CAF Confederation Cup yafutwa. Msimu ujao kutakuwa na mashindano mawili tu

CAF Confederation Cup yafutwa. Msimu ujao kutakuwa na mashindano mawili tu

AFL haingalii msimamo wa Ligi za ndani ukiwa na point za kutosha Caf unafuzu moja kwa moja kushiriki AFL.
Klabu bingwa itabaki kwa zile timu zilizokosa points za kushiriki AFL na kwa mantiki hiyo kuanzia mwakani usitegemee kuziona Al Ahly,Wydad,Mamelod,Raja AC au Simba kwenye Champions league timu zote hizo na nyingne jumla 24 zitajiandaa kushiriki AFL badala ya Cafcl
Kwa maelezo yako yapi ni mashindano yenye hadhi zaidi?
 
Msimu wa 2024/2025 kutakuwa na mashindano ya African football league na CAF champions league.

African football league itahusisha timu 24 ambazo zitatoka kwenye zone tatu kulingana na rank zao za CAF.

Zone 1) North Africa
Zone 2) West / Central Africa
Zone 3) South / East Africa

Kwa sheria kila zone itatoa timu 8 ambazo zitapatikana kutokana na Rank walizonazo.

Mpaka sasa mashindano yakiwa yanaendelea ya CAF kuna timu 4 zinazoweza kubadilisha msimamo wa ranking ambazo ni Tp Mazembe mwenye point 38 mpaka sasa, Zamalek wenye point 38 mpaka sasa, Berkane mwenye point 37 hadi sasa na USM Alger mwenye point 36. Hizo timu zinaweza zikaongeza points na atakaye athrika na hilo ni Simba na Peteo Luanda pekee kwavile ndio wenye point 39 kila mmoja. Juu ya Simba kuna Mamelodi ambaye hakuna anayeweza kuzifikia point zake anapoint 54.

Pamoja na hilo Simba bado atakuwa na faida kutokana na zone anayotokea hakuna timu nyingi juu yake.

Upande wa Yanga, kwa vyovyote itakavyokuwa atabakia nafasi yake ile ile ya 13 akiwa na point 31.

Tuangalie zone za CAF
1) COSAFA (Council of Southern Africa Football Associations)
Hii zone inahusisha nchi zifuatazo
Angola, Madagascar, Malawi, South Africa Mauritius, Mozambique, Namibia, Seychelles, Zambia, Zimbabwe, Botswana,Comoros,Eswatini,Lesotho

Kwenye hii zone ni Angola na South Africa pekee ndio waliokuwa na timu zenye rank ya juu ambapo ni Petro Luanda na Mamelod.

2)CECAFA (The Council for East and Central Africa Football Associations )

Hii zone inahusisha nchi zifuatazo Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, SouthSudan, Tanzania, Uganda, Zanzibar

Kwenye hii zone ni Simba na Yanga ndio wapo juu kwenye rank.

3) UNIFFAC(Central African Football Federations' Union)

Inahusisha nchi zifuatazo
Cameroon, Central African Republic,Chad, DR Congo, Equatorial, Gabon, São Tome

Kwenye hii zone ni DR Congo pekee akiwasilishwa na Tp Mazembe ndio yupo rank ya juu.

4) UNAF (Union of North Africain football)

Hapa ndio rank iliyosheheni wababe wa kwenye rank. Timu za kiarabu ndio zipo kwenye hii zone na ndio waliotawala kwenye rank ya CAF. Hii zone inahusisha Algeria,Tunisia, Egypt, Morocco na Libya.

5) WAFU (West African football union)
Hii zone kwenye ranking inawakilishwa na Asec na rivers united ambao wote hao hawaizidi Simba na Yanga point. Hii zone inahusisha nchi zifuatazo.

Cape Verde, Gambia, Guinea, Guinea Bissau, Mali, Mauritania, Liberia, Senegal, Sierra Leone, Ghana, Burkina Faso, Benin, Ivory coast, Niger, Nigeria, Togo.

Hivyo ukiachana na North zone, Simba na Yanga imeweza kuziacha timu nyingi sana za kutoka zone zinginezo hivyo swala la kushiriki michuano ya African football league ni uhakika.

Ikumbukwe msimu ujao kutakuwa na mashindano mawili pekee AFL na CAFCL) na haipaswi timu kushiriki mashindano yote mawili.
Simba ataazia robo tena kwenye AFL

Aaaahaaa
 
Huko juu ulisema zichukuliwe timu zenye rank za juu ndio zipambane maanake kwa hilo wazo lako timu zisingezidi 10+
Yes Nmesema hvy ila pia nikasema na vinginevyo watakavyoona, yn iwepo hy option yangu pamoja na nyngn watakavyoona
 
Kwa hali ilivyo msimu ujao Simba na Yanga zitashiriki AFL bila kujali ligi itaishaje tayari hizo timu mbili zina point za kutosha kuwafanya kuwepo miongoni mwa hizo timu 24
Azam na kati ya hawa Coastal union, KMC au Tanzania Prisons anaweza shiriki nao klabu bingwa barani Africa kwa msimamo wa NBC ulivyo
Nilichokiona hii AFL inaweza punguza ushindani wa vilabu kwenye domestic league maana timu hata ikimaliza nafasi ya kumi ina uhakika wa kucheza AFL kulingana na point zake alizonazo kwenye michuano ya Caf

Kwa mfano kwenye ligi yetu kwa sasa kati ya Simba na Azam baada ya kukosa ligi msimu huu inakuwa haina maana tena kugombania nafasi ya pili maana haitabadilisha chochote tayari Simba anajijua mwakani atashiriki wapi (AFL) na azam anajijua pia hata amalize wa 4 atashiriki klabu bingwa na bado hatujajua bingwa wa CRDB federation cup yeye atapata nafasi gani huko kimataifa?
lazima waweke utaratibu wa kudrop out so itabid mtu apambane ili asidrop
 
Kwa mtazamo wangu hii AFL ndo itakuwa ligi kubwa lakn bingwa wa ligi ndo atashiriki huko na wale wa pili wataenda CAFCL
 
Kwa mtazamo wangu hii AFL ndo itakuwa ligi kubwa lakn bingwa wa ligi ndo atashiriki huko na wale wa pili wataenda CAFCL
Sasa kwa kufanya hivyo si itakuwa ni sawasawa na CAFCL na CAFCC ila wamebadilisha majina ya mashindano?
Maana kawaida bingwa wa ligi kuu hucheza CAFCL na wale wanaoshika nafasi ya pili hushiriki CAFCC
 
Sasa kwa kufanya hivyo si itakuwa ni sawasawa na CAFCL na CAFCC ila wamebadilisha majina ya mashindano?
Maana kawaida bingwa wa ligi kuu hucheza CAFCL na wale wanaoshika nafasi ya pili hushiriki CAFCC
bahati mbaya unaweza shinda ligi ila usishiriki AFL...... imagine azam ashinde nbc pl, hawezi shiriki AFL

kiukweli CAF ya Motsepe inalenga kuua ligi za ndani, ndio mana ulaya walikataa hii kitu, hili shindano la AFL litakufa ndani ya miaka 5 ijayo! vilabu vingi vitapiga kelele.......

soka la afrika kwa sasa ni kama linaongozwa na Infantino, ndiye mwenye hamu sana na AFL
 
Waafrika ni bure tu, ni bora tuendelee copy and pastekutoka Ulaya vile vile, kuanzia kujifanya tuna mipango na fikra ndiipo tunapoharibu kabisa
 
Hu
bahati mbaya unaweza shinda ligi ila usishiriki AFL...... imagine azam ashinde nbc pl, hawezi shiriki AFL

kiukweli CAF ya Motsepe inalenga kuua ligi za ndani, ndio mana ulaya walikataa hii kitu, hili shindano la AFL litakufa ndani ya miaka 5 ijayo! vilabu vingi vitapiga kelele.......

soka la afrika kwa sasa ni kama linaongozwa na Infantino, ndiye mwenye hamu sana na AFL
Hiyo wala sio bahati mbaya ndio utaratibu wa AFL.

Mfano mzuri AS Far Rabat ya Morocco wanaongoza ligi na wapo na asilimia kubwa kuchukua ubingwa wa Morocco msimu huu ila hata hivyo hawatashiriki AFL badala yake ni Wydad Casablanca na RS Berkane ndio wenye points za kutosha Caf kushiriki AFL.

Kumbuka Wydad msimu huu walikuwa hawawezi hata kumaliza kwenye timu 2 za juu kwenye msimamo.
 
... 🚨 𝙊𝙁𝙁𝙄𝘾𝙄𝘼𝙇 & 𝘾𝙊𝙉𝙁𝙄𝙍𝙈𝙀𝘿

Michuano ya CAF Confederations cup iliyoanzishwa rasmi mwaka 2003 imefutwa rasmi na Shirikisho la soka Barani Afrika kuanzia msimu ujao 2024/25.

Kutakuwa na mashindano mawili.

◉ CAF champions league.
◉ African Football League.

African Football League itajumuisha timu (24) ambazo zimekidhi vigezo kwa kuwa na alama nyingi kwenye Ranks za (CAF).

Michuano ya CAF champions league itaendelea kama kawaida ambapo kila Nchi mwanachama itatoa timu mbili.

1713309799533.jpg
 
Kwa mtazamo wangu hii AFL ndo itakuwa ligi kubwa lakn bingwa wa ligi ndo atashiriki huko na wale wa pili wataenda CAFCL
Kwa hiyo mshimdi wa tatu ndiyo ataitwa Bingwa na kwenda kushiriki Ligi ya Mabingwa?

Sasa hapo Bingwa atakuwa nani?
 
... 🚨 𝙊𝙁𝙁𝙄𝘾𝙄𝘼𝙇 & 𝘾𝙊𝙉𝙁𝙄𝙍𝙈𝙀𝘿

Michuano ya CAF Confederations cup iliyoanzishwa rasmi mwaka 2003 imefutwa rasmi na Shirikisho la soka Barani Afrika kuanzia msimu ujao 2024/25.

Kutakuwa na mashindano mawili.

◉ CAF champions league.
◉ African Football League.

African Football League itajumuisha timu (24) ambazo zimekidhi vigezo kwa kuwa na alama nyingi kwenye Ranks za (CAF).

Michuano ya CAF champions league itaendelea kama kawaida ambapo kila Nchi mwanachama itatoa timu mbili.

View attachment 2965855
Hapa umeeleweka, so mshindi wa tatu na FA sasa hivi hawana Chao tena?
 
Back
Top Bottom