Bwana Misosi akiwa bado underground aliwezaje kuwapata wasanii wakubwa walioonekana katika video yake "Nitoke vipi?"

Umesema vyema
 
Kipusa ilitoka kabla ya nitoke vipi, sema haikuwa heat song
 
😂😂😂😂😂😂
 
Huo wimbo umenikumbusha nikiwa shule O - level nilikuwa nina urafiki na kakikundi fulani cha kihuni nikaponea chupuchupu kupewa suspension.. karibu kundi zima lilipata suspension. Bahati nzuri wote tulienda form five hadi chuo. Kwa sasa tukikutana tunakumbushia tu upuuzi tuliokuwa nao 😄
 
Ngoma imetoka 2002
Mimi nimezaliwa buku mbili , kumbukumbu yangu inaanzia matukio ya 2004 .

Kwa nature ya zamani Ngoma inakaa miaka mingi haisahauliki labda ndio maana nikajikuta bado Iko 🔥 🔥 🔥

Kipindi mdogo sasa Ngoma ambayo ilikuwa habari ya mjini ni ya Juma nature wanaimba "hakuna kulala , cheza kwa mapepe pepe mpaka watu wanakushangaaa ....."
 
Zamani ukumbuke MTU akatoa audio Kwanza ikihit ndio video inafuatia, hakuna atakaekudhamini video wakati nyimbo si nzuri.

So ilikua ni promo pia kwa hao wasanii sababu hii nyimbo ilitrend sana, assume msanii husika alisifiwa, maana alio wadiss kama Sugu hawapo kwenye Video.
 
Watu wengi wa Tanga hawezi kuja dar akawa Hana connection, at that time tayari kuna migration kubwa Sana toka Tanga kuja dar na tayari kuna wasanii wengi wa Tanga wapo peak kina Solo thang, Wagosi wa Kaya, Mr Ebo na wengineo.
 
Watu wengi wa Tanga hawezi kuja dar akawa Hana connection, at that time tayari kuna migration kubwa Sana toka Tanga kuja dar na tayari kuna wasanii wengi wa Tanga wapo peak kina Solo thang, Wagosi wa Kaya, Mr Ebo na wengineo.
Kumbe Mr Ebo wa Kamongo hakuwa Mmasai !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…