Bwawa la Mwalimu Nyerere lafikia MITA 185 ujazo, lajaa mpaka kikomo

Bwawa la Mwalimu Nyerere lafikia MITA 185 ujazo, lajaa mpaka kikomo

Hili bwawa sio Michezo lipo Kama ziwa ( lake ) !
Panaweza kuwa sehemu ya kivutio cha utalii ingawa kutakuwa na mi mamba ya kutosha!
 
Kwanini wafungulie kwani hakuna "overflow" kwenye design yake?
Kwenye Kingo za bwawa kutakuwa na sensor za kupima stress inayosababishwa na nguvu ya maji , sasa kuna vipimo vyake vya kuelekeza maji yafunguliwe au la kupunguza stress katika kingo za bwawa.
Na kufunguliwa sio yanafunguliwa yote Hapana , yanapunguzwa kidogo kidogo lakini bwawa linakuwa limejaa kuna li mlango la chuma Kama li geti linapanda juu maji yanapita ndiyo hio overflow au spillway.
 
Magufuli alisema pale chini ya bwawa kutakuwa na kilimo cha umwagiliaji, mpunga utakao limwa pale utaweza lisha dar yote, sasa sijui kama hilo lita fanyika maana mwenye wazo lake hayupo tena.

Aliwaambia watu wajipange kwa kufanya kazi. Ila sasa watu wenyewe ndio kina sisi. Tumepambana bwawa lisitokee imeshindikana. Sasa tunamwaga maji ili tusemeje?
 
Chadema walisema bwawa halitajaa kisa imekatwa miti milioni 3
.

Magufuli anawaaibisha wajinga nyie
Siyo CHADEMA. Kama una uchawa ndani basi unakufa ukiwa mnafiki na katika uzee wako utakuwa mchawi. NAPE ndiye aliyekuwa akisema Bwawa halitajaa maana Serikali inakata mamilioni ya miti. Nape tangu lini amekuwa CCM?
 
Bwawa la mwalimu Nyerere limejaa kabisa mpaka kufikia ujazo wa MITA 185 kati ya mita 186 kutoka usawa wa Bahari.

Hivyo Serikali kuanzia Muda wowote itaanza kumwaga maji au kufungulia maji Kwa lugha ya Magufuli, hili zoezi linafanyika kwakuwa mitambo ya uzalishaji umeme haijakamilika yote kama ilivyokusudiwa, maji yaliyopo ni mengi na mashine inayotembea ni moja tu, hivyo Serikali itafungulia maji bure Ili yaende baharini samaki wakanywe.

Mradi ukikamilika unatarajia kuzungusha mashine 9.

Makusudi.
Uharibifu huwa na hatua kuutekeleza
 
Wayapunguze haraka, mfumo usije elemewa yakazuka mengine!, "Jambo likazua jambo"
 
Kwahio sio kwamba maji ndio kikwazo (ukame) bali ni uzembe (AKA Ukame wa Juhudi)
Hawa watu tunatakiwa kuwawajibisha!! Tuwaunge Chadema mkono tundamane nchi nzima kupinga huu ujinga. Wanatuona watoto sana hawa ccm. Tundamane hadi kieleweke watupatie umeme wa uhakika,gharama za maisha zishuke chini.
 
Hili bwawa sio Michezo lipo Kama ziwa ( lake ) !
Panaweza kuwa sehemu ya kivutio cha utalii ingawa kutakuwa na mi mamba ya kutosha!
Magufuli alisema lita toa ajira kwa wavuvi, pia kilimo cha umwagiliaji kwa kule chini after maji kutoka,...ni maoni yangu wapeleke vifaranga vya sato na sangara pale ili wawe wana vuliwa pale na kuletwa dar kwa bei rahisi.
 
Kama wameshindwa kulitumia Kama ilivyotarajiwa turuhusiwe tukaogeleee
 
Siyo CHADEMA. Kama una uchawa ndani basi unakufa ukiwa mnafiki na katika uzee wako utakuwa mchawi. NAPE ndiye aliyekuwa akisema Bwawa halitajaa maana Serikali inakata mamilioni ya miti. Nape tangu lini amekuwa CCM?
Haaa! Nape sio CCM?
 
Back
Top Bottom