CAG afichua Serikali ya Magufuli ilivyoisababishia taifa hasara ya Sh 1.7 trilioni mradi wa SGR

Ripoti mpya ya CAG iliyotolewa Aprili 6, 2023, yasema Serikali ya Awamu ya 5 ilivunja sheria ya nchi kwenye utoaji wa kandarasi ya reli

Ilikubali masharti mabovu ya Benki ya StanChart kuwapa kandarasi Waturuki kwa gharama ya juu bila tenda ya wazi ya ushindani

Na Waandishi Wetu

SERIKALI ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli iliingizia taifa hasara ya Dola za Marekani milioni 742.4 (zaidi ya Shilingi trilioni 1.7) kwenye ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR baada ya kukubali masharti mabovu ya mkopo wa benki ya Standard Chartered.

Ripoti Kuu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo 2021/22 iliyotolewa juzi na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilisema kuwa hasara hiyo kwa taifa ilitokana na Serikali ya Magufuli kukubali masharti ya ajabu ya mkopo wa kibiashara wa Dola za Marekani Bilioni 1.46 kutoka kwa Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa SGR uliotolewa mwaka 2020.

Moja ya masharti ya mkopo huo ni kuwa Serikali ivunje Sheria ya Manunuzi ya Umma kwa kutoa kandarasi mbili za ujenzi wa reli ya SGR kwa kampuni ya Kituruki ya Yapi Merkezi Insaat VE Sanayi As bila zabuni ya wazi ya kushindanisha kampuni nyingine.

Serikali ya Magufuli ilikubali masharti hayo ya ajabu kwa kutoa kandarasi kwa Waturuki kinyume na sheria za nchi.

CAG alibaini kuwa gharama za ujenzi wa kipande cha reli ya Makutupora-Tabora (Lot 3) iliongezeka kwa Dola za Marekani milioni 1.3 (zaidi ya Shilingi Bilioni 3) kwa kila kilomita wakati gharama ya ujenzi wa kipande cha reli ya Tabora-Isaka (Lot 4) iliongezeka kwa Dola milioni 1.6 (Shilingi Bilioni 3.74) kwa kila kilomita.

"Shirika la Reli Tanzania (TRC) halikutumia njia ya ununuzi ya ushindani katika ujenzi wa reli ya kisasa kwa kipande cha tatu na cha nne na kusababisha kuongezeka kwa Dola za Kimarekani milioni 1.3 na milioni 1.6 kwa kilomita mtawalia ikilinganishwa na mikataba ya awali,," alisema CAG.

Reli ya Makutupora-Tabora yenye urefu wa kilomita 368 inajengwa kwa gharama ya Dola za Marekani Bilioni 1.9, wakati kipande cha Tabora-Isaka chenye urefu wa kilomita 165, kinajengwa kwa gharama za Dola za Marekani milioni 900.

Maana yake ni kuwa taifa limeingia jumla ya hasara ya Dola za Marekani 742.4 (zaidi ya Shilingi trilioni 1.7) kwenye vipande hivyo viwili vya reli.

"Mapitio yangu ya njia za ununuzi zilizotumika katika ununuzi wa mkandarasi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha 3 na 4 yalibainisha kuwa Benki ya Standard Chartered ambako Serikali ilipata mkopo iliweka masharti kwamba ingekubali jukumu la kuwa Mratibu wa
Kimataifa, na Wakala Kiongozi Aliye na Mamlaka kupanga ufadhili na mkopo kwa Wizara ya Fedha na Mipango (MoFP) tu kwa masharti kwamba kampuni ya Yapi Markezi iteuliwe kama Mkandarasi," alisema CAG kwenye ripoti hiyo.

"Wizara
ya Fedha na Mipango (MOFP) ilikubali mkopo huo kwa masharti yasiyofaa kutoka Benki ya Standard Chartered kupitia barua yenye kumbukumbu namba PST/GEN/2021/01/55."

Wakati barua hiyo inaandikwa, Doto James ndiye aliyekua Katibu Mkuu wa Hazina (PST) kwenye Wizara ya Fedha na Mipango.

CAG amebaini zaidi kuwa TRC iliamua kuchagua njia ya kutoa zabuni kwa njia
mzabuni mmoja licha ya ushauri uliotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Bodi ya Zabuni, ambayo iliishia kuigharimu serikali fedha zaidi, ambayo ingeweza kuepukwa.

"Ni maoni yangu kwamba, hakuna mfadhili anayeweza kuitaka Serikali ya Tanzania kumpa mkataba mkandarasi pasipo kuwa na uwazi, ushindani, usawa na haki kwa wakandarasi wote wenye sifa na wanaostahili katika mchakato wa ununuzi," alisema CAG.

Ripoti ya CAG ilibaini kuwa baada ya Serikali ya Magufuli kukubali masharti yasiyofaa ya kuwapa kandarasi ya Lot 3 na Lot 4 kwa Yapi Merkezi bila tenda ya wazi ya ushindani, Waturuki hao wakaongeza gharama ya ujenzi kuliko kawaida na kuliingizia taifa hasara kubwa.

Wakati vipande vingine vya reli ya SGR ya Tanzania vinajengwa kwa gharama ya kati ya Dola za Marekani milioni 3.9 na Dola la Marekani milioni 4.6 kwa kila kilomita, kipande cha Lot 3 walichopewa Waturuki bila ya tenda ya wazi wanakijenga kwa gharama ya juu ya Dola milioni 5.2 kwa kila kilomita.

Vile vile, kipande cha Lot 4 walichopewa Waturuki hao hao bila ya tenda ya wazi (single source) wanakijenga kwa gharama kubwa mno ya Dola Marekani milioni 5.5 kwa kila kilomita.

"Kulingana na tofauti hiyo, hapakuwa na faida ya kiuchumi kwa TRC kwa kutoa kandarasi kupitia njia ya chanzo kimoja kwa M/S Yapi Merkezi. Hii ni kwa sababu gharama awali za miradi mingine zilikuwa chini ikilinganishwa na mkataba aliopewa mkandarasi wa kipande cha 3 na 4," alisema CAG.

"Zaidi ya hayo, niligundua kuwa mawanda ya kazi kwa kipande cha 3 na 4 ya mradi ulikuwa mdogo na ulikuwa na miundombinu michache kuliko ile ya kipande cha 1, 2, na 5, na miundo mikuu zaidi."

CAG amependekeza kuwa menejimenti ya TRC iweke kipaumbele katika matumizi ya mbinu shindani ya ununuzi katika shughuli za manunuzi za siku zijazo ili kuepuka upotevu wa fedha za walipa
kodi.

Chanzo: Jambo TV

Hicho kichwa cha habari mnapotosha.

CAG report inaonesha kabisa kuwa LOT3 [makutupora - Tabora] ilisainiwa December 2021 magufuli hakukuwepo, sasa mnamuhusishaje na wizi wa serikali ya Samia
 
Kichwa Cha habari, Sani Abacha wa Tanzania?

Hicho kichwa cha habari mnapotosha.

CAG report inaonesha kabisa kuwa LOT3 [makutupora - Tabora] ilisainiwa December 2021 magufuli hakukuwepo, sasa mnamuhusishaje na wizi wa serikali ya Samia
 
Haya ni mataarifa ya kutoka kwa mwimba pambio maarufu wa aw5🤔.Nani anayemwelewa na kumwambia mwana mapambio huyu🏃

Hicho kichwa cha habari mnapotosha.

CAG report inaonesha kabisa kuwa LOT3 [makutupora - Tabora] ilisainiwa December 2021 magufuli hakukuwepo, sasa mnamuhusishaje na wizi wa serikali ya Samia
 
Acha upumbavu wewe,kwani hapo kioichoandikwa ni kweli au sio kweli?

Pili Samia sio kama yule aliyekuwa analinda Ufisadi ukifichua unafukuzwa au kupotezwa.

CAG sema ukweli wote,Nchi ilifiliaika sana awamu ya 5 na wanufaika mpo ndio maana mnatokwa na mapovu sana.

WEWE NDIO MPUMBAVU!

Hicho kichwa cha habari mnapotosha.

CAG report inaonesha kabisa kuwa LOT3 [makutupora - Tabora] ilisainiwa December 2021 magufuli hakukuwepo, sasa mnamuhusishaje na wizi wa serikali ya Samia
 
Awamu ya sita watajifichia kwenye mgongo wa awamu ya Tano mpaka wanamaliza muda wao.

Ila awamu itayofuata itawavua nguo.

Mleta habari amesahau sentesi moja tu kuwa Magufuli na Samia walisababishia hasara Taifa maana wakati Magu akiwa Rais Samia alikua makamu wake hivyo wametusababishia Hasara wote wawili.

Kwakua Samia yupo Sasa ni muda wa kutujibu fedha zimepoteaje maana mwenzake hayupo

Hicho kichwa cha habari mnapotosha.

CAG report inaonesha kabisa kuwa LOT3 [makutupora - Tabora] ilisainiwa December 2021 magufuli hakukuwepo, sasa mnamuhusishaje na wizi wa serikali ya Samia
 
Uzalendo uchwara wa awamu iliyopita unazidi kuanikwa peupe

Hicho kichwa cha habari mnapotosha.

CAG report inaonesha kabisa kuwa LOT3 [makutupora - Tabora] ilisainiwa December 2021 magufuli hakukuwepo, sasa mnamuhusishaje na wizi wa serikali ya Samia
 
Naona kila kitu mnataka kumpin nacho JPM...JPM alihusika na kipande cha 1,2 na 5...hivyo vingine vyote vimesainiwa mbele ya awamu ya 6.

Mkataba ya Lot 3 ulisainiwa ikulu Dec 28 2021 miezi 9 tangu JPM afariki, Lot 4 ulisainiwa Ikulu July 2022 zaidi ya mwaka na nusu tangu afariki.
Hapo JPM anahusikaje, au alifufuka akaja kuongoza mchakato?

Huu Uongo mnaousambaza unawasidia nn? Kwann hamtaki kua responsible kwa makosa mnayoyafanya?itafika 2030 bado mtamlaumu JPM kwa ufisadi wa 2029.

Agenda yao ni kulinda Serikali inayoendeshwa na WAHUNI, japo CAG anakili kwamba Zaidi ya hayo, niligundua kuwa mawanda ya kazi kwa kipande cha 3 na 4 ya mradi ulikuwa mdogo na ulikuwa na miundombinu michache kuliko ile ya kipande cha 1, 2, na 5, na miundo mikuu zaidi.
 
Mchakato ulianza toka enzi ya awamu ya mwendazake ambapo bodi kadhaa za wakurugenzi wa TRC walisimamia

Bodi ya Wakurugenzi TRC tarehe 17 February 2023 chini ya mwenyekiti Prof. John Wajanga
Kondoro waliotambulishwa ni Bw. Benjamini Adam Mbimbi, Bw. Kondo Abdalah Kibugula, Bw. Joseph Elias Salema, Bw. Juma Samhando Kijavara na Bw. Peter Mayunga Noni.

Wajumbe waliomaliza muda wao ni Bw. Wolfgang Ephraim Salia, Bi. Consolata Chrisostom Ngimbwa, Bw. Karim Godfrey Mattaka, Bw. Rogatus Hussein Mativila na Bw. Mahamud Mashaka Mabuyu.

Wajumbe wanaoendelea na nafasi zao ni pamoja na Bw. Jabir Bakari na Bi Lilian Ngilangwa. Baadhi ya wajumbe waliomaliza muda wao walipata fursa ya kutoa neno kwa menejimenti ya Shirika na kupongeza jitihada kubwa zilizofanywa kuhakikisha watumishi wanafanya kazi kwa weledi na kuleta tija katika utendaji wa Shirika.

Sources : TRC RELI TV / Mwanzo | TRC

Soma sehemu ya mwisho ya CAG report kuhusu TRC na standard, utaona jamaa wa TRC walibetua mara baada ya Magufuli kufa na kutoa tenda kinyume na sheria na kusign december 2021.
 
JPM alikuwa mwizi sana, nadhani Afrika mashariki na kati ndiye Rais aliyeongoza kwa wizi

Hicho kichwa cha habari mnapotosha.

CAG report inaonesha kabisa kuwa LOT3 [makutupora - Tabora] ilisainiwa December 2021 magufuli hakukuwepo, sasa mnamuhusishaje na wizi wa serikali ya Samia
 
Inabidi majaliwa na mpango pamoja na Samia wapishe maana ni sehemu ya serikali iliyosababisha hasara

Hicho kichwa cha habari mnapotosha.

CAG report inaonesha kabisa kuwa LOT3 [makutupora - Tabora] ilisainiwa December 2021 magufuli hakukuwepo, sasa mnamuhusishaje na wizi wa serikali ya Samia
 
Magufuli alikua mwizi aisee dah!

Hicho kichwa cha habari mnapotosha.

CAG report inaonesha kabisa kuwa LOT3 [makutupora - Tabora] ilisainiwa December 2021 magufuli hakukuwepo, sasa mnamuhusishaje na wizi wa serikali ya Samia
 
Kuna Wanawake wakifiwa Waume zao tu ndo utaanza kuona Rangi zao halisi .
Ripoti ya CAG huwa inahoji masuala kwa Serikali na Serikali inatakiwa kujibu. Ajabu kwamba CAG anatenganisha awamu na awamu. Basi alete na ripoti inayoonesha ufisadi na ubinafsishaji mbovu wa awamu ya 3 na ya 4 pia ambao umetufikisha hapa tulipo. Unazungumzia awamu!
Kwa hiyo ripoti ni kwa ajili ya awamu ya 5? Na bunge nalo ni awamu ipi? Waziri wa fedha wa hiyo awamu ya 5 si yupo? Basi yeye ndo atujibu
 
Tukisema Rais Samia ni Rais dhaifu kuwahi kutokea muwe mnaelewa angalia lot aliyosaini zilivyokuwa zinanuka ufisadiView attachment 2582647View attachment 2582648
Sasa atupe maelezo ya kina pesa zetu ziko wapi?

1.7 trillion zinapotea anaona hiyo ni lot moja tu bado zingine.

Ndege wamepiga 29 Milion USD .

Hapo ni kwa uchache tu.

Huyu hatufai huyu aachie tu hiyo nafasi.

Hasara atayotutia kwa muda atakao kuwa madarakani italiumiza. Taifa kwa muda Mrefu sana.
 
Kwani waliwahi kunyang'amywa? Sana sana hizo lots za kuanzia tabora-isaka, fela-isaka, ndizo walisema wapewe wachina, kwani kazi itachelewa sana wakimtegemea huyu mmoja!! Na ki uhalisia wachina ndio walitakiwa kujenga reli yote, ndio hayo madudu yalifanyika(kulingana na ripoti ya CAG wakatoswa)mbunge mpina ndio alilishikia saba bango hilo suala hadi akataka iundwe kamati maalumu ya kufuatilia,kwani kuna sehemu km ndogo ,gharama kubwa,sehemu nyingine km kubwa gharama kidogo,akawa ana hisi kuna upigaji
hatuna Rais makini.

Kama kwa maelezo Yako "mchakato" ulianzia kabla ya kusainiwa December 2021 mchakato ambao haujatuonesha kwa kutupa ushahidi japo kidogo tu kuwa ulianzia lini hasa kwanini Rais akubali kusaini mkataba uliojaa ufisadi wakati ana kila resources za kumsaidia kujua uhalali wake??

Au alisaini makusudi ili aje atuambie haya unayosema wewe??

Kama ndio hivyo basi hayupo makini maana awamu hii na ile zote zinamhusu.

Hatuna Rais makini ni hilo tu, na ni vyema akatueleza hizi 1.7 alizosaini huu mkataba yeye anaushuhudia na CAG anasema ni hasara kazipeleka wapi??
 
Hicho kichwa cha habari mnapotosha.

CAG report inaonesha kabisa kuwa LOT3 [makutupora - Tabora] ilisainiwa December 2021 magufuli hakukuwepo, sasa mnamuhusishaje na wizi wa serikali ya Samia

CAG kasomea kazi yake, hawezi kupotosha, game zima limechezwa na JPM
 
ila hamuonesh mali zake , nyiny mmetumwa , watu km nyiny hukum yen ni kutenganisha vchwa tu maana mnaukumbatia wiz kwa kupewa buku 3 ya bando
Unajua serikali imetaificha trilioni ngapi za JPM? Unadhani china kina Hela za pkea bargaining tu? Unajua uturuki waliopewa tenda ya SGR wamemtunzia mabilioni mangapi huko? Unajua Misri ana trilioni ngapi kwa sababu ya mradi wa bwawa la Mwalimu Nyerere.?

Unajua kwa nini Kila mradi lazima Mfugale awepo? Ndio alikuwa ana negotiate 10 pasenti na kuitunza, mara hee, JPM kafa, Mfugale bado ana matrilinloni katika akaunti, watu wakayafunga, wakamuweka mtu kati, akaamua kufa.

Hisa zake Songoro Marine unazijua? Ilifikia walikiona hata mfereji wa maji wa mtu anakojoa wanataka kujenga pantoni ili kampuni yake ipate Hela.

Nyanza Road, Mayanga? Majumba Kila Mkoa? Tena maghorofa?
 
Ripoti mpya ya CAG iliyotolewa Aprili 6, 2023, yasema Serikali ya Awamu ya 5 ilivunja sheria ya nchi kwenye utoaji wa kandarasi ya reli

Ilikubali masharti mabovu ya Benki ya StanChart kuwapa kandarasi Waturuki kwa gharama ya juu bila tenda ya wazi ya ushindani

Na Waandishi Wetu

SERIKALI ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli iliingizia taifa hasara ya Dola za Marekani milioni 742.4 (zaidi ya Shilingi trilioni 1.7) kwenye ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR baada ya kukubali masharti mabovu ya mkopo wa benki ya Standard Chartered.

Ripoti Kuu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo 2021/22 iliyotolewa juzi na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilisema kuwa hasara hiyo kwa taifa ilitokana na Serikali ya Magufuli kukubali masharti ya ajabu ya mkopo wa kibiashara wa Dola za Marekani Bilioni 1.46 kutoka kwa Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa SGR uliotolewa mwaka 2020.

Moja ya masharti ya mkopo huo ni kuwa Serikali ivunje Sheria ya Manunuzi ya Umma kwa kutoa kandarasi mbili za ujenzi wa reli ya SGR kwa kampuni ya Kituruki ya Yapi Merkezi Insaat VE Sanayi As bila zabuni ya wazi ya kushindanisha kampuni nyingine.

Serikali ya Magufuli ilikubali masharti hayo ya ajabu kwa kutoa kandarasi kwa Waturuki kinyume na sheria za nchi.

CAG alibaini kuwa gharama za ujenzi wa kipande cha reli ya Makutupora-Tabora (Lot 3) iliongezeka kwa Dola za Marekani milioni 1.3 (zaidi ya Shilingi Bilioni 3) kwa kila kilomita wakati gharama ya ujenzi wa kipande cha reli ya Tabora-Isaka (Lot 4) iliongezeka kwa Dola milioni 1.6 (Shilingi Bilioni 3.74) kwa kila kilomita.

"Shirika la Reli Tanzania (TRC) halikutumia njia ya ununuzi ya ushindani katika ujenzi wa reli ya kisasa kwa kipande cha tatu na cha nne na kusababisha kuongezeka kwa Dola za Kimarekani milioni 1.3 na milioni 1.6 kwa kilomita mtawalia ikilinganishwa na mikataba ya awali,," alisema CAG.

Reli ya Makutupora-Tabora yenye urefu wa kilomita 368 inajengwa kwa gharama ya Dola za Marekani Bilioni 1.9, wakati kipande cha Tabora-Isaka chenye urefu wa kilomita 165, kinajengwa kwa gharama za Dola za Marekani milioni 900.

Maana yake ni kuwa taifa limeingia jumla ya hasara ya Dola za Marekani 742.4 (zaidi ya Shilingi trilioni 1.7) kwenye vipande hivyo viwili vya reli.

"Mapitio yangu ya njia za ununuzi zilizotumika katika ununuzi wa mkandarasi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha 3 na 4 yalibainisha kuwa Benki ya Standard Chartered ambako Serikali ilipata mkopo iliweka masharti kwamba ingekubali jukumu la kuwa Mratibu wa
Kimataifa, na Wakala Kiongozi Aliye na Mamlaka kupanga ufadhili na mkopo kwa Wizara ya Fedha na Mipango (MoFP) tu kwa masharti kwamba kampuni ya Yapi Markezi iteuliwe kama Mkandarasi," alisema CAG kwenye ripoti hiyo.

"Wizara
ya Fedha na Mipango (MOFP) ilikubali mkopo huo kwa masharti yasiyofaa kutoka Benki ya Standard Chartered kupitia barua yenye kumbukumbu namba PST/GEN/2021/01/55."

Wakati barua hiyo inaandikwa, Doto James ndiye aliyekua Katibu Mkuu wa Hazina (PST) kwenye Wizara ya Fedha na Mipango.

CAG amebaini zaidi kuwa TRC iliamua kuchagua njia ya kutoa zabuni kwa njia
mzabuni mmoja licha ya ushauri uliotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Bodi ya Zabuni, ambayo iliishia kuigharimu serikali fedha zaidi, ambayo ingeweza kuepukwa.

"Ni maoni yangu kwamba, hakuna mfadhili anayeweza kuitaka Serikali ya Tanzania kumpa mkataba mkandarasi pasipo kuwa na uwazi, ushindani, usawa na haki kwa wakandarasi wote wenye sifa na wanaostahili katika mchakato wa ununuzi," alisema CAG.

Ripoti ya CAG ilibaini kuwa baada ya Serikali ya Magufuli kukubali masharti yasiyofaa ya kuwapa kandarasi ya Lot 3 na Lot 4 kwa Yapi Merkezi bila tenda ya wazi ya ushindani, Waturuki hao wakaongeza gharama ya ujenzi kuliko kawaida na kuliingizia taifa hasara kubwa.

Wakati vipande vingine vya reli ya SGR ya Tanzania vinajengwa kwa gharama ya kati ya Dola za Marekani milioni 3.9 na Dola la Marekani milioni 4.6 kwa kila kilomita, kipande cha Lot 3 walichopewa Waturuki bila ya tenda ya wazi wanakijenga kwa gharama ya juu ya Dola milioni 5.2 kwa kila kilomita.

Vile vile, kipande cha Lot 4 walichopewa Waturuki hao hao bila ya tenda ya wazi (single source) wanakijenga kwa gharama kubwa mno ya Dola Marekani milioni 5.5 kwa kila kilomita.

"Kulingana na tofauti hiyo, hapakuwa na faida ya kiuchumi kwa TRC kwa kutoa kandarasi kupitia njia ya chanzo kimoja kwa M/S Yapi Merkezi. Hii ni kwa sababu gharama awali za miradi mingine zilikuwa chini ikilinganishwa na mkataba aliopewa mkandarasi wa kipande cha 3 na 4," alisema CAG.

"Zaidi ya hayo, niligundua kuwa mawanda ya kazi kwa kipande cha 3 na 4 ya mradi ulikuwa mdogo na ulikuwa na miundombinu michache kuliko ile ya kipande cha 1, 2, na 5, na miundo mikuu zaidi."

CAG amependekeza kuwa menejimenti ya TRC iweke kipaumbele katika matumizi ya mbinu shindani ya ununuzi katika shughuli za manunuzi za siku zijazo ili kuepuka upotevu wa fedha za walipa
kodi.

Chanzo: Jambo TV
Hapo aliyekuwa makamu wa rais, waziri mkuu, waziri wa fedha na waziri wa ujenzi wachomokaje kwenye ufisadi huu wa kutisha?
 
Wakati huya yakitokea makamu wa rais alikuwa rais wa sasa
Waziri mkuu alikuwa Majaliwa
Waziri wa fedha alikuwa makamu wa rais wa sasa
Waziri wa ujenzi alikuwa Makame
NB: SERKALI YA MAGUFULI = SERIKALI YA CCM
 
Back
Top Bottom