Bwawa la umeme la JNHP lingekamilika mapema hizi athari za vita vya Ukraine visingetuathiri kwa kiasi kikubwa. Uzembe wa January Makamba unatugharimu

Bwawa la umeme la JNHP lingekamilika mapema hizi athari za vita vya Ukraine visingetuathiri kwa kiasi kikubwa. Uzembe wa January Makamba unatugharimu

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
January Makamba kama waziri mwenye dhamana ya nishati hapa nchini alipaswa kukomaa kwa hali na mali kuhakikisha JNHP inakamilika kwa wakati na ikiwezekana hata kabla ya wakati.

Kwa nini bila sababu za msingi alileta mizengwe juu ya ujazaji maji na kuchepusha maji?

Leo hii tungekamilisha JNHP kwa wakati tungesababisha bei ya umeme kushuka na hii ingesaidia kushusha gharama za uzalishaji kushuka na kusabisha bei za bidhaa kushuka.

Vita vya Ukraine hata kama vingeleta athari ingelikuwa kidogo sana.
 
Watu hamuelewi na ni kwasababu Serikali imejengeka katika mfumo wa kuficha siri. Ukweli ni kwamba aliyefanya Bwawa la Nyerere lichelewe si Samia wala January wala Kalemani. Ni Mwendazake.

Narudia tena ni Mwendazake kwa ubahiri wake wa kuipa kampuni isiyo na uwezo katika kutekeleza baadhi ya kazi.

Hiki kitu msitarajie kwamba kitakuja kisemwa hadharani na hata kama kitasemwa je mtakiamini? Serikali inalipa kwa wakati pesa na haidaiwi sasa si mjiulize kama shida ni Samia au January au nani?

Men, kufagia uchafu wa Malaika wa Chato si Jambo rahisi kama mnavyodhani.
 
Watu hamuelewi na ni kwasababu Serikali imejengeka katika mfumo wa kuficha siri. Ukweli ni kwamba aliyefanya Bwawa la Nyerere lichelewe si Samia wala January wala Kalemani. Ni Mwendazake. Narudia tena ni Mwendazake kwa ubahiri wake wa kukupa kampuni isiyo na uwezo katika kutekeleza baadhi ya kazi. Hiki kitu msitarajie kwamba kitakuja kisemwa hadharani na hata kama kitasemwa je mtakiamini? Serikali inalipa kea wakati pesa na haidaiwi sasa si mjiulize kama shida ni Samia au January au nani? Men, kufagia uchafu wa Malaika wa Chato si Jambo rahisi kama mnavyodhani.
Hoja iliyopo mezani ni athari za vita ya Ukraine kwenye uchumi wetu. Athari zingepungua sana kama umeme ungepungua bei baada ya kukamilika JNHP.
 
According to master plan lilikuwa likamilike lini? Mwendazake aliliache kwenye stage gani interms of pc??
 
Back
Top Bottom