CAF Confederation Cup yafutwa. Msimu ujao kutakuwa na mashindano mawili tu

CAF Confederation Cup yafutwa. Msimu ujao kutakuwa na mashindano mawili tu

Mashindano hayawezi kufanywa kuwa matatu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma wakati kulikuwa na mashindano ya klabu bingwa Afrika, mashindano ya kombe la washindi na mashindano ya kombe la Caf (Mashood Abiola Cup).

Lakini kuleta huu mfumo hauna maana kabisa kumbe yangebakia tu kama yalivyokuwa. Caf ni bure kabisa.
 
Mmmmh mkuu yani haipaswi timu kushiriki mashindano yote mawili ilhali zinatizamwa timu zenye rank ya juu!?
AFL inaanza kabla ya CAFCL.
Rekebisha maelezo mkuu.
Mamelody ndio mshindi wa AFL na sasa yupo nusu fainali CAFCL.
Mwaka huu AFL ilikua anafanyiwa majaribio tu hata timu zilishiriki chache
 
Mmmmh mkuu yani haipaswi timu kushiriki mashindano yote mawili ilhali zinatizamwa timu zenye rank ya juu!?
AFL inaanza kabla ya CAFCL.
Rekebisha maelezo mkuu.
Mamelody ndio mshindi wa AFL na sasa yupo nusu fainali CAFCL.
Wewe ndio hujaelewa mkuu soma kwa utulivu.
 
Kwa upande wangu naona hii haijakaa sawa washiriki wanaoshindania ubingwa wa Afrika inatakiwa wapatikane kulingana na nafasi walizoshika katika ligi zao msimu uliopita kwa mchakato wa kupatikana washiriki AFL maana yake azam akichukua ubingwa hawezi kushiriki mashindano ya kumtafuta bingwa wa jumla katika ligi zote maana kigezo cha point kitamnyima nafasi ya kushiriki, kuna maana gani sasa ya kuwa na ligi kuu? Sijui nani alikuja na huu utaratibu wa kuangalia point za misimu mitano nyuma ni utaratibu wa ovyo yaani kama timu sasa hivi ni mbovu ipewe ushiriki kwa sababu kwenye interval ya miaka 3-5 iliyopita ilikua vizuri., Ridiculous.!
sasa hao si ndo wanaenda CAFCL
 
Aya ngojea tuone ila hayo maelezo sijayaelewa na kama hayaleti mantiki.
Hakuna mkanganyiko wowote wa kimantiki sema kwa maoni yangu naona iyo AFL isingekuwepo tu, sijaona ulazima wowote wa kuleta hayo mashindano
 
Ushauri wangu ni bora mambo yangekuwa hivi

AFL
Caf champions league
Caf Confederation cup

Kwenye hiyo AFL wapambane wale wenye rank kubwa kwenye champions league mfano (waliocheza fainali) mshindi wa kwanza na wa pili na wengineo kama watakavopanga.

Caf champions league iwe ni ya wale walioshika nafasi ya kwanza na ya pili kwenye ligi zao. Kama wote wawili watakuwa kwenye AFL bc aliyeshika nafasi ya kwanza atabaki AFL na wa pili atarudi champions league na watatu nae atashiriki champions ikiwa kama bingwa wa ligi atacheza AFL (rejea hapo juu kwenye AFL)

Caf confederation cup iwe ya walioshika nafasi ya tatu na nne kwenye ligi zao. Ikiwa mshindi wa tatu atakuwa anacheza champions bc nafasi ya nne na tano watacheza confederation.
ubora wa vilabu vya Africa upo chini sana kitendo cha kusema vilabu vilivoshika nafasi ya nne na tatu vicheze michuano ya kimataifa ni aibu tupu hukujifuza tu walichokifanya Namungo kweny Msimu wake wa kwanza kwenye shirikisho makosa yalikua Mengi sana mfano issue ya wachezaji kutaftiea pasport za kusafiria wiki moja kabla ya kusafiri kwenda kucheza mechi ugenini ilikua aibu kubwa sana
 
Hy aibu n kwa huku Bongo, kwan timu za north haziwezi kusafiri.? Nadhani wengn n kupewa Sapoti tuu
 
Back
Top Bottom