CAF Champions League: Al Ahly vs Yanga 20/04/16

CAF Champions League: Al Ahly vs Yanga 20/04/16

timu mbovu ilingane na Toto Africans?
Coastal Union imezifunga Simba, Yanga, Azam na Mtibwa. Inashika mkia kwenye ligi, ipo nusu fainali kwenye FA. Sasa nataka uniambie, Coastal Union ni mbovu au sio mbovu?
 
Mkuu umeongea kitu cha maana sana,hii kauli ya tumejitahd ndio inaharibu hii timu,tulitolewa kwa penalty tukasema tumejitahd Leo tumetolewa tena tunasema tumejitahd,tunaenda kwenye shirikisho nako tukifungwa mbili moja tukatolewa tutasema tumejitahdi,Mimi tangu nianze kuzijua hizi team tangu miaka ya 90 zinajitahd tu.zitaweza lini? Lazima tukubali kuwa sisi huwa tunaenda kushiriki ila hawa wenzetu huwa wanataka kuchukua Kombe.
 
Nasikia wakirudi wanapitia Pemba moja kwa moja kudai pesa zao na kufufua zile maiti walizofukia kutafuta ushindi Misri.


Hawa wachovu mpira wao mpaka wale wataalam wa kupuliza vile vitu ndiyo maana hawafanikiwi kamwe. Kelele zao wao ni hapa Bongo tu, wakipanda ndege na kuvuka bahari basi juwa wanakwenda kubebeshwa magunia ya magoli huko ugenini.
 
Jana Yanga imepoteza lakini wachezaji wamegain, waliojituma mawakala wamewaona, ndio sababu straika wenu wa Simba ameweka wazi kama mkikosa nafasi ya kupanda ndege hatosaini tena Simba, maana ndondo Cup zinahudhuliwa na mawakala wa Mwadui fc na Twiga stars.
 
Jana Yanga imepoteza lakini wachezaji wamegain, waliojituma mawakala wamewaona, ndio sababu straika wenu wa Simba ameweka wazi kama mkikosa nafasi ya kupanda ndege hatosaini tena Simba, maana ndondo Cup zinahudhuliwa na mawakala wa Mwadui fc na Twiga stars.
Aende tu kwa Mpira gani alionao[emoji1] [emoji1] [emoji1] mkumbushe bangi na bia hazichezi Mpira
 
Jamani....mimi kama shabiki wa kutupwa wa Yanga niliyetukuka nikikaa kimya kuhusu hili nitakuwa sijatenda haki kabisa.

Mpira jana nimeuangalia,na hakika vijana wetu walifanya poa sana.
Tatizo walianza kuzubaa kuanzia dakika ya 80 na nilimuambia mwenzangu niliyekuwa naangalia nae kwamba hapa tunafungwa.
Binafsi naona Yondani ndiye aliyetugharimu.
Utamlindaje mtu halafu ukae nyuma yake kwa angle ile kutoka kwa mwenye mpira?
Angekuwa sharp akawahi kukaa mbele ya yule jamaa aliyeunganisha krosi ile kwa kichwa huenda leo hii yangekuwa mengine.
Lakini,hakuna jinsi,yaliyotokea yametokea.
Niliumia sana kwa lile goli,niliwaza harakaharaka ni kitu gani ninachokipenda kinachoweza kunitolea stress nikatafuta Korean series moja kali sana (Birth of a beauty) imenifariji na nimeamka poa kabisa.

Pongezi za kipekee zimfikie kipa wetu Munish (Dida) kwa kazi nzito na iliyotukuka aliyoifanya jana.
Wanayanga wenzangu,tumeonesha kwamba mpira tunauweza,kama sio vijana kuchanganyikiwa kwa mashambulizi yale ya haraka.....ila ukweli wako vizuri sana.
Na yeyote atakayethubutu kutukejeli atakuwa mnafiki tu,moyoni atakiri Yanga ni habari nyingine.
Period
 
Back
Top Bottom