Bwawa la umeme likikamilika sitegemei Dar iwe na barabara za giza hata kwa bahati mbaya

Bwawa la umeme likikamilika sitegemei Dar iwe na barabara za giza hata kwa bahati mbaya

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Kwa sasa Tanganyika inatumia Takriban Megawatt 1,500 za umeme, ukijumlisha na zile Megawatt 100 wanazopewa bure wala urojo inakuwa MW 1,600.

Bwawa la Nyerere likikamilika litazalisha Megawatt 2,100, na kufanya jumla ya Megawatt kwenye Gridi ya Tanganyika kuwa 3,700.

Kwakuwa umeme unaozalishwa kwenye bwawa hauwezi kutunzwa kwenye battery kama za gari, inabidi utumike wote na kuisha, kufanikisha hili itabidi mambo kadhaa yatokee.

1.) Kushusha bei ya umeme ili viwamda na wananchi watumie umeme mwingi zaidi sababu ni wa bei nafuu AU

2.) Umeme ugawiwe bure kwa sekta maalum kama wanavyopewa bure wala urojo.

Sekta hizo ni

1.) Afya - Mahospitali, Zahanati na vituo vyote vya afya wapewe umeme bure kama Zanzibar.

2.) Elimu - Mashule yote ya kutwa na bweni wapewe umeme bure kama Zanzibar

3.)Barabara - Taa zote za barabarani zipewe umeme bure kama Zanzibar

Kinyume cha haya, itabidi tufungulie maji kwenye bwawa yamwagike bure (uchawi mtupu!) bila kuzalisha umeme, kama ilivyokuwa ikifanyika kipindi cha Jakaya Msoga ili kutengeneza uhaba feki na kupiga pesa za Richmond.

Sioni namna nyingine, labda waharibu mitambo kwa makusudi.

Hivyo sitegemei jiji letu la Dar liwe giza usiku, tunataka ling’ae kama Almasi ya Eden!

========================

 
Wewe ni hamnazo,nani atakuwa analioia bill za umeme? Mji upi hapa Tzn umeona wanatumia umeme wa Tanesco Kwa street lightening?
 
Wewe ni hamnazo,nani atakuwa analioia bill za umeme? Mji upi hapa Tzn umeona wanatumia umeme wa Tanesco Kwa street lightening?
Kwani Bwawa kajenga nani? Tuache maji yamwagike bila kuzalisha umeme? Au utawapa Tanesco battery za kuhifadhi umeme?
 
Umeme wa maji unaweza kutunzwa. Badala ya kufungulia maji ya kuendesha turbines zote. Unaendesha zinazohitajika na hivyo kubakiza maji mengi bwawani. Wakati wa ukame unaongeza kufungulia.
 
Huku Ruangwa Lindi taa zote za barabarani zinatumia Solar,sio umeme wa Tanesco..
Kumbe Solar panel zinagawiwa bure siku hizi? Sasa kwanini watu wanaendelea kutumia umeme wa Tanesco majumbani badala ya Solar?
 
Screenshot_20230729_140839_WhatsApp.jpg
 
nampongeza raisi wa jamuhuri ya tanzania kwa kutupigania watanzania .pia nitoe shukurani zangu kwa chama cha mapinduzi na kamati kuu kwa kuzidi kuitumikia ilani ya chama kwa maslai mapana ya taifa
 
Back
Top Bottom