Bwana Misosi akiwa bado underground aliwezaje kuwapata wasanii wakubwa walioonekana katika video yake "Nitoke vipi?"

Mkuu tuseme umechuma ubao leo.!

Utazikwa pale muhimbili kwa Kina tambaza bampa 2 bampa, au una mji wako kimanzichana.?
Mimi sitaki kuzikwa mkuu.

Kuzikwa ni uharibifu wa mazingira na kuhodhi ardhi kwa vizazi vijavyo.

Yale makaburi yetu ya Tambaza pale Muhimbili ilibidi mengine yafukuliwe patengenezwe barabara ya Maliki kuunganisha Upanga chini huku kupanda kwenda Muhimbili hospitali.

Ndiyo maana yale makaburi kuna ya upande wa msikitini tulipomzika Masha na upande wa shule ya msingi Muhimbili huku kwa kina Abbas Pambe.

Sasa mimi sitaki kuzikwa leo halafu baada ya vizazi watu wakataka kujenga kitu chao, kaburi langu liwe tatizo kwao.
 
Basi sawa
 
Dah!! Umri wa mwanangu wa kike wewe! Ila mnavyotutukana humu,wakati ni baba zenu behind the key board!
 
"Tunakatana Mitaa Ya Chaga Bite,,Asubuhi Tunapata Zetu Supu Kwa Chapati...."
Dah! Kitambo sana ,ilikuwa kiwanja changu CHAGA BITE kula michemsho,au pale BREAK POINT kula nyama pori.....miaka imeenda na Age Go! kifo kipo karibu yetu kuliko uhai mrefu Tena ......miongo mitatu ijayo sidhani kama tutakuwepo sisi wa Age Go.... inshallah Mungu atupe umri mrefu tuje kushuhudia CCM ikiwa chama pinzani.
 
Mike T na TID walitisha sana kwenye vipande walivyoonekana.
 
Nimegumiana nao sana pale chaga bite makumbusho miaka ya 2002! Kina jafarai

Ndio, Jafarai alikuwa hatulii na virasta vyake kipindi hiyo na wimbo wake Nipo Busy. Kila siku lazima aje kudundika mitaa ya kati, sijui daladala za Mwenge alikuwa anapanda bure
 
Watu wengi wa Tanga hawezi kuja dar akawa Hana connection, at that time tayari kuna migration kubwa Sana toka Tanga kuja dar na tayari kuna wasanii wengi wa Tanga wapo peak kina Solo thang, Wagosi wa Kaya, Mr Ebo na wengineo.
Badala ya kumtaja mh naibu waziri khamis mwinjuma unamtaja Mim mmasai bwana nasema mi mmasai.
 
Nakumbuka mwaka 2006 nilimuacha demu wangu kisa aliniletea kiburi. Nikawa namsindikiza kwa ule wimbo wa Dully Sykes, eti, "Hunifahamu,sikufahamu dada iweje Leo unipakazie..."

Dr am 4 real PhD ulikuwa wapi kipindi kile?
 
Badala ya kumtaja mh naibu waziri khamis mwinjuma unamtaja Mim mmasai bwana nasema mi mmasai.
Mwana FA na Bwana misosi ni age moja kimuziki, wote watoto wa 2000 mwanzoni, hao niliowataja kina Solo na Mr Ebo tayari walikua ma super star wakati Misosi anatoka, ndio maana aliwataja kwenye nyimbo yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…