Bwawa la kufua umeme la Nyerere ni dogo mno kulinganisha na uwezo wa maji katika bonde la mto Kilombero na Rufiji. Tulipaswa kutengeneza walau 6000MW!

CCM huwa HAIPENDI kabisa kutumia takwimu.

Ndiyo maana walitunga Sheria kali kuzika Umma kutumia takwimu.
 
mabwawa yotee yamejaa!sasa tusisikie kuna mgao!maaan hii serikali haishindwi!!
 
Kwanza lazima ujue flow rate ya maji ya mto. Avarage flow rate. Usiangalie maji yanayotiririka kwa wingi kipindi cha Masika tena mwaka wa Elnino. Pili unatakiwa uone unaweza kujenga bwawa lenye kimo cha kiasi gani. Maeneo ya milima unaweza jenga bwawa lenye kimo kirefu, hivyo hata kama mto ni mdogo bado unaweza zalisha umeme mwingi.
 
Haiwezekani siku zijazo kukafanyika mradi mwingine huko, kama Inga Dam ya DRC kuna Dam 1, 2 na sasa 3 , ina uwezo wa kuzalisha MW 100,000 kutosheleza Africa nzima lakini Kwa sasa hii ya 3 itakuwa ina zalisha MW 30,000 Tu
 
KWA MARA NYINGINE TENA TUMEZALISHA GUNIA MOJA LA MAHINDI KWENYE HEKA MOJA NA TUNAWASIFU VIONGOZI WETU SANA KWA HILO!
Ipi bora mkuu.kuzalisha gunia moja kwa heka angalau ukala ugali au kuendelea kuhemea
huku heka yako moja ikizidi kuota mbigiri?
Mi nadhani Tanesco wakijiongeza,wanaweza kuongeza uwezo wa mashine kwa kufunga mashine za kisasa zaidi
hapo mbeleni.Kwa sasa tupongeze hatua iliyofikiwa.
 
Inauma sana mambo mengi nchi yanaamuliwa na wanasiasa wasiojua ukweli wa mambo na wageni kutoka nje wanapenda mno hali hii manake wanapiga hela hadi wanafurahi. Unaona Mwendokasi Dar, tuna miundombinu lakini usafiri Dar bado ni wa shida kubwa inabidi uwe na uwezo mkubwa wa kusukumana na watu ili uweze kusafiri, tatizo ni uwezo mdogo kifikra wa viongozi wetu. Na SGR nayo itakuwa hivyo hivyo kama hatutabinafsisha mapema.
 
Suala si kubinafsisha, suala ni ipo ya kufanya kitu, mfano hao wenye kufikiria kubinafsisha wanasema hivyo kwa madhumuni yapi. Nia binafsi au Kwa ajili ya umma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…