Ubaya Ubwela
JF-Expert Member
- Jul 24, 2024
- 1,353
- 3,060
Inasemekana Shirikisho la Soka Afrika CAF limeufungia uwanja wa Benjamin Mkapa kwa muda kutokana na ubovu wa eneo la kuchezea (pitch). Ripoti inaonyesha pitch mbovu na inazidi kuzorota. Wameitaka TFF kuchagua kiwanja kingine kwajili ya Robo fainali ya Shirikisho ya Simba hapo tarehe 9 April
Huu uwanja toka msimu unaanza hautumiki kwa mechi za ndani walidai kua wanaufanyia marekebisho, hii ncho yetu Siasa nyingi sana,
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeufungia kwa muda Uwanja wa Benjamin Mkapра, Dar es Salaam kutokana na eneo la kuchezea (pitch) kuendelea kupungua ubora wake.
CAF imeelekeza eneo hilo liboreshwe haraka kufikia viwango vinavyotakiwa ili kuepuka Uwanja huo kufungiwa kwa muda mrefu.
Mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF (CAF CC) kati ya Simba na Al Masry ya Misri imepangwa kuchezwa kwenye uwanja huo Aprili 9, 2025.
Ili kuondoa usumbufu, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetakiwa kutuma jina la uwanja mbadala utakaotumiwa na Simba kufikia Machi 14, 2025.
CAF itafanya ukaguzi wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Machi 20, 2025 ili kuona maboresho yaliyofanyika kabla ya kuamua kuuruhusu utumike au kuendelea kuufungia. Mbali ya mechi hizo za CAF CC, Uwanja wa Benjamin Mkapa umepangwa kutumika kwa ajili ya Fanali za CHAN zitakazofanyika Agosti 2025.
Pia soma: Msigwa Atoa Ufafanuzi Taarifa ya CAF Kuufungia Uwanja wa Mkapa, Kuhusu Derby Asema Waulizeni TFF
View attachment 3267578