CAG afichua Serikali ya Magufuli ilivyoisababishia taifa hasara ya Sh 1.7 trilioni mradi wa SGR

Mikataba iliyosainiwa Dec 2021 na July 2022 kwa Lot 3 na 4 inahusikaje na awamu ya 5? Heb tuelezee huo uzalendo uliwezaje kuvuka mipaka mpaka dec 2021 while awamu ya 6 ilianza March 2021.?

Mchakato ulianza toka enzi ya awamu ya mwendazake ambapo bodi kadhaa za wakurugenzi wa TRC walisimamia

Bodi ya Wakurugenzi TRC tarehe 17 February 2023 chini ya mwenyekiti Prof. John Wajanga
Kondoro waliotambulishwa ni Bw. Benjamini Adam Mbimbi, Bw. Kondo Abdalah Kibugula, Bw. Joseph Elias Salema, Bw. Juma Samhando Kijavara na Bw. Peter Mayunga Noni.

Wajumbe waliomaliza muda wao ni Bw. Wolfgang Ephraim Salia, Bi. Consolata Chrisostom Ngimbwa, Bw. Karim Godfrey Mattaka, Bw. Rogatus Hussein Mativila na Bw. Mahamud Mashaka Mabuyu.

Wajumbe wanaoendelea na nafasi zao ni pamoja na Bw. Jabir Bakari na Bi Lilian Ngilangwa. Baadhi ya wajumbe waliomaliza muda wao walipata fursa ya kutoa neno kwa menejimenti ya Shirika na kupongeza jitihada kubwa zilizofanywa kuhakikisha watumishi wanafanya kazi kwa weledi na kuleta tija katika utendaji wa Shirika.

Sources : TRC RELI TV / Mwanzo | TRC
 
JPM alikuwa mwizi sana, nadhani Afrika mashariki na kati ndiye Rais aliyeongoza kwa wizi
 
Naona kila kitu mnataka kumpin nacho JPM...JPM alihusika na kipande cha 1,2 na 5...hivyo vingine vyote vimesainiwa mbele ya awamu ya 6.

Mkataba ya Lot 3 ulisainiwa ikulu Dec 28 2021 miezi 9 tangu JPM afariki, Lot 4 ulisainiwa Ikulu July 2022 zaidi ya mwaka na nusu tangu afariki.
Hapo JPM anahusikaje, au alifufuka akaja kuongoza mchakato?

Huu Uongo mnaousambaza unawasidia nn? Kwann hamtaki kua responsible kwa makosa mnayoyafanya?itafika 2030 bado mtamlaumu JPM kwa ufisadi wa 2029.
Kwa nini andiko kama hili wahusika wa JF wasilipandishe na kuwekwa chini ya mada husika; ili kila anayemaliza kusoma andiko la gazeti, asome chini yake haya aliyoweka mkuu 'Gobole' hapa!
 
Ripoti mpya ya CAG iliyotolewa Aprili 6, 2023, yasema Serikali ya Awamu ya 5 ilivunja sheria ya nchi kwenye utoaji wa kandarasi ya reli

Ilikubali masharti mabovu ya Benki ya StanChart kuwapa kandarasi Waturuki kwa gharama ya juu bila tenda ya wazi ya ushindani

Na Waandishi Wetu

SERIKALI ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli iliingizia taifa hasara ya Dola za Marekani milioni 742.4 (zaidi ya Shilingi trilioni 1.7) kwenye ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR baada ya kukubali masharti mabovu ya mkopo wa benki ya Standard Chartered.

Ripoti Kuu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo 2021/22 iliyotolewa juzi na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilisema kuwa hasara hiyo kwa taifa ilitokana na Serikali ya Magufuli kukubali masharti ya ajabu ya mkopo wa kibiashara wa Dola za Marekani Bilioni 1.46 kutoka kwa Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa SGR uliotolewa mwaka 2020.

Moja ya masharti ya mkopo huo ni kuwa Serikali ivunje Sheria ya Manunuzi ya Umma kwa kutoa kandarasi mbili za ujenzi wa reli ya SGR kwa kampuni ya Kituruki ya Yapi Merkezi Insaat VE Sanayi As bila zabuni ya wazi ya kushindanisha kampuni nyingine.

Serikali ya Magufuli ilikubali masharti hayo ya ajabu kwa kutoa kandarasi kwa Waturuki kinyume na sheria za nchi.

CAG alibaini kuwa gharama za ujenzi wa kipande cha reli ya Makutupora-Tabora (Lot 3) iliongezeka kwa Dola za Marekani milioni 1.3 (zaidi ya Shilingi Bilioni 3) kwa kila kilomita wakati gharama ya ujenzi wa kipande cha reli ya Tabora-Isaka (Lot 4) iliongezeka kwa Dola milioni 1.6 (Shilingi Bilioni 3.74) kwa kila kilomita.

"Shirika la Reli Tanzania (TRC) halikutumia njia ya ununuzi ya ushindani katika ujenzi wa reli ya kisasa kwa kipande cha tatu na cha nne na kusababisha kuongezeka kwa Dola za Kimarekani milioni 1.3 na milioni 1.6 kwa kilomita mtawalia ikilinganishwa na mikataba ya awali,," alisema CAG.

Reli ya Makutupora-Tabora yenye urefu wa kilomita 368 inajengwa kwa gharama ya Dola za Marekani Bilioni 1.9, wakati kipande cha Tabora-Isaka chenye urefu wa kilomita 165, kinajengwa kwa gharama za Dola za Marekani milioni 900.

Maana yake ni kuwa taifa limeingia jumla ya hasara ya Dola za Marekani 742.4 (zaidi ya Shilingi trilioni 1.7) kwenye vipande hivyo viwili vya reli.

"Mapitio yangu ya njia za ununuzi zilizotumika katika ununuzi wa mkandarasi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha 3 na 4 yalibainisha kuwa Benki ya Standard Chartered ambako Serikali ilipata mkopo iliweka masharti kwamba ingekubali jukumu la kuwa Mratibu wa
Kimataifa, na Wakala Kiongozi Aliye na Mamlaka kupanga ufadhili na mkopo kwa Wizara ya Fedha na Mipango (MoFP) tu kwa masharti kwamba kampuni ya Yapi Markezi iteuliwe kama Mkandarasi," alisema CAG kwenye ripoti hiyo.

"Wizara
ya Fedha na Mipango (MOFP) ilikubali mkopo huo kwa masharti yasiyofaa kutoka Benki ya Standard Chartered kupitia barua yenye kumbukumbu namba PST/GEN/2021/01/55."

Wakati barua hiyo inaandikwa, Doto James ndiye aliyekua Katibu Mkuu wa Hazina (PST) kwenye Wizara ya Fedha na Mipango.

CAG amebaini zaidi kuwa TRC iliamua kuchagua njia ya kutoa zabuni kwa njia
mzabuni mmoja licha ya ushauri uliotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Bodi ya Zabuni, ambayo iliishia kuigharimu serikali fedha zaidi, ambayo ingeweza kuepukwa.

"Ni maoni yangu kwamba, hakuna mfadhili anayeweza kuitaka Serikali ya Tanzania kumpa mkataba mkandarasi pasipo kuwa na uwazi, ushindani, usawa na haki kwa wakandarasi wote wenye sifa na wanaostahili katika mchakato wa ununuzi," alisema CAG.

Ripoti ya CAG ilibaini kuwa baada ya Serikali ya Magufuli kukubali masharti yasiyofaa ya kuwapa kandarasi ya Lot 3 na Lot 4 kwa Yapi Merkezi bila tenda ya wazi ya ushindani, Waturuki hao wakaongeza gharama ya ujenzi kuliko kawaida na kuliingizia taifa hasara kubwa.

Wakati vipande vingine vya reli ya SGR ya Tanzania vinajengwa kwa gharama ya kati ya Dola za Marekani milioni 3.9 na Dola la Marekani milioni 4.6 kwa kila kilomita, kipande cha Lot 3 walichopewa Waturuki bila ya tenda ya wazi wanakijenga kwa gharama ya juu ya Dola milioni 5.2 kwa kila kilomita.

Vile vile, kipande cha Lot 4 walichopewa Waturuki hao hao bila ya tenda ya wazi (single source) wanakijenga kwa gharama kubwa mno ya Dola Marekani milioni 5.5 kwa kila kilomita.

"Kulingana na tofauti hiyo, hapakuwa na faida ya kiuchumi kwa TRC kwa kutoa kandarasi kupitia njia ya chanzo kimoja kwa M/S Yapi Merkezi. Hii ni kwa sababu gharama awali za miradi mingine zilikuwa chini ikilinganishwa na mkataba aliopewa mkandarasi wa kipande cha 3 na 4," alisema CAG.

"Zaidi ya hayo, niligundua kuwa mawanda ya kazi kwa kipande cha 3 na 4 ya mradi ulikuwa mdogo na ulikuwa na miundombinu michache kuliko ile ya kipande cha 1, 2, na 5, na miundo mikuu zaidi."

CAG amependekeza kuwa menejimenti ya TRC iweke kipaumbele katika matumizi ya mbinu shindani ya ununuzi katika shughuli za manunuzi za siku zijazo ili kuepuka upotevu wa fedha za walipa
kodi.

Chanzo: Jambo TV
Inabidi majaliwa na mpango pamoja na Samia wapishe maana ni sehemu ya serikali iliyosababisha hasara
 
Mzalendo na Rais wa wanyonge, kwa mlango wa nyuma alikuwa anatunyonga huku tukishangilia. Serikali iitishe wito wa kimataifa haya matrilinloni yarejeshwe kama vile ilivyofanywa kwa Sani AbachaView attachment 2582428
Mnataka kuamija ajenda ee hapa hakuna Cha Magufuli Wala nini mliorithi ndo mtuambie. Mbona mazuri yake mnasema yenu hata mabaya yachukueni
 
Mwakani tunafumua ununuzi wa ndege moja baada ya nyingine, na mlikoficha Hela za kickback
 
Mama na Kikundi chake ni Majizi, mmetia hasara Nchi hii, Ndani ya miaka miwili tu.

sasa mnatumia nguvu nyiiiingi sana kutaka kumfunika Wizi wa Mama na Kikundi chake, kwakutumia Mgongo wa JPM.
Kwa hiyo wewe ulikuwa kikundi kipi usichopenda kisemwe kilivyopiga, kikundi cha JPM au cha mama. Prof. Asad alikiambia cha JPM kilipiga 1.5T, na huyu CAG ameibua 1.7T.

Wewe unapendezwa na kipi cha kwako, kile au hiki?😎
 
Mzalendo na Rais wa wanyonge, kwa mlango wa nyuma alikuwa anatunyonga huku tukishangilia. Serikali iitishe wito wa kimataifa haya matrilinloni yarejeshwe kama vile ilivyofanywa kwa Sani AbachaView attachment 2582428
Daah! Huyu mtu huyu sijui tukalifanye nn kaburi lake. Anyway! Ndiyo maana mwaka huu kumbukizi yake tumeidogosha sana
 
Ripoti mpya ya CAG iliyotolewa Aprili 6, 2023, yasema Serikali ya Awamu ya 5 ilivunja sheria ya nchi kwenye utoaji wa kandarasi ya reli

Ilikubali masharti mabovu ya Benki ya StanChart kuwapa kandarasi Waturuki kwa gharama ya juu bila tenda ya wazi ya ushindani

Na Waandishi Wetu

SERIKALI ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli iliingizia taifa hasara ya Dola za Marekani milioni 742.4 (zaidi ya Shilingi trilioni 1.7) kwenye ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR baada ya kukubali masharti mabovu ya mkopo wa benki ya Standard Chartered.

Ripoti Kuu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo 2021/22 iliyotolewa juzi na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilisema kuwa hasara hiyo kwa taifa ilitokana na Serikali ya Magufuli kukubali masharti ya ajabu ya mkopo wa kibiashara wa Dola za Marekani Bilioni 1.46 kutoka kwa Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa SGR uliotolewa mwaka 2020.

Moja ya masharti ya mkopo huo ni kuwa Serikali ivunje Sheria ya Manunuzi ya Umma kwa kutoa kandarasi mbili za ujenzi wa reli ya SGR kwa kampuni ya Kituruki ya Yapi Merkezi Insaat VE Sanayi As bila zabuni ya wazi ya kushindanisha kampuni nyingine.

Serikali ya Magufuli ilikubali masharti hayo ya ajabu kwa kutoa kandarasi kwa Waturuki kinyume na sheria za nchi.

CAG alibaini kuwa gharama za ujenzi wa kipande cha reli ya Makutupora-Tabora (Lot 3) iliongezeka kwa Dola za Marekani milioni 1.3 (zaidi ya Shilingi Bilioni 3) kwa kila kilomita wakati gharama ya ujenzi wa kipande cha reli ya Tabora-Isaka (Lot 4) iliongezeka kwa Dola milioni 1.6 (Shilingi Bilioni 3.74) kwa kila kilomita.

"Shirika la Reli Tanzania (TRC) halikutumia njia ya ununuzi ya ushindani katika ujenzi wa reli ya kisasa kwa kipande cha tatu na cha nne na kusababisha kuongezeka kwa Dola za Kimarekani milioni 1.3 na milioni 1.6 kwa kilomita mtawalia ikilinganishwa na mikataba ya awali,," alisema CAG.

Reli ya Makutupora-Tabora yenye urefu wa kilomita 368 inajengwa kwa gharama ya Dola za Marekani Bilioni 1.9, wakati kipande cha Tabora-Isaka chenye urefu wa kilomita 165, kinajengwa kwa gharama za Dola za Marekani milioni 900.

Maana yake ni kuwa taifa limeingia jumla ya hasara ya Dola za Marekani 742.4 (zaidi ya Shilingi trilioni 1.7) kwenye vipande hivyo viwili vya reli.

"Mapitio yangu ya njia za ununuzi zilizotumika katika ununuzi wa mkandarasi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha 3 na 4 yalibainisha kuwa Benki ya Standard Chartered ambako Serikali ilipata mkopo iliweka masharti kwamba ingekubali jukumu la kuwa Mratibu wa
Kimataifa, na Wakala Kiongozi Aliye na Mamlaka kupanga ufadhili na mkopo kwa Wizara ya Fedha na Mipango (MoFP) tu kwa masharti kwamba kampuni ya Yapi Markezi iteuliwe kama Mkandarasi," alisema CAG kwenye ripoti hiyo.

"Wizara
ya Fedha na Mipango (MOFP) ilikubali mkopo huo kwa masharti yasiyofaa kutoka Benki ya Standard Chartered kupitia barua yenye kumbukumbu namba PST/GEN/2021/01/55."

Wakati barua hiyo inaandikwa, Doto James ndiye aliyekua Katibu Mkuu wa Hazina (PST) kwenye Wizara ya Fedha na Mipango.

CAG amebaini zaidi kuwa TRC iliamua kuchagua njia ya kutoa zabuni kwa njia
mzabuni mmoja licha ya ushauri uliotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Bodi ya Zabuni, ambayo iliishia kuigharimu serikali fedha zaidi, ambayo ingeweza kuepukwa.

"Ni maoni yangu kwamba, hakuna mfadhili anayeweza kuitaka Serikali ya Tanzania kumpa mkataba mkandarasi pasipo kuwa na uwazi, ushindani, usawa na haki kwa wakandarasi wote wenye sifa na wanaostahili katika mchakato wa ununuzi," alisema CAG.

Ripoti ya CAG ilibaini kuwa baada ya Serikali ya Magufuli kukubali masharti yasiyofaa ya kuwapa kandarasi ya Lot 3 na Lot 4 kwa Yapi Merkezi bila tenda ya wazi ya ushindani, Waturuki hao wakaongeza gharama ya ujenzi kuliko kawaida na kuliingizia taifa hasara kubwa.

Wakati vipande vingine vya reli ya SGR ya Tanzania vinajengwa kwa gharama ya kati ya Dola za Marekani milioni 3.9 na Dola la Marekani milioni 4.6 kwa kila kilomita, kipande cha Lot 3 walichopewa Waturuki bila ya tenda ya wazi wanakijenga kwa gharama ya juu ya Dola milioni 5.2 kwa kila kilomita.

Vile vile, kipande cha Lot 4 walichopewa Waturuki hao hao bila ya tenda ya wazi (single source) wanakijenga kwa gharama kubwa mno ya Dola Marekani milioni 5.5 kwa kila kilomita.

"Kulingana na tofauti hiyo, hapakuwa na faida ya kiuchumi kwa TRC kwa kutoa kandarasi kupitia njia ya chanzo kimoja kwa M/S Yapi Merkezi. Hii ni kwa sababu gharama awali za miradi mingine zilikuwa chini ikilinganishwa na mkataba aliopewa mkandarasi wa kipande cha 3 na 4," alisema CAG.

"Zaidi ya hayo, niligundua kuwa mawanda ya kazi kwa kipande cha 3 na 4 ya mradi ulikuwa mdogo na ulikuwa na miundombinu michache kuliko ile ya kipande cha 1, 2, na 5, na miundo mikuu zaidi."

CAG amependekeza kuwa menejimenti ya TRC iweke kipaumbele katika matumizi ya mbinu shindani ya ununuzi katika shughuli za manunuzi za siku zijazo ili kuepuka upotevu wa fedha za walipa
kodi.

Chanzo: Jambo TV

Makamu wake wa Rais bado yupo so anaweza kuwa na majibu
 
Mmetumwa na majizi original kutupigia kelele Magufuli alikuwa fisadi ili yenyewe yaendelee kupiga bila kelele yaani mafisadi yamemfanya Magufuli kuwa kichaka cha kuficha ufisadi wao wanaoufanya sasahivi na nyie wanaolipwa kuja kutuanzia uzi wa kinafiki
 
Kwa nn report ya CAG haikuongelea hayo mambo Mwaka 2021 ,2022 ,?Mwaka wa pili mama anasherekea Urais ndio mnatuletea mambo ya Magufuli?Ambaye hayupo zaid ya miaka miwili?Acheni ujinga na upumbufu.Watanzania tuna akili na tunaelewa.
 
Kama kipande cha tatu ,nne na sita vilisainiwa na JPM mm ni mbwaaaaaaaaaa.
 
Magufuli alisaini 1,2 na 5 na hiyo 3 na 4 alisaini Samia
 
Back
Top Bottom