Bwawa la umeme likikamilika sitegemei Dar iwe na barabara za giza hata kwa bahati mbaya

Bwawa la umeme likikamilika sitegemei Dar iwe na barabara za giza hata kwa bahati mbaya

Kwa sasa Tanganyika inatumia Takriban Megawatt 1,500 za umeme, ukijumlisha na zile Megawatt 100 wanazopewa bure wala urojo inakuwa MW 1,600.

Bwawa la Nyerere likikamilika litazalisha Megawatt 2,100, na kufanya jumla ya Megawatt kwenye Gridi ya Tanganyika kuwa 3,700.

Kwakuwa umeme unaozalishwa kwenye bwawa hauwezi kutunzwa kwenye battery kama za gari, inabidi utumike wote na kuisha, kufanikisha hili itabidi mambo kadhaa yatokee.

1.) Kushusha bei ya umeme ili viwamda na wananchi watumie umeme mwingi zaidi sababu ni wa bei nafuu AU

2.) Umeme ugawiwe bure kwa sekta maalum kama wanavyopewa bure wala urojo.

Sekta hizo ni

1.) Afya - Mahospitali, Zahanati na vituo vyote vya afya wapewe umeme bure kama Zanzibar.

2.) Elimu - Mashule yote ya kutwa na bweni wapewe umeme bure kama Zanzibar

3.)Barabara - Taa zote za barabarani zipewe umeme bure kama Zanzibar

Kinyume cha haya, itabidi tufungulie maji kwenye bwawa yamwagike bure (uchawi mtupu!) bila kuzalisha umeme, kama ilivyokuwa ikifanyika kipindi cha Jakaya Msoga ili kutengeneza uhaba feki na kupiga pesa za Richmond.

Sioni namna nyingine, labda waharibu mitambo kwa makusudi.

Hivyo sitegemei jiji letu la Dar liwe giza usiku, tunataka ling’ae kama Almasi ya Eden!
Umeme unazalishwa kwa gharama kubwa sana alafu hauna aibu kutaja neno Bure katikati ya maandishi yako?bloody fool

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
 
Umeme unazalishwa kwa gharama kubwa sana alafu hauna aibu kutaja neno Bure katikati ya maandishi yako?bloody fool

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
Umeme wa maji ni wa gharama ya chini sana by comparison, na kwakuwa maji yana flow yenyewe, ile nguvu yake ndio inazalisha umeme. Sasa sijasema bure as a first option, bali a option ni kushusha bei accordingly ili matumizi yaongezeke kuweza kumaliza 3700MW. Kama hawataki kushusha bei, badi itabidi wagawe bure, maana hakuna netri ya kuhifadhi umeme utakaozalishwa bwawani...
 
Kama hauna matatizo ya akili basi utakua na shida ingine.
Izo trill 7 zilizowekwa apo rufiji zinatakiwa zirudi usilete hadithi zako za ujinga

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
 
Kama hauna matatizo ya akili basi utakua na shida ingine.
Izo trill 7 zilizowekwa apo rufiji zinatakiwa zirudi usilete hadithi zako za ujinga

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
Zitarudi kwa kuyaacha maji yamwagikie chini bila kuzalisha umeme? Au utawapa Tanesco betri za kuhifadhi umeme? Mbona unaongea kama mwendawazimu bila kugusa hoja niilizobainisha mwehu wewe..
 
Wenye nchi washasema bei haitashuka!
Screenshot_2023-07-30-19-36-11-86_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
 
Umeme wa maji unaweza kutunzwa. Badala ya kufungulia maji ya kuendesha turbines zote. Unaendesha zinazohitajika na hivyo kubakiza maji mengi bwawani. Wakati wa ukame unaongeza kufungulia.
Basi wataendelea kuminya hivyo ili watukamue wakalipie madeni ya mikataba mibovu waliotuingiza mkenge.
 
Mr bure wait and see

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
Jibu hoja, utarudisha gharama za kujenga bwawa kwa kuyaacha maji yamwagike chini bila kuzalisha umeme? Au utayatumia maji yote kuzalisha umeme halafu huo umeme utauhifadhi kwenye battries?! Au utashusha Bei ili umeme wote utumike ili viwanda vitor ajira na wananchi wafaidike kwa pesa walizotumia kujenga bwawa lao? Au hilo bwawa kajenga mjomba wako kwa pesa zake?

Nikasema kama watashindwa kushusha bei kwa roho zao mbaya za kichawi, basi itabidi wagawe bure huo umeme, maana huwezi kuuhifahi
 
Hili bwawa tumegharamika wote, likikamilika wote tufaidi, maana watu washajioanga formation kali za 4-4-2 kupiga mapato yote...
 
zo trill 7 zilizowekwa apo rufiji zinatakiwa zirudi usilete hadithi zako za ujinga
Hizo pesa, ni mimi na wewe yaani serikali tumezilipa kufanya huo uwekezaji. Ili gharama ya nishati ishuke tuzalishe viwanda zaidi. Tz ya viwanda kumbuka?

Kama tumekopa tunaweza kuanza kuzilipia, lakini kama zinajengwa kwa fedha za ndani basi ndio sasa hivi mimi na wewe tunazilipa kupitia tozo.

Serikali ipo kuhakikisha mazingira ya wanaserikali kuzalisha yanakuwa njema ndio jukumu la kwanza kabisa na lengo la kuundwa kwa serikali yenyewe. Elewa.

Hivi unaelewa hasa kimsingi serikali ni nini? Serikali ni mimi na wewe (majirani) tukijenga kidaraja ili tuvushe magari yetu kuingia kwetu. Tunaposhirikiana kujenga daraja tayari tunalipia ili baadae tuzifaidi faida zake. Hatuwezi tena baadaye kushauriana eti kila tukivuka kidaraja tulipie ili kulipia gharama za ujenzi!!!! Halafu hizo pesa ziende wapi?
 
Bwawa lilijengwa kisiasa, hatukuwa na uhitaji mkubwa hivyo, tulipaswa ongeza uzalishaji kwenye gesi angalau tufikie 1200MG ambayo ingekuwa rahisi zaidi
 
Back
Top Bottom