CAG aibua ufisadi TPA ya Deus Kakoko, Ni mbaya kuliko wa Kigwangalla

CAG aibua ufisadi TPA ya Deus Kakoko, Ni mbaya kuliko wa Kigwangalla

sasa hapo kipi umekiona kigeni? wewe hujui kuwa yule aliyetoka tetesi ni kwa sababu ya kuibua mambo yaliyoko kwenye serikali zaidi, na mkuu anataka serikali ione hakuna sehemu kuna upigaji?
Mwangalieni huyu! Sasa huyo Mkuu ndie Mkurugenzi wa Bandari?!

Jibu ni kwamba NDIYO, aliwekwa kumlinda Mkuu na mihamala yake inayopitishwa Ikulu bila hata kujadiliwa Bungeni!!

Jibu ni kwamba NDIYO, aliwekwa kumlinda Mkuu ili aendelee kuficha manunuzi mabovu kama yale ya ndege za ATCL ambazo CAG aliyepita alianza kunusanusa na kusema wazi kwamba ameshindwa kupata data!!

Jibu ni NDIYO, amewekwa kumlinda Mkuu ili tenda za kujuana kama zile za ujenzi wa Chato International Airport aliyopewa swahibu wake Mkuu watu wasifahamu mengi!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wiki zima mitandao ya jamii imemshupalia Dr Hamis Kigwangalla kwa ufisadi wa kutumia Tsh 2.58 bila idhini ya Bunge. Pengine Kigwangalla yuko kwenye "spotlight" kwa vile siku zote ni mtu wa majibizano kwenye mtandao ya jamii.

Sasa kuna manunuzi ya Tsh 22.69 yaliyifanywa na TPA ya Deus Kakoko. Katika DHAMBI au makosa makubwa ya manunuzi yanayo mhusisha mnunuzi moja kwa moja na RUSHWA ni kununua kwa SINGLE SOURCE.

Tumpunzishe Dr Kigwangala, tujikite na huyu Deus Kakoko anayejinasibu kuwa ni "home port" na JPM na huwa ana nguvu kuliko mawaziri wa wizara ya mawasiliano. Kumbuka alishindana na Waziri Mbarawa, na Mbarawa akang'oka.View attachment 1413440
Ni vibaya sana kumhukumu mtu, wakati PAC na bunge hawajajibu hiyo hoja ya CAG. Tuwe na subira ili kupata majibu ya uhakika. Isije ikawa kama stori za tril 1.5 na mwenyekiti wa PAC, Naghenjwa Kaboyoka (Chadema M.p) alikuja kusema ukweli.
 
CAG anapofanya ukaguzi usidhani yale yote aliyoyaibua kwenye ukaguzi ni ya kweli. Unapokaguliwa kunatakiwa pia mrejesho/majibu kutoka kwa mkaguliwa na hivyo majibu yakiishatolewa yanaweza kumridhisha CAG. Kumhukumu Meneja Mkuu wa TPA bado ni mapema sana. Bwana Kakoko ni mfanyakazi bora na wa kuigwa.
Doho tabu...

Wasukuma bhana... dah!
 
Kwa wiki zima mitandao ya jamii imemshupalia Dr Hamis Kigwangalla kwa ufisadi wa kutumia Tsh 2.58 bila idhini ya Bunge. Pengine Kigwangalla yuko kwenye "spotlight" kwa vile siku zote ni mtu wa majibizano kwenye mtandao ya jamii.

Sasa kuna manunuzi ya Tsh 22.69 yaliyifanywa na TPA ya Deus Kakoko. Katika DHAMBI au makosa makubwa ya manunuzi yanayo mhusisha mnunuzi moja kwa moja na RUSHWA ni kununua kwa SINGLE SOURCE.

Tumpunzishe Dr Kigwangala, tujikite na huyu Deus Kakoko anayejinasibu kuwa ni "home port" na JPM na huwa ana nguvu kuliko mawaziri wa wizara ya mawasiliano. Kumbuka alishindana na Waziri Mbarawa, na Mbarawa akang'oka.View attachment 1413440
Huyu ni mpigaji sana wachunguze upigaji wa bandari ya Kigoma. na wachunguze washauri au wapigaji walio karibu naye Mr. Tony aliyekuwa TAFFA na wengine
 
Eng.Kakoko ni mtumishi aliyetukuka amejenga miradi mingi ya bandari/Gati karibu sehemu zote muhimu za maziwa yetu ambako usafirishaji wa abiria na Huduma ulikuwa katika hali mbaya sana.
Wewe tetea wakwapuaji kama nayo sifa
 
Tofauti na awamu iliyopita tulinufaika wote na ufisadi awamu hii wanufaika wa chache na upiga haswaa.
[/QUOTE]
Nimeipenda hii sana.. kwa Maana ukianglia ESCROL na wadogo zake hakina MEREMETA issues watu wengi walipata Maji ya Kunywa lakini hii ya sasa ni Kimya Kimya.....
 
Hamisi wana m target sana kisiasa. Sio mbaya hivyo. Kuna watu wabaya zaidi. Shida ya Hamisi ni kuongea. Angekuwa anakaa kimya na kuignore baadhi ya mambo yangekuwa yanapita kimya kimya.
Shida ni "Hamisi".
 
Huyu kakoko huwa anatamba sana na kunyanyasa wanyakazi wa chini yake, huwa anasema bila aibu wala kificho kuwa hakuna wa kumtisha bali mmoja tu. Anyway ni mtu wa kanda pendwa tena home boy. Ila yana mwisho!
 
Eng.Kakoko ni mtumishi aliyetukuka amejenga miradi mingi ya bandari/jetty karibu sehemu zote muhimu za maziwa yetu ambako usafirishaji wa abiria na Huduma ulikuwa ni mbaya sana.
Sidhani kama unajua mada iliyoletwa au ni akili za kuokota ndio zinakutuma kuandika huu utumbo.
 
sasa hapo kipi umekiona kigeni? wewe hujui kuwa yule aliyetoka tetesi ni kwa sbu ya kuibua mambo yaliyoko kwenye serikali zaidi, na mkuu anataka serikali ione hakuna sehemu kuna upigaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
Narudia: Watu wanatuhumu Ofisi ya Rais kufanya manunuzi ambayo hakuna anayefahamu zaidi ya Magu na Dotto, labda na wengine watu wa karibu! Haya manunuzi yanakiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma!!!

Mfano mzuri ni ununuzi wa ndege kwa jina la Wakala wa Ndege za Serikali. Wabunge wa upinzani ambao ndio walikosoa zaidi kuhusu CAG mpya wanaamini manunuzi yale hayakufuata taratibu!

Kwa mujibu wa Zitto akiwa Bungeni, ndege zilinunuliwa kupitia Fungu #62 la Wizara ya Uchukuzi lakini baada ya Wabunge kumtaka CAG Assad afanye ukaguzi wa manunuzi ya zile ndege, Zitto akaendelea kusema kwa lengo la kutaka kuficha taarifa, serikali ikahamishia Wakala wa Ndege za Serikali kwenye Ofisi ya Rais kupitia tangazo la serikali la Juni 2018.

Hata wewe leo hii ukiulizwa, tenda ya ununuzi wa ndege ilitangazwa wapi, sidhani kama unaweza kutoa jibu lenye uthibitisho! Hata nikikuuliza taarifa za ukaguzi wa ATCL na ndege zake, sidhani kama utakuwa na jibu!

Profesa Mbarawa kwa mfano, baada ya kubanwa Bungeni hakuna alichosema zaidi ya kwamba ATCL haijakaguliwa tangu 2007 wakati watu interest yao KUBWA ilikuwa ni kufahamu mchakato huu wa sasa ambao main actor ni Magu!!
 
Back
Top Bottom