Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maji inaendelea kutekeleza Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kidunda mkoani Morogoro, mradi unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 335.
Mradi huu ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati inayolenga kuongeza uhakika wa upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, ambao hutumia Mto Ruvu kama chanzo kikuu cha maji kwa mikoa hiyo.
Ujenzi wa Bwawa la Kidunda umefikia asilimia 60.1 ya utekelezaji na inatarajiwa kufikia hatua ya kuanza kuhifadhi maji ifikapo Disemba 2026.
Mradi huu umebuniwa kama hatua muhimu ya Serikali kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo vipindi vya ukame vinavyoweza kupunguza kiwango cha maji katika chanzo cha mto Ruvu. Uhifadhi wa maji katika Bwawa la Kidunda utasaidia upatikanaji wa maji katika Mto Ruvu katika majira yote ya Mwaka hivyo kuchangia upatikanaji endelevu wa huduma ya majisafi kwa wananchi.
Msimamizi wa mradi huo Mhandisi Christian Gava ameeleza kuwa mbali na kuhakikisha upatikanaji wa maji, kukamilika kwa mradi huo kutaleta manufaa mbalimbali kwa jamii zinazozunguka bwawa na Taifa kwa ujumla. Miongoni mwa manufaa hayo ni kuboresha huduma ya maji kwa vijiji vinavyolizunguka bwawa, kuwezesha uzalishaji wa umeme wa megawati 20 utakaoingizwa katika gridi ya Taifa, pamoja na kuchochea shughuli za kilimo cha umwagiliaji, uvuvi na utalii. Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza fursa za kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi katika maeneo yanayozunguka mradi.
"Mradi wa Bwawa la Kidunda pia unatarajiwa kuwa chanzo muhimu cha ajira na shughuli za kiuchumi katika kipindi chote cha utekelezaji. Zaidi ya ajira 1,000 zimezalishwa, huku wananchi wakinufaika pia na fursa mbalimbali zitakazochochewa na uwepo wa miundombinu ya bwawa, uboresha miundombinu ya barabara kwa kiwango cha changarawe kwa urefu wa takribani kilomita 75 kutoka Ngerengere hadi Kijiji cha Kidunda, hatua inayolenga kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa pamoja na kurahisisha shughuli za utekelezaji na uendeshaji wa mradi" ameeleza Mhandisi Christopher.
"Kazi kubwa zinazoendelea kwasasa ni pamoja na ujenzi wa tuta, ujenzi wa mitambo ya kuzalisha, kupooza na kusafirisha umeme, ujenzi wa Barabara kilomita 75 kwa kiwango cha changarawe pamoja na Ujenzi wa makazi ya kuduma kwa watumishi watakaohusika na uendeshaji wa mtambo" ameongeza Mhandisi Christopher.
Bwawa la Kidunda ni mradi wa kimkakati wenye umuhimu mkubwa katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa na uhakika wa rasilimali za maji katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Kukamilika kwake kutaimarisha upatikanaji wa maji kwa mamilioni ya wananchi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, huku ukifungua fursa mpya katika uzalishaji wa umeme, kilimo, uvuvi, utalii, ajira na maendeleo ya miundombinu katika Mkoa wa Morogoro na maeneo mengine yanayonufaika na mradi huo.