Jamani....mimi kama shabiki wa kutupwa wa Yanga niliyetukuka nikikaa kimya kuhusu hili nitakuwa sijatenda haki kabisa.
Mpira jana nimeuangalia,na hakika vijana wetu walifanya poa sana.
Tatizo walianza kuzubaa kuanzia dakika ya 80 na nilimuambia mwenzangu niliyekuwa naangalia nae kwamba hapa tunafungwa.
Binafsi naona Yondani ndiye aliyetugharimu.
Utamlindaje mtu halafu ukae nyuma yake kwa angle ile kutoka kwa mwenye mpira?
Angekuwa sharp akawahi kukaa mbele ya yule jamaa aliyeunganisha krosi ile kwa kichwa huenda leo hii yangekuwa mengine.
Lakini,hakuna jinsi,yaliyotokea yametokea.
Niliumia sana kwa lile goli,niliwaza harakaharaka ni kitu gani ninachokipenda kinachoweza kunitolea stress nikatafuta Korean series moja kali sana (Birth of a beauty) imenifariji na nimeamka poa kabisa.
Pongezi za kipekee zimfikie kipa wetu Munish (Dida) kwa kazi nzito na iliyotukuka aliyoifanya jana.
Wanayanga wenzangu,tumeonesha kwamba mpira tunauweza,kama sio vijana kuchanganyikiwa kwa mashambulizi yale ya haraka.....ila ukweli wako vizuri sana.
Na yeyote atakayethubutu kutukejeli atakuwa mnafiki tu,moyoni atakiri Yanga ni habari nyingine.
Period