By 2015 Kigoma kuwa kama Dubai, Mwanza kuwa kama California

Kabisa. Watu wanaamini tukichukia mabeberu ndo tutaendelea. Yaani kuongea sijui sisi ni matajiri ndo kutatufanya tuendelee.
Kitu ambacho siyo.
Ili kuendelea tunatakiwa tushirikiane na walioendelea. Hao ndo tufanye nao biashara,tuweke mazingira bora ya uwekezaji hapo tutacreate ajira na kuboresha maisha ya watu wetu.
 
Afadhali hata ile ahadi ya Mzee wa Fyekelea Mbali kwa Tabora kuwa kama jiji la Toronto. Angalau jitihada za upandaji miti na kuzuia ndoa za utotoni zimeonekana. Hizi ahadi za Mzee kwa sasa ni kutaka kutuingiza chaka mazima na tena lenye upupu.
 
""""Haiwezekani taifa likaendelea bila kufanya biashara ya kimataifa, kuuza bidhaa na huduma nje pamoja na kuruhusu uwekezaji. Chanzo kikubwa cha utajiri wa Uchina na Marekani ni biashara za kimataifa na siyo maneno matupu."""
Maelezo haya yanakinzana na misingi yote ya hoja zako uliyoweka mkuu.
Umedai kilichomsadia Deng ni miundombinu imara iliyowekwa na watangulizi, huku Sera Mbovu za Mao zilishindwa kuifanya miundombinu hiyo iwe nufaishi kwa China.

Sasa wachumi wote wanakubaliana na maelezo yako uwekezaji katika miundombinu imara ni uti wa mgongo au reli ya maendeleo katika maeneo uliyotaja Biashara za kimataifa, Kuuza Bidhaa nje Kuruhusu Uwekezaji mkubwa.

Sasa kwa miaka mitano JPM amekuwa akifanya hayo hadi mnamuita rais wa Ujenzi. Sasa kwa nini uamini Wakina Deng Xioping na wakina Zhao Ziyang waweze kutumia miundombinu ya mababu zao kuinufaisha china kwa Sera nzuri walizoziweka Ila Unabisha kuamini JPM anaweza kuleta maendeleo makubwa kwa Miundombinu alliyoiweka yeye na yawatangulizi wake japo sio ktk viwango vya china na marekani.


Najaribu kutafuta unajenga hoja za kumpinga kutokea upande au jukwaa lipi sioni mkuu.
 
Kutoka Ilani ya CCM 2015/2020.
Standard Gauge ilitakiwa iwe imeshaanza kujengwa kote hapa
 
Kumbe 2015/2020 ilitakiwa tuwe na chuo kikuu cha Kilimo Butiama.Tuwe na chuo kikuu cha madini Shinyanga. Je tunavyo ????Halafu tunaambiwa by 2025 tutakuwa kama Finland.
 
Haya sasa je vijana wana ajira ?kutoka ilani ya CCM 2015/2020.
Ninaomba tuwajaji CCM kwa ilani yao ya 2015/2020 .
Yaani hata asilimia 5 ya ilani yao hawajatimiza.
 
Wapumbavu mko wengi,kama anaweza kufanya mwanza kama ulaya ndani ya miaka 5 ijayo basi miaka 5 iliyopita ingeshakuwa kama ulaya,mbona mnakuwa wapumbavu hivi
Bibie kwani nini khofu yako??

Hakuna linaloshindikana chini ya jua. Hivi kwa nini uone unadanganywa???

Kura kwa Magufuli October 2020.

[emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]
 
Tuna msomi Chenge mkuu, japo watu wanamwita fisadi. Tuna Rostam pia, ni brain inayoheshimika hadi nchi za dunia ya kwanza
 
Neno miondombinu "Infrastructure" ni "Operational" hivyo halijikiti kwenye vitu tu. Tunaposema neno "Mioundombinu" kwenye dhana nzima ya maendeleo tunazungumzia mipangilio ya vitu (Tangible or Intangile (Abstract) ) vinavyoiwezesha jamii kuendelea. Hivyo mfumo mzima wa elimu kuanzia vidudu hadi chuo kikuu inategemea "miundombinu" iliyowekwa katika utoaji elimu: Hapa hatuzungumzii Hostel kama zile za Magufuli peke yake, bali rasilimali ambazo zinawezesha utoaji mzuri wa elimu. Kila sehemu ya jamii inahitaji "Miundombinu" ili kuendelea, hata utoaji haki (The Judicial System) una miundombinu yake.

Sasa ninaposema neno "Miundombinu" kule Uchina namaanisha ule mpangilio mzima wa jamii ya Uchina ambao umewezesha nchi kufika hapa ilipo. Kuanzia suala zima la Uraia, Utoaji Elimu (Kama ulinisoma vizuri nilitaja vyuo), njia za Uchukuzi kama reli, barabara na bandari (ambazo wewe unahisi ndiyo miondombinu yenyewe). Sasa bila miundombinu ambayo imeeachwa na Mzee Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete sidhani kama Raisi Magufuli angeweza kujivika taji isiyo yake kama ambavyo anafanya leo.

Nikisema "Miundombinu yote Ukusanyaji wa Kodi" hapa nchini nazungumzia taasisi mbalimbali na sheria ambazo zinaiwezesha Serikali kukusanya mapato na tozo kutoka kwa wananchi wake kwa njia rahisi kabisa. Hivyo Tanzania Revenua Authority in Operational Terms forms part of Revenue Infrastructure of Tanzania.

NB: UNAPOTOKA SANA UNAPODHANI NJIA ZA UCHUKUZI PEKE YAKE NDIYO MIUNDOMBINU (Think Big My Friend)
 
Wapumbavu mko wengi,kama anaweza kufanya mwanza kama ulaya ndani ya miaka 5 ijayo basi miaka 5 iliyopita ingeshakuwa kama ulaya,mbona mnakuwa wapumbavu hivi
Kabisa. Tena kumjaji Magufuli ni rahisi sana. Miaka 5 kafanya nini la maana kabisa ambalo litatufanya tuamini Tanzania itakuwa kama Ulaya ?
 
Mimi niliposema Miundombinu nilimaanisha Miundombinu ndio maana wizara zote zio za miundombinu au nchi nzima kila kitu sio miundombinu kwa tafsiri ya uelewa wa kawaida kabisa. Na hiki ndicho mnasema wachumi Infrastructure is a stimulant for Economic Development. ukitanua goli kusema kila kitu ni miundombinu sawa ila utaongezea migogoro kwenye hoja zako.

AHA NIPOKEE HOJA YA MIUNDOMBINU DEMOCRACY, JUDICIALLY, ELIMU etc
Hukohuko china Unakumbuka Tianjin Massacre wanafunzi walikuwa wanadai miundombinu democracy maana ilikuwa haipo.
Watu wanapotezwa Muundombinu amani haupo akiwemo PM aliyefia Kifungo cha ndani kisa tu anamawazo tofauti.
Hukohuko zingapole ilikuwa ni zaidi ya udikteta dunia nzima muundombinu Judicially ulikuwa mfukoni mwa Dicteta Lee Kuan yew lakini aliboresha miundombinu Elimu.

Lazima tupruni mambo tusifanye yasiyo matatizo nayo yakawa matatizo.
Kwa sasa chini ya utawala huu Kuna maeneo mengi yameboreshwa tuchukulie tunayaita miundombinu, lakni tukijumuisha na Miundombinu ninayozungumzia BAdo hakusa sababu ya kupinga kuwa JPM hawezi kufanya kitu kikubwa cha ziada kwa kipindi cha miaka mitano iliyobaki ikiwa Dhamiri yake haitabadilika mkuu.

MFANO MIUNDOMBUNU YA KUKUSANYA MAPATO
Juzi nilikuwa latra tunasajili vyombo vya usafiri katika mfumo rafiki wa kukusanya mapato Online kupitiua huduma namba, Nimeona pia WCF na taasisi nyingi za kiserikali zimejipanga kwenye kuboresha mifumo ya kupata mapato na kupunguza urasimu. Zikiwekewa miguu vizuri JPM atakuwa na kazi ndogo sana Baada ya kazi kubwa aliyifanya kwa machozi miaka mitano iliyopita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…