Unaiambia Mahakama kuwa huwezi kuruhusu na hauna amri yoyote ya Mahakama? Uko serious kweli au hujaelewa ili tufanye maamuzi na sisi sasa?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Waheshimiwa
majaji naomba radhi.

Jaji anamkata jicho😂🤣🤣🤣
Aisee
 
Kuna siku nilikuwa naongea na baadhi makada wa chama ambao wako karibu na buyu la asali!

Walisema wazi "kitendo cha serikali kuendelea kumshikilia Lissu gerezani hakikisaidii chama. Isipokuwa kinazidi tu kumuongezea umaarufu, huku wananchi wakimchukulia juwa ni shujaa, mzalendo na mpambanaji wa kweli kwa nchi yake." Mwisho wa kunukuu.
 
Kama kesi ni kuhusiana na utaratibu wa kumuona Lisu Magereza halafu bado na yeye anaendelea kuruhusu watu katika utaratibu aliouzoea huoni kama hapo anajiweka kwenye wakati mgumu?

Busara ni kusimamisha mambo yote mpaka mahakama iamue kuhusiana na jambo hilo.

Majaji walipandwa na hasira bure tu.
Ulisoma sheria wapi?hapo suo swala la mazoea ,sheria inasemaje?
 
Kama kesi ni kuhusiana na utaratibu wa kumuona Lisu Magereza halafu bado na yeye anaendelea kuruhusu watu katika utaratibu aliouzoea huoni kama hapo anajiweka kwenye wakati mgumu?

Busara ni kusimamisha mambo yote mpaka mahakama iamue kuhusiana na jambo hilo.

Majaji walipandwa na hasira bure tu.

Yawezekana ulichokikosa siyo maarifa pekee, umekosa hata ile akili ya kawaida.

Wewe ni mjinga wa kiwango cha pekee!!

Kuwepo kwa kesi yoyote mahakamani, hakuzuii jambo lolote la kisheria kuendelea kufanyika kwa mujibu wa shetia. Kesi iliyopo mahakamani haishughuliki kubadilisha sheria yoyote ambayo ipo, bali inachunguzwa kama magereza ilikiuka sheria. Lakini huyo mkuu wa magereza alivyo na akili ndogo, amethibitisha pasipo shaka kuwa amekuwa akivunja sheria na katiba ya nchi. Yaani ameyapa nguvu mashtaka ya walalamikaji, yaani amegeuka kuwa shahidi wa kuthibitisha kuwa magereza yamekuwa yakivunja sheria! Yawezekana huyu mkuu wa magereza ana akili na uelewa mdogo kuukaribia wa kwako.
 
Mpumbavu wewe umeandika ugoro tu hapa.
 
Mhe. Lissu: Kuanzia niingie Gerezani Wakili Dickson Matata na Deogratias Mahinyila hujawahi kuwaruhusu waingie gerezani. Huyu Matata ni Mwenyekiti Kanda ya Magharibi na Mahinyila ni Mwneyekiti wa Vijana Taifa hawajawahi kuruhusiwa?

Ntamamiro (Bwana Jela): Siwalazimishi waje au wasije.

Mhe. Lissu: Kumbe ndio hivyo. Haya Mahinyila na Matata kesho njooni Ukonga.
Ntamamiro (Bwana Jela): Kesi iko Mahakamani sitawaruhusu

Mhe. Lissu: John Heche, Amani Gorugwa, Katibu Mkuu Mnyika wakiwa kama mashahidi wangu kwenye kesi ya uhaini wamezuiwa kuingia?

Ntamamiro (Bwana Jela):
Hawawezi kuingia.

Jaji: Hilo la kwamba huwezi kuruhusu umelitoa wapi? Kuna amri yoyote ya Mahakama?

Ntamamiro (Bwana Jela):
Siwezi kuwaruhusu.

Jaji Mruma: Tumefikia huko. Unaiambia Mahakama kuwa huwezi kuruhusu na hauna amri yoyote ya Mahakama? Uko serious kweli au hujaelewa ili tufanye maamuzi na sisi sasa?

Ntamamiro (Bwana Jela): Waheshimiwa majaji naomba radhi.

Tukiondoa ushabiki wa Kichadema na CCM huyo Bwana Jela alichojibu ni sahihi kabisa.

Hata mimi ningefanya kama alivyofanya. Kuzuia kila kitu mpaka maamuzi yatoke.
Anayetoa maamuzi na sheria ya zuio ni hiyo hiyo mahakama inayomshangaa afisa magereza anayepuyanga na kiburi, badala ya kutaja kifungu cha kuzuia kutotembelewa.
 
Jaji Mkuu 😀😀😀😀😀Wamevuliwa nguo ndani ya banda lao na Afisa magereza na wakashindwa cha kumfanya...what a shame😀😀
Jamaa kanyea mahakama mchana kweupe..hata akikatwa jicho ..amenyeaa tayari
 
Back
Top Bottom