Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,281
Bwana Ndugai anahitaji msaada wa haraka wa saikolojia.
Malisa GJ
Mosi, Huu uchungu anaouonesha Ndugai sio wa Halima na wenzake kupigwa, ni uchungu wa kupoteza yale matrilioni ya wafadhili. Ameshaona dalili zote kwamba hata akiwalinda akina Mzee Halima na wenzake waendelee kuwa wabunge, wafadhili wanaweza kugomea kutoa yale matrilioni.
Pili, Halima na wenzake hawakupigwa kwa ajili ya Mbowe. Walipigwa kwa sababu ya kutetea haki zao. Walipotolewa Segerea askari magereza waliwapiga kama vibaka kwa sababu tu walienda kupokelewa na wafuasi wao. Mashinji alipokelewa na msafara wa wafuasi wa CCM lakini hakupigwa. Double standards. Kama kweli Ndugai ana uchungu angewakemea wale askari waliofanya unyama ule sio Mbowe.
Tatu, Mzee Halima na wenzake hawajafukuzwa bila kusikilizwa. Walipewa haki ya kusikilizwa (audi alteram partem) lakini wakakataa kuitumia. Waliitwa kwa maandishi kwenye kamati kuu ili wasikilizwe wakagoma. Sasa Bwana Ndugai alitaka chama kifanyeje? Hata mahakamani mtuhumiwa akikataa kujitetea bila sababu za msingi, mahakama hulazimika kuamua kwa kusikikiza upande mmoja.
Nne, Maamuzi ya Chadema hayakufanywa na Mbowe. Yalifanywa na Kamati kuu ambayo ina wajumbe zaidi ya 40. Ni ujinga kuamini wajumbe wote hawakua na sauti isipokua Mbowe peke yake. Ndugai elewa kwamba Mbowe sio kamati kuu ya Chadema.
Tano, kumbe Ndugai anajua Halima na mwenzake walipigwa hadi wakazimia pamoja na kuvunjwa mikono na askari magereza? Unyama huu aliwahi kuulaani popote? Aliwahi kumuita Kamishna Mkuu wa Magereza kwenye kamati za bunge ajieleze kwanini Askari wake walifanya unyama ule tena kwa wabunge wanawake? Au aliona ni sawa tu kwa sababu walikua Chadema. Leo wamefurushwa ndio anasikia uchungu.
Huu utaratibu wa mtu kuonewa lakini unakaa kimya kwa sababu sio wa chama chako sio ubinadamu kabisa. Ningemuona Ndugai ana hoja kama angekemea tukio lilipotokea. Sasa Halima ameshapona na kusahau ndio Ndugai anasikia uchungu leo? Haina tofauti na mkeo kulia kwa uchungu na kukuomba msamaha kwa sababu ya vita vya majimaji eti babu yake alishirikiana na wakoloni kuwapiga wazawa. Wendawazimu!