Misosi ametoa Nitoke Vipi alikuwa tayari ana jina ,wimbo wake uliomtoa ni KIPUSA na hata moja ya verse kwenye huo wimbo amesema hivi "Soggy pacha wamchanganya ,jay mo mvua na jua ,misosi nitoke vipi na KIPUSA nimewagongea? Dully mr misifa mwanasesele ikamtoa ,nini mnataka mazee Piggy Black akatoboa".
Hapo anaposema KIPUSA nimewagongea ni wimbo wake unaitwa KIPUSA na ndipo Late Misanya Bingi akaanzisha kipindi radio One kinaitwa KIPUSA unaulizwa swali ukikosa unapigiwa Kengele ,hiyo idea aliitoa kwenye wimbo wa Bwana Misosi.