By 2015 Kigoma kuwa kama Dubai, Mwanza kuwa kama California

By 2015 Kigoma kuwa kama Dubai, Mwanza kuwa kama California

Huyu ndiye alikuwa Chief Ecomonist wa Mzee Nyerere, alifanya mambo makubwa sana hapa Tanzania. Alikuwa anaamini kwamba Tanzania itaendelea tu endapo itaweka mkazo kwenye Elimu (Kitu ambacho hata mimi naamini): Tafuta maandiko yake kuhusu Tanzania ndiyo utafahamu kwamba Tanzania ilibahatika kuwa na mtu wa namna gani lakini hatukumtumia vizuri. Tatizo letu ni lile lile ambalo hata Mwalimu Nyerere alilikubali: Tunapenda kupuuza mambo ya msingi na kukumbatia Propaganda zisizo na kichwa wala miguu.

Kama Mzee Nyerere angeamua kuwasikiliza wakina Rweyemamu mbona hili taifa lingekuwa mbali sana. Lakini ndiyo vile tena, tulimpenda Karl Marx zaidi pamoja na falsafa zake za Command Economy and Arrested Development ambazo hata wao waliotuletea kutoka Moscow na Beijing ziliwashinda vibaya. Dhana nzima ya KUJITEGEMEA haimaanishi kwamba tusishirikiane na mataifa ya nje kibiashara.

IFIKE MAHALI TUBADILIKE ILI NCHI ISONGE MBELE........
Kabisa. Watu wanaamini tukichukia mabeberu ndo tutaendelea. Yaani kuongea sijui sisi ni matajiri ndo kutatufanya tuendelee.
Kitu ambacho siyo.
Ili kuendelea tunatakiwa tushirikiane na walioendelea. Hao ndo tufanye nao biashara,tuweke mazingira bora ya uwekezaji hapo tutacreate ajira na kuboresha maisha ya watu wetu.
 
Jana nilimsikia Rais Magufuli akisema ndani ya miaka yake mitano ijayo endapo atashinda basi Tanzania kuwa kama Ulaya by 2025.

Hivi Watanzania turudi nyuma kidogo. JK alituambia Kigoma itakuwa kama Dubai by 2015, leo tupo 2020, je Kigoma imeshakuwa kama Dubai?

Watanzania wenzangu tusidanganyike na maneno ya Rais Magufuli. Kusema ukweli Tanzania kuwa kama Germany by 2025 hilo haliwezekani kabisa. Miaka mitano SGR Dar es Salaam mpaka Dodoma bado inawasumbua wataweza kujenga SGR Dodoma Mwanza/Kigoma ndani ya miaka mitano mingine?

Tusidanganyike. Halafu wanatuona hatuna akili kwa kutuahidi mambo matamu ambayo wanajua kabisa hawawezi timiza.
Afadhali hata ile ahadi ya Mzee wa Fyekelea Mbali kwa Tabora kuwa kama jiji la Toronto. Angalau jitihada za upandaji miti na kuzuia ndoa za utotoni zimeonekana. Hizi ahadi za Mzee kwa sasa ni kutaka kutuingiza chaka mazima na tena lenye upupu.
 
Write a comment
IMG-20200712-WA0033.jpeg
 
Haiwezekani taifa likaendelea bila kufanya biashara ya kimataifa, kuuza bidhaa na huduma nje pamoja na kuruhusu uwekezaji. Chanzo kikubwa cha utajiri wa Uchina na Marekani ni biashara za kimataifa na siyo maneno matupu. Marekani ameanza kuwa taifa tajiri kipindi cha The Gilded Age 1870 ambapo alifanya sana biashara za kimataifa na mataifa ya Ulaya. Mwaka 1945 yeye akawa ndiyo The Leading Exporter of Merchandise akawa anamiliki nusu nzima ya GDP ya dunia kwasababu ya kuuza silaha za vita na kutoa mikopo huko Ulaya.

Uchina amefika hapo alipo kwasababu Deng-Xiaoping aliachana na The Concept of Centralized Economy and Arrested Development. Halafu Uchina ilikuwa na miondombinu mizuri sana iliyoachwa na serikali ya Chian-Kai Shek lakini Mao-Zedong aliamua kuivuruga kupitia sera yake ya The Great Leap Forward na Cultural Revolution, au unataka kujitoa ufahamu kwamba alichofanya Mao Uchina ni sawa na alichofanya Mugabe kule Zimbabwe. Ukumbuke miondombinu waliyorithi wakina Mao ndiyo hiyo iliyotumika kuwasaidia wakina Chian-Kai Shek kushinda vita ya pili ya dunia ambayo naye alilirithi kutoka Qing-Dynasty (Ufalme uliotawala Uchina tokea 1644-1912)

Singapore ya Lee-Kuan Yew inategemea mfereji wa Malacca na Bandari ambapo asilimia 50% ya bidhaa za dunia hii zinapita pale na kuelekea Ulaya na Mashariki ya Mbali. Hivyo wawanakusanya kodi sana kuruhusu uwekezaji kupitia Economic Exclusive Zones (EEZ). Sisi watanzania tunauza nini nje ya nchi ambacho kitatufanya tuendelee kwa kasi kama Singapore wakati Raisi hataki wawekezaji na anachukia kuona watanzania wakitajirika ???



Nikisema umepengukiwa Hekima tafadhali usichukie. Uchina ya Mao-Zedong na Deng-Xiaoping ndiyo ileile ambayo ilikuwa tajiri na ikasainishwa mikataba ya hovyo kama The Treaty of Nanjin 1842. Mikataba iliyosainiwa miaka 200 iliyopita imeibana Uchina mpaka leo hii. Hong-Kong ilichukuliwa miaka zaidi ya 200 na ikarudishwa mwaka 1996. Hivyo miondombinu ya barabara, bandari, reli, vyuo na mengineyo iliyoachwa na wafalme wa Uchina kipindi cha The Opium Wars, The Concessions na The Koumintang ndiyo iliwasiaidia wakina Deng-Xioaping kufanya harakati zao za kiuchumi na kisiasa hadi kufika hapa walipo.

Hizi Misri na Mali za leo hii hazina muendelezo wowote ule kiutawala kwasababu mataifa haya yalishaanguka na kupotea. Lakini Uchina ya leo ndiyo ileile ya The Ming Dynasty and Qing-Dynasty (1644-1912) ambazo ndizo zilisaini mikataba na mataifa ya Ulaya miaka 1800's ambayo inawabana wachina mpaka leo. Au huyaoni ya Hong-Kong mzee ???

MKIAMBIWA MMEPUNGUKIWA HEKIMA MSICHUKIE, MAANA NDIYO UKWELI WENYEWE HUO. (WAPUMBAVU)
YOU PEOPLE ARE SIMPLY MORALLY DEPRAVED AND SPIRITUALLY BANKRUPT

NB: Mtu yoyote mwenye kuipenda Tanzania toka moyoni kamwe hawezi shabikia anachofanya Raisi Magufuli....
""""Haiwezekani taifa likaendelea bila kufanya biashara ya kimataifa, kuuza bidhaa na huduma nje pamoja na kuruhusu uwekezaji. Chanzo kikubwa cha utajiri wa Uchina na Marekani ni biashara za kimataifa na siyo maneno matupu."""
Maelezo haya yanakinzana na misingi yote ya hoja zako uliyoweka mkuu.
Umedai kilichomsadia Deng ni miundombinu imara iliyowekwa na watangulizi, huku Sera Mbovu za Mao zilishindwa kuifanya miundombinu hiyo iwe nufaishi kwa China.

Sasa wachumi wote wanakubaliana na maelezo yako uwekezaji katika miundombinu imara ni uti wa mgongo au reli ya maendeleo katika maeneo uliyotaja Biashara za kimataifa, Kuuza Bidhaa nje Kuruhusu Uwekezaji mkubwa.

Sasa kwa miaka mitano JPM amekuwa akifanya hayo hadi mnamuita rais wa Ujenzi. Sasa kwa nini uamini Wakina Deng Xioping na wakina Zhao Ziyang waweze kutumia miundombinu ya mababu zao kuinufaisha china kwa Sera nzuri walizoziweka Ila Unabisha kuamini JPM anaweza kuleta maendeleo makubwa kwa Miundombinu alliyoiweka yeye na yawatangulizi wake japo sio ktk viwango vya china na marekani.


Najaribu kutafuta unajenga hoja za kumpinga kutokea upande au jukwaa lipi sioni mkuu.
 
Kutoka Ilani ya CCM 2015/2020.
Standard Gauge ilitakiwa iwe imeshaanza kujengwa kote hapa
20200807_110008.jpg
 
Kumbe 2015/2020 ilitakiwa tuwe na chuo kikuu cha Kilimo Butiama.Tuwe na chuo kikuu cha madini Shinyanga. Je tunavyo ????Halafu tunaambiwa by 2025 tutakuwa kama Finland.
20200807_105830.jpg
 
Haya sasa je vijana wana ajira ?kutoka ilani ya CCM 2015/2020.
Ninaomba tuwajaji CCM kwa ilani yao ya 2015/2020 .
Yaani hata asilimia 5 ya ilani yao hawajatimiza.
20200807_105647.jpg
 
Wapumbavu mko wengi,kama anaweza kufanya mwanza kama ulaya ndani ya miaka 5 ijayo basi miaka 5 iliyopita ingeshakuwa kama ulaya,mbona mnakuwa wapumbavu hivi
Bibie kwani nini khofu yako??

Hakuna linaloshindikana chini ya jua. Hivi kwa nini uone unadanganywa???

Kura kwa Magufuli October 2020.

[emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]
 
Uchina ni taifa lenye miaka zaidi ya 6000 na katika vipindi hivyo limekuwa na milima na mabonde. Mpaka kufika karne ya 15 ndiyo lilikuwa taifa tajiri na lenye teknolojia kubwa zaidi duniani: Wakomunisti unaowaona walipochukua nchi mwaka 1949 ilikuwa ni taifa masikini lakini lenye miondombinu ya kuliwezesha kuendelea kwa haraka. Usisahau kwamba Uchina ilianza kukua kiuchumi miaka ya 1979 baada ya Deng-Xiaoping kufungua milango na kuruhusu mataifa ya nje kama Japani, Uingereza na Marekani wawekeze kwa wingi Uchina. Hivyo Today's China is just rebounding lilishwahi kuwa taifa tajiri zaidi duniani likufuatiwa na India.

Deng-Xiaoping aliwaonya sana Wachina kuachana na ujinga wa kuwatukana watu ambao wangeweza kuusaidia Uchumi wao. Aliachana na propaganda za kipumbavu za Kikomunisti za wakina Mao-Zedong na Zhou-Enlai na akauvaa uhalisia kwamba bila mataifa ya Magharibi Uchina isingeweza kurudi katika hali yake ya utajiri mkubwa ambao ilikuwa nao miaka 200 iliyopita. Ndipo akaja na sera maarufu kabisa ya "BIDE AND HIDE" na kuanza kuruhusu wawekezaji kutoka nje.

Raisi wetu akiwa na genge lake la wale TISS wenye akili za Vita Baridi (The Soldiers of the bygone regime) wameamua kuirudisha nchi yetu kwenye siasa za kijamaa zilizokuwa zimejaa propaganda mufilisi za Vita Baridi. Hawa watu wanaomshauri mkuu wa nchi ni watu waliopungukiwa hekima na maarifa, They are Morally Depraved and Spiritually Bankrupt. Hivi kuna taifa ambalo linaweza kuendelea kiuchumi hapa duniani bila kushirikiana na mabepari ??? Umoja wa Kisovieti ulijaribu kufanya hivi lakini pumzi iliwakatikia miaka ya 70 hadi kupelekea kuanguaka.

Unapotolea mfano wa nchi kama Singapore unazidi kutudhihirishia ule msemo kwamba "In Tanzania intellectuals are an endangered specie". Hivi kuna mtu mwenye akili timamu anaweza kulinganisha Singapore ya Lee Kuan Yew na Tanzania ya Magufuli kweli ??? Basi ni lazima atakuwa mwendawazimu aliyepungukiwa na akili. Singapore imefika hapo ilipo kwa kucheza karata yake vizuri katika kushirikiana na mataifa hasimu kama Uchina na Marekani ambayo yanatumia sana mfereji wa Malacca. Hakufungamana na upande wowote ule katika siasa za kimataifa na kipaumbele chake kikubwa kilikuwa ni ELIMU (Maendeleo ya watu) siyo maendeleo ya vitu. Ndiyo maana leo hii Singapore inatoa wasomi nguli kama Dr. Kishore Mahbubani ambao Alma Mater zao ni Harvard University. Ninyi mna wakina nani hata kujivunia kimataifa ???

ACHA UPUMBAVU........
Tuna msomi Chenge mkuu, japo watu wanamwita fisadi. Tuna Rostam pia, ni brain inayoheshimika hadi nchi za dunia ya kwanza
 
Sasa wachumi wote wanakubaliana na maelezo yako uwekezaji katika miundombinu imara ni uti wa mgongo au reli ya maendeleo katika maeneo uliyotaja Biashara za kimataifa, Kuuza Bidhaa nje Kuruhusu Uwekezaji mkubwa.

Najaribu kutafuta unajenga hoja za kumpinga kutokea upande au jukwaa lipi sioni mkuu.
Neno miondombinu "Infrastructure" ni "Operational" hivyo halijikiti kwenye vitu tu. Tunaposema neno "Mioundombinu" kwenye dhana nzima ya maendeleo tunazungumzia mipangilio ya vitu (Tangible or Intangile (Abstract) ) vinavyoiwezesha jamii kuendelea. Hivyo mfumo mzima wa elimu kuanzia vidudu hadi chuo kikuu inategemea "miundombinu" iliyowekwa katika utoaji elimu: Hapa hatuzungumzii Hostel kama zile za Magufuli peke yake, bali rasilimali ambazo zinawezesha utoaji mzuri wa elimu. Kila sehemu ya jamii inahitaji "Miundombinu" ili kuendelea, hata utoaji haki (The Judicial System) una miundombinu yake.

Sasa ninaposema neno "Miundombinu" kule Uchina namaanisha ule mpangilio mzima wa jamii ya Uchina ambao umewezesha nchi kufika hapa ilipo. Kuanzia suala zima la Uraia, Utoaji Elimu (Kama ulinisoma vizuri nilitaja vyuo), njia za Uchukuzi kama reli, barabara na bandari (ambazo wewe unahisi ndiyo miondombinu yenyewe). Sasa bila miundombinu ambayo imeeachwa na Mzee Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete sidhani kama Raisi Magufuli angeweza kujivika taji isiyo yake kama ambavyo anafanya leo.

Nikisema "Miundombinu yote Ukusanyaji wa Kodi" hapa nchini nazungumzia taasisi mbalimbali na sheria ambazo zinaiwezesha Serikali kukusanya mapato na tozo kutoka kwa wananchi wake kwa njia rahisi kabisa. Hivyo Tanzania Revenua Authority in Operational Terms forms part of Revenue Infrastructure of Tanzania.

NB: UNAPOTOKA SANA UNAPODHANI NJIA ZA UCHUKUZI PEKE YAKE NDIYO MIUNDOMBINU (Think Big My Friend)
 
Wapumbavu mko wengi,kama anaweza kufanya mwanza kama ulaya ndani ya miaka 5 ijayo basi miaka 5 iliyopita ingeshakuwa kama ulaya,mbona mnakuwa wapumbavu hivi
Kabisa. Tena kumjaji Magufuli ni rahisi sana. Miaka 5 kafanya nini la maana kabisa ambalo litatufanya tuamini Tanzania itakuwa kama Ulaya ?
 
Neno miondombinu "Infrastructure" ni "Operational" hivyo halijikiti kwenye vitu tu. Tunaposema neno "Mioundombinu" kwenye dhana nzima ya maendeleo tunazungumzia mipangilio ya vitu (Tangible or Intangile (Abstract) ) vinavyoiwezesha jamii kuendelea. Hivyo mfumo mzima wa elimu kuanzia vidudu hadi chuo kikuu inategemea "miundombinu" iliyowekwa katika utoaji elimu: Hapa hatuzungumzii Hostel kama zile za Magufuli peke yake, bali rasilimali ambazo zinawezesha utoaji mzuri wa elimu. Kila sehemu ya jamii inahitaji "Miundombinu" ili kuendelea, hata utoaji haki (The Judicial System) una miundombinu yake.

Sasa ninaposema neno "Miundombinu" kule Uchina namaanisha ule mpangilio mzima wa jamii ya Uchina ambao umewezesha nchi kufika hapa ilipo. Kuanzia suala zima la Uraia, Utoaji Elimu (Kama ulinisoma vizuri nilitaja vyuo), njia za Uchukuzi kama reli, barabara na bandari (ambazo wewe unahisi ndiyo miondombinu yenyewe). Sasa bila miundombinu ambayo imeeachwa na Mzee Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete sidhani kama Raisi Magufuli angeweza kujivika taji isiyo yake kama ambavyo anafanya leo.

Nikisema "Miundombinu yote Ukusanyaji wa Kodi" hapa nchini nazungumzia taasisi mbalimbali na sheria ambazo zinaiwezesha Serikali kukusanya mapato na tozo kutoka kwa wananchi wake kwa njia rahisi kabisa. Hivyo Tanzania Revenua Authority in Operational Terms forms part of Revenue Infrastructure of Tanzania.

NB: UNAPOTOKA SANA UNAPODHANI NJIA ZA UCHUKUZI PEKE YAKE NDIYO MIUNDOMBINU (Think Big My Friend)
Mimi niliposema Miundombinu nilimaanisha Miundombinu ndio maana wizara zote zio za miundombinu au nchi nzima kila kitu sio miundombinu kwa tafsiri ya uelewa wa kawaida kabisa. Na hiki ndicho mnasema wachumi Infrastructure is a stimulant for Economic Development. ukitanua goli kusema kila kitu ni miundombinu sawa ila utaongezea migogoro kwenye hoja zako.

AHA NIPOKEE HOJA YA MIUNDOMBINU DEMOCRACY, JUDICIALLY, ELIMU etc
Hukohuko china Unakumbuka Tianjin Massacre wanafunzi walikuwa wanadai miundombinu democracy maana ilikuwa haipo.
Watu wanapotezwa Muundombinu amani haupo akiwemo PM aliyefia Kifungo cha ndani kisa tu anamawazo tofauti.
Hukohuko zingapole ilikuwa ni zaidi ya udikteta dunia nzima muundombinu Judicially ulikuwa mfukoni mwa Dicteta Lee Kuan yew lakini aliboresha miundombinu Elimu.

Lazima tupruni mambo tusifanye yasiyo matatizo nayo yakawa matatizo.
Kwa sasa chini ya utawala huu Kuna maeneo mengi yameboreshwa tuchukulie tunayaita miundombinu, lakni tukijumuisha na Miundombinu ninayozungumzia BAdo hakusa sababu ya kupinga kuwa JPM hawezi kufanya kitu kikubwa cha ziada kwa kipindi cha miaka mitano iliyobaki ikiwa Dhamiri yake haitabadilika mkuu.

MFANO MIUNDOMBUNU YA KUKUSANYA MAPATO
Juzi nilikuwa latra tunasajili vyombo vya usafiri katika mfumo rafiki wa kukusanya mapato Online kupitiua huduma namba, Nimeona pia WCF na taasisi nyingi za kiserikali zimejipanga kwenye kuboresha mifumo ya kupata mapato na kupunguza urasimu. Zikiwekewa miguu vizuri JPM atakuwa na kazi ndogo sana Baada ya kazi kubwa aliyifanya kwa machozi miaka mitano iliyopita.
 
Back
Top Bottom