CAF hawawezi kukubali Taifa stars kufuzu Afcon

CAF hawawezi kukubali Taifa stars kufuzu Afcon

Mvimba macho njoo ufute huu utahira ulioandika hapa.
 
Ukifa kwa pressure bongo ni uzembe wako wa kutokutumia mitandao ya kijamii. Nimesoma hii thread toka mwanzo sikumuelewa mwandishi anamaanisha nini ila nipofika kwa Engonga nimecheka sana.
 
Mpira ni biashara

Timu letu Bado ni bovu

Stars umeenda Afcon mara mbili mfululizo ila haijawahi kushinda wala kutoa sare

Timu letu kila likienda linapigwa na kututia aibu. Me Mtanganyika ila sitaki timu letu lifuzu
Yaani tumeikosa Ghana, tena tuikose Guinea, iyo Afcon itakuwa kama ndondo cup
Timu letu linapewa hamasa
Likishinda Kuna watu wanajipa hati miliki Bora lifungwe ili wote tunune

Kibiashara Taifa stars haitazamwi kama Guinea
Guinea ina professional wengi wanaocheza Europe

Yaani CAF waipitishe timu lililojaza wachezaji wa KMC, Mashujaa na Dodoma Jiji

Me nasimama na timu Baltasary Engonga, Guinea
Mkuu hii tuloidunga ni Guinea ya Bissau kama sijakosea yako ni Equetorial Guimea
 
Ogopa Mungu na technology, aibu kubwa sana hii, alafu ukute ni mke wa mtu na ameolewa
 
Swali la msingi hivi sisi kufuzu siku hizi ni ubora au kubadilishwa kwa mfumo kunafanya kuwa rahisi kufuzu AFCON? maana zamani ilikuwa team 12 na ilikuwa kazi kupata nafasi halafu wakaja kuongeza 16 na haikuwa rahisi ila baada ya kuongeza team 24 naona kama ukishindwa basi wewe mbovu tu wala haihitaji team kuwa ya ushindani sana, kwa maana team ya kawaida tu inaweza kufuzu siku hizi hata Comoro wapo sana tu huko.
 
Back
Top Bottom