Huwa natafakari sana hili jambo!!Honestly simkubali Magufuli hata kidogo kwa mambo mengi aliyoyafanya ila nilikubaliana naye vitu viwili tu!!
Kwenye Covid na mradi wa Bwawa la Nyerere!!
Najiuliza alitoa wapi uthubutu wa kuamua kujenga bwawa la Nyerere?Hakuogopa mabeberu na makampuni ya solar ya dunia?
Hivi mnajua miradi kama hii inavyopigwa vita na wakubwa?Kuna nguvu kubwa sana ya kupinga hii miradi hususan kwa hao mabwana wakubwa wa dunia na vibaraka wao!!
Ethiopia wenyewe lile bwawa lao la Megawatts 7000 wamelijenga kwa kukomaa sana,maana lilipigwa vita sana na nchi za Misri na Sudan walitumiwa sana na kuna kipindi ilifika hadi Misri ikataka kwenda kulilipua lile Bwawa.Lakini wamepambana wamelijenga leo hii Ethiopia ndo nchi miongoni wenye umeme nafuu zaidi kule units bei yake ni chee mnoo yaani umeme wa jero ni units za kutosha
Halafu kuna wajinga wanathubutu kubeza mradi mtakatifu kama huu wa bwawa la Nyerere Magufuli sikumpenda ila kwa hili nilimuunga mkono kwa 100% na kwa hili tumpe maua yake tu.Kuna mambo yanahitaji utaifa na uzalendo huu mradi ukienda kama ilivyopangwa lazima utakua suluhisho la shida za umeme Tanzania
Huu mradi ulipigwa Vita tokea kipindi cha Nyerere hakuna aliyethubutu kujenga wala kufungua file lake na kuchungulia kwasababu huko ni kutafuta ugomvi na wakuu wa dunia na wauza solar na majenereta Lakini jpm did...Kuamua kufanya maamuzi kama haya sio kazi rahisi ni kama kujiingiza katikati ya chui wakali tu
Tz bado tuna changamoto ya wahuni ni wengi, bado amini nawaambieni mimi Kimsboy kuna jambo nataka niliseme hapa na mlimark kabisa[emoji1313][emoji1313]
Ninapata hisia kuwa huenda huu mradi ukija kukamilika utahujumiwa tu!!Aidha ukikamilika uhujumiwe hadi uzalishe megawatts chache tu ili ipatikane sababu kuwa huu mradi ulitakiwa utoe megawatts 2200 lakini unazalisha megawatts kidogo sana tofauti na matarajio hivyo inabidi tutafute miradi mbadala (solar,mafuta na upepo)
Huenda huu mradi utakamilika lakini wahuni wakaanza kutengeneza matatizo ya mgao kwa kuzuia maji yasiende bwawani au kuyafungulia mimi simuamini Makamba kabisa kwa hili nalitamka wazi
Huu mradi hata hivyo haupo salama chini ya Makamba!!
Makamba na Maharage sidhani kama ni watu sahihi wa kusimamia huu mradi yaani hata koti la uzalendo au la huu mradi ukiwavalisha haliwaivi kabisa yaani hawafananii kabisa kusimamia huu mradi na sijui kwanini siwezi kuwaamini hawa watu mimi Makamba na huu mradi naona ni kama maji na mafuta tu yaani haviendani kabisa sijui ilikuaje Mama akampa makamba hii wizara sijui na sidhani kama ni yeye alifanya haya maamuzi au ndo mambo ya "rimoti"?
Huu mradi inabidi ukikamilika upate mtu mkali kidogo na asiecheka na wahuni watengeneza migao, hapo kuna watu washauandalia mahesabu kuwa watauhujumu vipi hii natoa kama indhari tu