Bwawa la umeme likikamilika sitegemei Dar iwe na barabara za giza hata kwa bahati mbaya

Bwawa la umeme likikamilika sitegemei Dar iwe na barabara za giza hata kwa bahati mbaya

Hizo pesa, ni mimi na wewe yaani serikali tumezilipa kufanya huo uwekezaji. Ili gharama ya nishati ishuke tuzalishe viwanda zaidi. Tz ya viwanda kumbuka?

Kama tumekopa tunaweza kuanza kuzilipia, lakini kama zinajengwa kwa fedha za ndani basi ndio sasa hivi mimi na wewe tunazilipa kupitia tozo.

Serikali ipo kuhakikisha mazingira ya wanaserikali kuzalisha yanakuwa njema ndio jukumu la kwanza kabisa na lengo la kuundwa kwa serikali yenyewe. Elewa.

Hivi unaelewa hasa kimsingi serikali ni nini? Serikali ni mimi na wewe (majirani) tukijenga kidaraja ili tuvushe magari yetu kuingia kwetu. Tunaposhirikiana kujenga daraja tayari tunalipia ili baadae tuzifaidi faida zake. Hatuwezi tena baadaye kushauriana eti kila tukivuka kidaraja tulipie ili kulipia gharama za ujenzi!!!! Halafu hizo pesa ziende wapi?
Mnavyojificha kwenye kivuli cha kodi zetu wakati wanaolipa kodi za serikali hawafiki hata 5M mnakua mnakera sana

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom