CAG afichua Serikali ya Magufuli ilivyoisababishia taifa hasara ya Sh 1.7 trilioni mradi wa SGR

Kwa nn report ya CAG haikuongelea hayo mambo Mwaka 2021 ,2022 ,?Mwaka wa pili mama anasherekea Urais ndio mnatuletea mambo ya Magufuli?Ambaye hayupo zaid ya miaka miwili?Acheni ujinga na upumbufu.Watanzania tuna akili na tunaelewa.
Mbona kama lot 3 na 4 aliyesaini ni Samia.
 
Ripoti mpya ya CAG iliyotolewa Aprili 6, 2023, yasema Serikali ya Awamu ya 5 ilivunja sheria ya nchi kwenye utoaji wa kandarasi ya reli

Ilikubali masharti mabovu ya Benki ya StanChart kuwapa kandarasi Waturuki kwa gharama ya juu bila tenda ya wazi ya ushindani

Na Waandishi Wetu

SERIKALI ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli iliingizia taifa hasara ya Dola za Marekani milioni 742.4 (zaidi ya Shilingi trilioni 1.7) kwenye ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR baada ya kukubali masharti mabovu ya mkopo wa benki ya Standard Chartered.

Ripoti Kuu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo 2021/22 iliyotolewa juzi na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilisema kuwa hasara hiyo kwa taifa ilitokana na Serikali ya Magufuli kukubali masharti ya ajabu ya mkopo wa kibiashara wa Dola za Marekani Bilioni 1.46 kutoka kwa Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa SGR uliotolewa mwaka 2020.

Moja ya masharti ya mkopo huo ni kuwa Serikali ivunje Sheria ya Manunuzi ya Umma kwa kutoa kandarasi mbili za ujenzi wa reli ya SGR kwa kampuni ya Kituruki ya Yapi Merkezi Insaat VE Sanayi As bila zabuni ya wazi ya kushindanisha kampuni nyingine.

Serikali ya Magufuli ilikubali masharti hayo ya ajabu kwa kutoa kandarasi kwa Waturuki kinyume na sheria za nchi.

CAG alibaini kuwa gharama za ujenzi wa kipande cha reli ya Makutupora-Tabora (Lot 3) iliongezeka kwa Dola za Marekani milioni 1.3 (zaidi ya Shilingi Bilioni 3) kwa kila kilomita wakati gharama ya ujenzi wa kipande cha reli ya Tabora-Isaka (Lot 4) iliongezeka kwa Dola milioni 1.6 (Shilingi Bilioni 3.74) kwa kila kilomita.

"Shirika la Reli Tanzania (TRC) halikutumia njia ya ununuzi ya ushindani katika ujenzi wa reli ya kisasa kwa kipande cha tatu na cha nne na kusababisha kuongezeka kwa Dola za Kimarekani milioni 1.3 na milioni 1.6 kwa kilomita mtawalia ikilinganishwa na mikataba ya awali,," alisema CAG.

Reli ya Makutupora-Tabora yenye urefu wa kilomita 368 inajengwa kwa gharama ya Dola za Marekani Bilioni 1.9, wakati kipande cha Tabora-Isaka chenye urefu wa kilomita 165, kinajengwa kwa gharama za Dola za Marekani milioni 900.

Maana yake ni kuwa taifa limeingia jumla ya hasara ya Dola za Marekani 742.4 (zaidi ya Shilingi trilioni 1.7) kwenye vipande hivyo viwili vya reli.

"Mapitio yangu ya njia za ununuzi zilizotumika katika ununuzi wa mkandarasi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha 3 na 4 yalibainisha kuwa Benki ya Standard Chartered ambako Serikali ilipata mkopo iliweka masharti kwamba ingekubali jukumu la kuwa Mratibu wa
Kimataifa, na Wakala Kiongozi Aliye na Mamlaka kupanga ufadhili na mkopo kwa Wizara ya Fedha na Mipango (MoFP) tu kwa masharti kwamba kampuni ya Yapi Markezi iteuliwe kama Mkandarasi," alisema CAG kwenye ripoti hiyo.

"Wizara
ya Fedha na Mipango (MOFP) ilikubali mkopo huo kwa masharti yasiyofaa kutoka Benki ya Standard Chartered kupitia barua yenye kumbukumbu namba PST/GEN/2021/01/55."

Wakati barua hiyo inaandikwa, Doto James ndiye aliyekua Katibu Mkuu wa Hazina (PST) kwenye Wizara ya Fedha na Mipango.

CAG amebaini zaidi kuwa TRC iliamua kuchagua njia ya kutoa zabuni kwa njia
mzabuni mmoja licha ya ushauri uliotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Bodi ya Zabuni, ambayo iliishia kuigharimu serikali fedha zaidi, ambayo ingeweza kuepukwa.

"Ni maoni yangu kwamba, hakuna mfadhili anayeweza kuitaka Serikali ya Tanzania kumpa mkataba mkandarasi pasipo kuwa na uwazi, ushindani, usawa na haki kwa wakandarasi wote wenye sifa na wanaostahili katika mchakato wa ununuzi," alisema CAG.

Ripoti ya CAG ilibaini kuwa baada ya Serikali ya Magufuli kukubali masharti yasiyofaa ya kuwapa kandarasi ya Lot 3 na Lot 4 kwa Yapi Merkezi bila tenda ya wazi ya ushindani, Waturuki hao wakaongeza gharama ya ujenzi kuliko kawaida na kuliingizia taifa hasara kubwa.

Wakati vipande vingine vya reli ya SGR ya Tanzania vinajengwa kwa gharama ya kati ya Dola za Marekani milioni 3.9 na Dola la Marekani milioni 4.6 kwa kila kilomita, kipande cha Lot 3 walichopewa Waturuki bila ya tenda ya wazi wanakijenga kwa gharama ya juu ya Dola milioni 5.2 kwa kila kilomita.

Vile vile, kipande cha Lot 4 walichopewa Waturuki hao hao bila ya tenda ya wazi (single source) wanakijenga kwa gharama kubwa mno ya Dola Marekani milioni 5.5 kwa kila kilomita.

"Kulingana na tofauti hiyo, hapakuwa na faida ya kiuchumi kwa TRC kwa kutoa kandarasi kupitia njia ya chanzo kimoja kwa M/S Yapi Merkezi. Hii ni kwa sababu gharama awali za miradi mingine zilikuwa chini ikilinganishwa na mkataba aliopewa mkandarasi wa kipande cha 3 na 4," alisema CAG.

"Zaidi ya hayo, niligundua kuwa mawanda ya kazi kwa kipande cha 3 na 4 ya mradi ulikuwa mdogo na ulikuwa na miundombinu michache kuliko ile ya kipande cha 1, 2, na 5, na miundo mikuu zaidi."

CAG amependekeza kuwa menejimenti ya TRC iweke kipaumbele katika matumizi ya mbinu shindani ya ununuzi katika shughuli za manunuzi za siku zijazo ili kuepuka upotevu wa fedha za walipa
kodi.

Chanzo: Jambo TV
Huyo aliyekutuma na wewe wote hamna Akili Kwa Sababu kwanini upotoshe?lot 3 na 4 aliyesaini ni Samia.
 
Ndio nakwambia anayeweka standaiza wapi single source ifanyike ni ppra sio taasisi inayotaka kufanya ununuzi.

Single source pia haipo Kwa Ajili ya kutia hasara serikali Bali Kwa mazingira maalumu..

Mwisho yaani unapangiwa contractor na creditor Kwa Ajili ya nini hasa? Haya ndio madhara ya kudanganya ooh tunajenga Kwa pesa zetu matokeo yake ni commercial loans Zenye masharti ya kipumbavu kama haya na Jiwe hakuwa na options zaidi ya kunywea.
Yaani nukta hii nilikuwa najiuliza sana. Kila kukicha nasikia kauli ya 'TUNAJENGA KWA PESA ZETU SISI NI MATAJIRI' nashangaza hapa hii Bank ya standard chartered na mkopo inakujaje hapa ?
 
Hasara ya Trillion 1.7 ! Astaghfirullah
 
Sawa lakini hasara ambayo ameliletea taifa lazima zisemwe kwani ni mzigo wa kizazi cha leo na cha kesho!!kama ambavyo sifa zake zitakavyotangazwa kwa yale mazuri aliyofanya(kama yapo lakini)
Aliyesaini lot 3 na 4 ni Magufuli?
download.jpg
 
Naona kila kitu mnataka kumpin nacho JPM...JPM alihusika na kipande cha 1,2 na 5...hivyo vingine vyote vimesainiwa mbele ya awamu ya 6.

Mkataba ya Lot 3 ulisainiwa ikulu Dec 28 2021 miezi 9 tangu JPM afariki, Lot 4 ulisainiwa Ikulu July 2022 zaidi ya mwaka na nusu tangu afariki.
Hapo JPM anahusikaje, au alifufuka akaja kuongoza mchakato?

Huu Uongo mnaousambaza unawasidia nn? Kwann hamtaki kua responsible kwa makosa mnayoyafanya?itafika 2030 bado mtamlaumu JPM kwa ufisadi wa 2029.

Aliyesaini lot 3 na 4 ni Magufuli?View attachment 2582646
Awamu ya kwanza: Dar es salaam – Morogoro (Km 300). Ujenzi wa reli ya kisasa kwa awamu ya kwanza ulizinduliwa na Rais wa awamu ya tano. Dr John Pombe Magufuli siku ya tarehe 12, april 2017. Na kwa sasa ujenzi bado unaendelea chini ya mkandarasi YAPI MERKEZI kutoka Uturuki akishirikiana MOTA ENGIL AFRICA kutoka Ureno.

Awamu ya pili: Morogoro - Makutupora ( Km 442). Ujenzi wa mradi ulizinduliwa na Rais wa awamu ya tano. Dr John Pombe Magufuli siku ya tarehe 14, machi 2018. Na kwa sasa hatua za awali za ujenzi zimeanza chini ya mkandarasi YAPI MERKAZI.

Awamu ya 3, 4, na 5: Awamu hizi, ziko katika hatua mbalimbali za manunuzi.
Mkataba mkuu ulishasainiwa wote na JPM,hizo wanazosaini sasa ni kwa lot husika ili pesa iliyoishakubaliwa ianze kutoka hazina,kulingana na kazi inavyoendelea(raised certificates)
 
Ripoti mpya ya CAG iliyotolewa Aprili 6, 2023, yasema Serikali ya Awamu ya 5 ilivunja sheria ya nchi kwenye utoaji wa kandarasi ya reli

Ilikubali masharti mabovu ya Benki ya StanChart kuwapa kandarasi Waturuki kwa gharama ya juu bila tenda ya wazi ya ushindani

Na Waandishi Wetu

SERIKALI ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli iliingizia taifa hasara ya Dola za Marekani milioni 742.4 (zaidi ya Shilingi trilioni 1.7) kwenye ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR baada ya kukubali masharti mabovu ya mkopo wa benki ya Standard Chartered.

Ripoti Kuu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo 2021/22 iliyotolewa juzi na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilisema kuwa hasara hiyo kwa taifa ilitokana na Serikali ya Magufuli kukubali masharti ya ajabu ya mkopo wa kibiashara wa Dola za Marekani Bilioni 1.46 kutoka kwa Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa SGR uliotolewa mwaka 2020.

Moja ya masharti ya mkopo huo ni kuwa Serikali ivunje Sheria ya Manunuzi ya Umma kwa kutoa kandarasi mbili za ujenzi wa reli ya SGR kwa kampuni ya Kituruki ya Yapi Merkezi Insaat VE Sanayi As bila zabuni ya wazi ya kushindanisha kampuni nyingine.

Serikali ya Magufuli ilikubali masharti hayo ya ajabu kwa kutoa kandarasi kwa Waturuki kinyume na sheria za nchi.

CAG alibaini kuwa gharama za ujenzi wa kipande cha reli ya Makutupora-Tabora (Lot 3) iliongezeka kwa Dola za Marekani milioni 1.3 (zaidi ya Shilingi Bilioni 3) kwa kila kilomita wakati gharama ya ujenzi wa kipande cha reli ya Tabora-Isaka (Lot 4) iliongezeka kwa Dola milioni 1.6 (Shilingi Bilioni 3.74) kwa kila kilomita.

"Shirika la Reli Tanzania (TRC) halikutumia njia ya ununuzi ya ushindani katika ujenzi wa reli ya kisasa kwa kipande cha tatu na cha nne na kusababisha kuongezeka kwa Dola za Kimarekani milioni 1.3 na milioni 1.6 kwa kilomita mtawalia ikilinganishwa na mikataba ya awali,," alisema CAG.

Reli ya Makutupora-Tabora yenye urefu wa kilomita 368 inajengwa kwa gharama ya Dola za Marekani Bilioni 1.9, wakati kipande cha Tabora-Isaka chenye urefu wa kilomita 165, kinajengwa kwa gharama za Dola za Marekani milioni 900.

Maana yake ni kuwa taifa limeingia jumla ya hasara ya Dola za Marekani 742.4 (zaidi ya Shilingi trilioni 1.7) kwenye vipande hivyo viwili vya reli.

"Mapitio yangu ya njia za ununuzi zilizotumika katika ununuzi wa mkandarasi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha 3 na 4 yalibainisha kuwa Benki ya Standard Chartered ambako Serikali ilipata mkopo iliweka masharti kwamba ingekubali jukumu la kuwa Mratibu wa
Kimataifa, na Wakala Kiongozi Aliye na Mamlaka kupanga ufadhili na mkopo kwa Wizara ya Fedha na Mipango (MoFP) tu kwa masharti kwamba kampuni ya Yapi Markezi iteuliwe kama Mkandarasi," alisema CAG kwenye ripoti hiyo.

"Wizara
ya Fedha na Mipango (MOFP) ilikubali mkopo huo kwa masharti yasiyofaa kutoka Benki ya Standard Chartered kupitia barua yenye kumbukumbu namba PST/GEN/2021/01/55."

Wakati barua hiyo inaandikwa, Doto James ndiye aliyekua Katibu Mkuu wa Hazina (PST) kwenye Wizara ya Fedha na Mipango.

CAG amebaini zaidi kuwa TRC iliamua kuchagua njia ya kutoa zabuni kwa njia
mzabuni mmoja licha ya ushauri uliotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Bodi ya Zabuni, ambayo iliishia kuigharimu serikali fedha zaidi, ambayo ingeweza kuepukwa.

"Ni maoni yangu kwamba, hakuna mfadhili anayeweza kuitaka Serikali ya Tanzania kumpa mkataba mkandarasi pasipo kuwa na uwazi, ushindani, usawa na haki kwa wakandarasi wote wenye sifa na wanaostahili katika mchakato wa ununuzi," alisema CAG.

Ripoti ya CAG ilibaini kuwa baada ya Serikali ya Magufuli kukubali masharti yasiyofaa ya kuwapa kandarasi ya Lot 3 na Lot 4 kwa Yapi Merkezi bila tenda ya wazi ya ushindani, Waturuki hao wakaongeza gharama ya ujenzi kuliko kawaida na kuliingizia taifa hasara kubwa.

Wakati vipande vingine vya reli ya SGR ya Tanzania vinajengwa kwa gharama ya kati ya Dola za Marekani milioni 3.9 na Dola la Marekani milioni 4.6 kwa kila kilomita, kipande cha Lot 3 walichopewa Waturuki bila ya tenda ya wazi wanakijenga kwa gharama ya juu ya Dola milioni 5.2 kwa kila kilomita.

Vile vile, kipande cha Lot 4 walichopewa Waturuki hao hao bila ya tenda ya wazi (single source) wanakijenga kwa gharama kubwa mno ya Dola Marekani milioni 5.5 kwa kila kilomita.

"Kulingana na tofauti hiyo, hapakuwa na faida ya kiuchumi kwa TRC kwa kutoa kandarasi kupitia njia ya chanzo kimoja kwa M/S Yapi Merkezi. Hii ni kwa sababu gharama awali za miradi mingine zilikuwa chini ikilinganishwa na mkataba aliopewa mkandarasi wa kipande cha 3 na 4," alisema CAG.

"Zaidi ya hayo, niligundua kuwa mawanda ya kazi kwa kipande cha 3 na 4 ya mradi ulikuwa mdogo na ulikuwa na miundombinu michache kuliko ile ya kipande cha 1, 2, na 5, na miundo mikuu zaidi."

CAG amependekeza kuwa menejimenti ya TRC iweke kipaumbele katika matumizi ya mbinu shindani ya ununuzi katika shughuli za manunuzi za siku zijazo ili kuepuka upotevu wa fedha za walipa
kodi.

Chanzo: Jambo TV
Waliosani mkataba lot ya 3 na 4 ni hawa hapa bado wapo hai wawajibishweView attachment 2582660
images%20(8).jpg
 
Awamu ya kwanza: Dar es salaam – Morogoro (Km 300). Ujenzi wa reli ya kisasa kwa awamu ya kwanza ulizinduliwa na Rais wa awamu ya tano. Dr John Pombe Magufuli siku ya tarehe 12, april 2017. Na kwa sasa ujenzi bado unaendelea chini ya mkandarasi YAPI MERKEZI kutoka Uturuki akishirikiana MOTA ENGIL AFRICA kutoka Ureno.

Awamu ya pili: Morogoro - Makutupora ( Km 442). Ujenzi wa mradi ulizinduliwa na Rais wa awamu ya tano. Dr John Pombe Magufuli siku ya tarehe 14, machi 2018. Na kwa sasa hatua za awali za ujenzi zimeanza chini ya mkandarasi YAPI MERKAZI.

Awamu ya 3, 4, na 5: Awamu hizi, ziko katika hatua mbalimbali za manunuzi.
Mkataba mkuu ulishasainiwa wote na JPM,hizo wanazosaini sasa ni kwa lot husika ili pesa iliyoishakubaliwa ianze kutoka hazina,kulingana na kazi inavyoendelea(raised certificates)
Kwaio awamu hii kila certificate ikiwa raised mnaenda Ikulu kusainiana?kuna wakati muwe mnaficha ujinga wenu...you are as dumb as f**k aisee...km hujui kitu ni bora kukaa kimya kuliko kujidhalilisha...
 
Umeshajibiwa na wenye akili
 
Kwaio awamu hii kila certificate ikiwa raised mnaenda Ikulu kusainiana?kuna wakati muwe mnaficha ujinga wenu...you are as dumb as f**k aisee...km hujui kitu ni bora kukaa kimya kuliko kujidhalilisha...
Daaaa!! pathetic!!kumbe huna ufahamu wowote wa jinsi wakandarasi wanavyolipwa?!!
Baada ya hoja yako ya kuwa awamu ya tano hawahusiki na lot hiyo kuipiga chini,ndio umedandia tena treni kwa mbele?!kwanza ungekuwa unajua anayepitisha hizo certificates usingeuliza ushuzi huuu!!!shame on u,kama una mpenda sana mlishaambiwa mmfuate wapi(MUNGU FUNDI)
 
Shame on you kama hawasaini mkataba huwa wanaoenda kufanya nini ikulu? Na nakumbuka Samia suluhu mwenyewe alisema walitangaza tenda.shem on you Kwa kuongea uongo hadharani.
 
huyo unayemuona ana akili kwako sio lazima na mimi nimuone hivyo(kulingana na uelewa wako anaweza kuwa genius kwako,lakini kwangu akawa pimbi tu)
Huoni lot 1,2 na 5 zilizosainiwa na serikali ya Magufuli ilivyokuwa clean?
 
Aliyesaini lot 3 na 4 ni mama yenu acheni upotoshaji.huyo aliyewatuma wote hamna Akili Kwa huu upotoshaji.
Hapa sio fb ambako watu hawana data!mchakato wa manunuzi wa vifaa vya lot 3,4,5 ulishaanza toka awamu ya tano.Hapa nani hana akili sasa??
 
Daaaa!! pathetic!!kumbe huna ufahamu wowote wa jinsi wakandarasi wanavyolipwa?!!
Baada ya hoja yako ya kuwa awamu ya tano hawahusiki na lot hiyo kuipiga chini,ndio umedandia tena treni kwa mbele?!kwanza ungekuwa unajua anayepitisha hizo certificates usingeuliza ushuzi huuu!!!shame on u,kama una mpenda sana mlishaambiwa mmfuate wapi(MUNGU FUNDI)
una utoto mwing sana hata reply zako zinaonesha kbs
 
Back
Top Bottom