By 2015 Kigoma kuwa kama Dubai, Mwanza kuwa kama California

Mkuu Mbona China, Singapole, Malaysia zilibadilika ndani ya muda mfupi tu licha ya kufulia kwa muda mrefu.

Usimbeze wala usimfananishe na asiye yeye, Kikubwa ni kumuuliza " How" ya hicho alichokisema
Kwa mipango ipi tuliyonayo, mleta mada kakupa mfano mmoja wa SGR miaka 5 km 200 tu kwenda Moro zimetushinda je km 2000 itatuchukua miaka mingapi.
 
Haiwezekani taifa likaendelea bila kufanya biashara ya kimataifa, kuuza bidhaa na huduma nje pamoja na kuruhusu uwekezaji. Chanzo kikubwa cha utajiri wa Uchina na Marekani ni biashara za kimataifa na siyo maneno matupu. Marekani ameanza kuwa taifa tajiri kipindi cha The Gilded Age 1870 ambapo alifanya sana biashara za kimataifa na mataifa ya Ulaya. Mwaka 1945 yeye akawa ndiyo The Leading Exporter of Merchandise akawa anamiliki nusu nzima ya GDP ya dunia kwasababu ya kuuza silaha za vita na kutoa mikopo huko Ulaya.

Uchina amefika hapo alipo kwasababu Deng-Xiaoping aliachana na The Concept of Centralized Economy and Arrested Development. Halafu Uchina ilikuwa na miondombinu mizuri sana iliyoachwa na serikali ya Chian-Kai Shek lakini Mao-Zedong aliamua kuivuruga kupitia sera yake ya The Great Leap Forward na Cultural Revolution, au unataka kujitoa ufahamu kwamba alichofanya Mao Uchina ni sawa na alichofanya Mugabe kule Zimbabwe. Ukumbuke miondombinu waliyorithi wakina Mao ndiyo hiyo iliyotumika kuwasaidia wakina Chian-Kai Shek kushinda vita ya pili ya dunia ambayo naye alilirithi kutoka Qing-Dynasty (Ufalme uliotawala Uchina tokea 1644-1912)

Singapore ya Lee-Kuan Yew inategemea mfereji wa Malacca na Bandari ambapo asilimia 50% ya bidhaa za dunia hii zinapita pale na kuelekea Ulaya na Mashariki ya Mbali. Hivyo wawanakusanya kodi sana kuruhusu uwekezaji kupitia Economic Exclusive Zones (EEZ). Sisi watanzania tunauza nini nje ya nchi ambacho kitatufanya tuendelee kwa kasi kama Singapore wakati Raisi hataki wawekezaji na anachukia kuona watanzania wakitajirika ???

Ukisema eti kwa sababu wao waliwahi kuwa matajili huko nyuma unaleta propaganda hata Misri imewahi kuwa superpower zaidi ya karne nyingi tu, ugiliki, Mali empire lakini umiaka wao mingi wa tajiri hauonyeshi hiki tunachokiona kwenye mifano niliyotoa.

Nikisema umepengukiwa Hekima tafadhali usichukie. Uchina ya Mao-Zedong na Deng-Xiaoping ndiyo ileile ambayo ilikuwa tajiri na ikasainishwa mikataba ya hovyo kama The Treaty of Nanjin 1842. Mikataba iliyosainiwa miaka 200 iliyopita imeibana Uchina mpaka leo hii. Hong-Kong ilichukuliwa miaka zaidi ya 200 na ikarudishwa mwaka 1996. Hivyo miondombinu ya barabara, bandari, reli, vyuo na mengineyo iliyoachwa na wafalme wa Uchina kipindi cha The Opium Wars, The Concessions na The Koumintang ndiyo iliwasiaidia wakina Deng-Xioaping kufanya harakati zao za kiuchumi na kisiasa hadi kufika hapa walipo.

Hizi Misri na Mali za leo hii hazina muendelezo wowote ule kiutawala kwasababu mataifa haya yalishaanguka na kupotea. Lakini Uchina ya leo ndiyo ileile ya The Ming Dynasty and Qing-Dynasty (1644-1912) ambazo ndizo zilisaini mikataba na mataifa ya Ulaya miaka 1800's ambayo inawabana wachina mpaka leo. Au huyaoni ya Hong-Kong mzee ???

MKIAMBIWA MMEPUNGUKIWA HEKIMA MSICHUKIE, MAANA NDIYO UKWELI WENYEWE HUO. (WAPUMBAVU)
YOU PEOPLE ARE SIMPLY MORALLY DEPRAVED AND SPIRITUALLY BANKRUPT

NB: Mtu yoyote mwenye kuipenda Tanzania toka moyoni kamwe hawezi shabikia anachofanya Raisi Magufuli....
 
Asante sana Mkuu kwa habari hii muhimu. Huyu msomi, nilikuwa sijamuweka kwenye kumbukumbu zangu. Ila imeniuma sana kujua aliondoka duniani akiwa na umri mdogo vile tena kwa kansa. Sijui alikuwa threat kwa nani kiasi cha (nahisi) kupandikizwa kansa.
===
Justinian Rweyemamu - Wikipedia
 
Sisi tunaye Palamagamba Mwaliko Kabudii..Professor wa Sheria..😀😀, Harrison Mwakyembe Dr. Prof. Ndalichako etc.
 
Napata tabu sana. Kuona watanzania wenzangu bado akili zao zimeganda. Mpk leo hawajui kama walitaabika Jana sababu ya ahadi za anaetoa ahadi leo! [emoji15][emoji15]
Nani kagombea bila ahadi au we ndo zimeganda unauhakika gani huyo atatekeleza hzo ahadi
 
Asante sana Mkuu kwa habari hii muhimu. Huyu msomi, nilikuwa sijamuweka kwenye kumbukumbu zangu.
===
Justinian Rweyemamu - Wikipedia
Huyu ndiye alikuwa Chief Ecomonist wa Mzee Nyerere, alifanya mambo makubwa sana hapa Tanzania. Alikuwa anaamini kwamba Tanzania itaendelea tu endapo itaweka mkazo kwenye Elimu (Kitu ambacho hata mimi naamini): Tafuta maandiko yake kuhusu Tanzania ndiyo utafahamu kwamba Tanzania ilibahatika kuwa na mtu wa namna gani lakini hatukumtumia vizuri. Tatizo letu ni lile lile ambalo hata Mwalimu Nyerere alilikubali: Tunapenda kupuuza mambo ya msingi na kukumbatia Propaganda zisizo na kichwa wala miguu.

Kama Mzee Nyerere angeamua kuwasikiliza wakina Rweyemamu mbona hili taifa lingekuwa mbali sana. Lakini ndiyo vile tena, tulimpenda zaidi Myahudi Karl Marx pamoja na falsafa zake za Command Economy and Arrested Development ambazo hata wao waliotuletea kutoka Moscow na Beijing ziliwashinda vibaya. Dhana nzima ya KUJITEGEMEA haimaanishi kwamba tusishirikiane na mataifa ya nje kibiashara na kidiplomasia.

IFIKE MAHALI TUBADILIKE ILI NCHI ISONGE MBELE........
 
Kwani tofauti ya Kigoma na Dubai ni ipi?

Mungu Ibariki Tz - MITz
 
Tunajivunia Chenge kwa wizi wake na kwa ujasiri wake kile kipindi cha Operation kuvua gamba kwa kumwambia katibu wa uenezi wa CCM Nape mbele ya kikao cha CCM kikiongozwa na JK 'NIMEVUA GAMBA LKN LIMEFIKA KIUNONI LIMEGOMA KUTOKA MWENYE WA KUWEZA KULITOA AJE ANISAIDIE',wote wakafyata mkia.

Huyo ndio msomi wetu.
 
Sisi tunaye Palamagamba Mwaliko Kabudii..Professor wa Sheria..😀😀, Harrison Mwakyembe Dr. Prof. Ndalichako etc.
Professor Kabudi, mzee wangu yule ni mtu mwenye akili sana na mzalendo pia. Namuheshimu sana na nitaendelea kumheshimu lakini nachelea kusema amepotoka na sasa yupo kwenye kundi la wasomi wa Tanzania waliopungukiwa Hekima ya Kimungu: He's Morally Depraved and Spiritually Bankrupt.

NB: Japo yeye anaamini kabisa kwamba anachofanya ni kulisaidia taifa (He's dead wrong and deceived)
 
Yaani anajua anaongea na watu kawashina upeo wa akili. Believe me kuna watu watampigia kura just because wanaamini ataifaya Tanzania kuwa kama Uholanzi.
Kwa kusikia tu viongozi wetu wanaogopa kwenda kutembelea hata nchi ndogo kama Uholanzi ambayo ni nchi muhimu sana kwa Tanzania kwa ujumla na kwa Magufuli. KLM ni Shirika la Ndege la Uholanzi lenye uzoefu wa muda mrefu zaida ya miaka 100 na linahudumia Tanzania muda mrefu kuliko lingine lolote, uzoefu ambao ungesaidia ATCL ya Magufuli. Makaburu wa Afrika ya Kusini walioendeleza nchi hiyo walihamia toka Uholanzi kwa hiyo Tanzania ingeweza kujifunza mengi na kuwa kama Afrika ya Kusini siyo Ulaya.
Yaani anajua anaongea na watu kawashina upeo wa akili. Believe me kuna watu watampigia kura just because wanaamini ataifaya Tanzania kuwa kama Uholanzi.
 
Miaka 60 ya uhuru Tanzania yenye maziwa makuu wananchi hawana maji safi, ujinga ni mtaji muhimu sana kisiasa.
 
Kaka tunachukia tu unavyotushinda kwa hoja Ila inabidi tukupingepinge ili JPM wetu awe juu. Ila sisi wa TZ tunahitaji yeye atupeleke hivyo hivyo kwa ideas zake za kiuchumi sababu tunashawshiana kuwa wapinzani hawana uzoefu as if Kuna alizaliwa akiwa Rais au ameusomea. Ni kweli hatuwezi kuwa na maendeleo bila mabeberu..tatizo ni namna tunavyowa engage hao mabeberu katika uchumi wetu.
 
Wawekezaji wenyewe wanakaliwa kohoni. Nchi imekosa wawekezaji rasilimali zinaoza tuu.. hii nchi itabadirishwa na vitukuu vyetu kwasisi bado wengi harujaelimika,,,

Mtu anapost video yenye kumwelimisga YouTube mtu anakomment kwa kuomba likess..

Elimu, elimu, elimu, elimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…