CAG: ATCL imetengeneza hasara ya Tsh. Bilioni 153.542 ndani ya miaka Mitano

CAG: ATCL imetengeneza hasara ya Tsh. Bilioni 153.542 ndani ya miaka Mitano

View attachment 1746920

MATAGA bado hamjaamini kuwa bunge ni dhaifu? Bado ninaamini mwenda zake alikuwa rais wa wanyonge? Bado unaamini alipambana na ufisadi?

Mwenye takwimu za ufisadi enzi za JK na JPM tulinganishe.
Asante Mungu kwa kutupunguzia makali,sa hivi angeongeza miaka mitano ingekuaje?🤔🤔
Hapo tuweke serikali nyingine tu, huyu mama sidhani kama ataweza komesha majizi. Kama mfupa ulimshinda mwendazake, huyu mama ataweza kweli?. Nategemea wazee wa ruksa watakula mpaka na miguu kipindi cha Sasha. Ni suala la wakati tu.
 
Kampuni ya Ndege imekuwa ikitengeneza hasara kwa miaka 5 mfululizo na mwaka huu ilitengeneza hasara ya Sh. Bilioni 60.246. Kwa miaka mitano imetengeneza hasara ya Sh. Bilioni 153.542.

View attachment 1746953

====

Kampuni ya Ndege Tanzania

Nilifanya ukaguzi wa kiutendaji (Startegic and Operational Efficiency) kwenye Kampuni ya Ndege Tanzania na kubaini yafuatayo:

Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2020, Serikali ilikuwa imenunua ndege 8 kwa gharama ya Sh. Trilioni 1.028 katika juhudi ya kuifufua Kampuni ya Ndege Tanzania.

Ndege hizo zinamilikiwa na Wakala wa Ndege za Serikali na ATCL huzikodisha.

Pamoja na kununua ndege, kwa miaka mitano yaani kuanzia 2015/16 hadi 2019/20 Serikali imeisaidia Kampuni ya Ndege kiasi cha Sh. Bilioni 153.711 kwa ajili ya shughuli za uendeshaji na maendeleo.

Kampuni ya Ndege imekuwa ikitengeneza hasara kwa miaka 5 mfululizo na mwaka huu ilitengeneza hasara ya Sh. Bilioni 60.246. Kwa miaka mitano imetengeneza hasara ya Sh. Bilioni 153.542.

Hata hivyo nilibaini changamoto zifuatazo ambazo zinatakiwa kushughulikiwa ili kuimarisha utendaji wa Kampuni ya Ndege:

Bodi ya Wakurugenzi haina mjumbe hata mmoja ambaye ana uzoefu kwenye masuala ya usafiri wa anga.

Wakati wa changamoto ya Corona (Covid 19) ndege nyingi zilikuwa zimesimama lakini ATCL ilikuwa inatozwa gharama za ukodishaji bila kujali kwamba ndege zilikuwa hazifanyi kazi kutokana na changamoto ya Covid 19. Hii inatokana na ukweli kwamba Mkataba wa ukodishaji kati ya TGFA na ATCL hauna kipengele cha Force majure. Katika kipindi kati ya Machi 2020 na Juni 2020 ATCL ilitozwa na TGFA kiasi cha Sh. Bilioni 15.464 kwa ajili ya ukodishaji wa ndege.

ATCL imerithi madeni makubwa ambayo hutozwa riba, kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 ATCL imetozwa riba ya Sh. Bilioni 12.497.

Kutokana na madeni hayo, inakuwa vigumu kwa ndege za ATCL kusafiri kwenda nje ya nchi kwani zinaweza kukamatwa.

Kuna changamoto ya viwanja vya ndege hapa nchini kiasi kwamba ndege za ATCL haziwezi kuruka usiku na pia kuna viwanja ambavyo ndege haziwezi kutua zikiwa zimechukua abiria kwa uwezo wake.

Soma pia:

1) ATCL yatengeneza faida ya $14M, yafuatayo yanasisimua
Kwa muda huu tangu ifufuliwe je wamefikia Beakeven kweli ATCL au ni kuwaonea tu. Je CAG amesoma business Plan. Hasara imetokana na nini? Ndege ni kati ya miradi ya kifahari na urithi wetu.
 
Sasa kama mambo ndivyo yako hivi since the beginning of this project, hilo gawio la faida ya Tshs. 25bn ambazo ATCL walitoa kwa serikali mwaka 2019 zilitoka wapi..?

Hivi ndiyo tuseme Hayati John P. Magufuli akishirikiana na hawa ATCL walikuwa wanacheza mchezo hatari na wa kijinga kiasi hiki dhidi ya Watanzania..?

I am completely speechless and puzzled na Urais wa John Pombe Magufuli maana mtu akisoma haya hataelewa maana ya haya mambo ilikuwa ni nini hasa..

Ni kana kwamba nchi ilikuwa inaongozwa na mwizi tu 100%...
Waligawa hasara jamaa alikua na fix balaa et anatetea wanyonge....bora JK alikua anagawa mishahara tuu na ufisadi wake hela zilikua mtaani
 
Hapo tuweke serikali nyingine tu, huyu mama sidhani kama ataweza komesha majizi. Kama mfupa ulimshinda mwendazake, huyu mama ataweza kweli?. Nategemea wazee wa ruksa watakula mpaka na miguu kipindi cha Sasha. Ni suala la wakati tu.
Bila katiba mpya tuzoee tu kuwa na wezi hakuna nmna
 
Huyu mjinga naye marehemu angekuwepo angetoa hii report?
marehem ndie aliemchagua. weakness yake kubwa marehem ni ubishi, na hakutaka taarifa mbaya. huyu angempelekea hiyo report kazi yake ingeishia hapo hapo.

get back to CAG aliepita. aliibua mambo kama haya. tena this time jeshi la polisi likapatwa na kashfa kubwa.
CAG prof assad kilimkuta nini?
 
Ndiyo maana nakwambia report hii asingeipeleka hata kidogo
 
Dreamliner moja iliyopaki ni sawa na matreka elf 10 mapya na vifaa vyake tena kwa cash, Kama ni kwa mkopo unapata trekta elf 50 za horse power 75.Trekta moja ulima heka 25 kwa siku kwa speed ya kivivu. Trekta moja utoa ajira kwa vijana 100.
So badala ya dreamliner moja iliyopaki kutoa ajira kwa watu 30 zingekuwa ni trekta zingetoa ajira milioni 5 za moja kwa moja achilia wategemezi wao.Ajira zote zilizonunulia ndege zingenunua trekta laki moja ambazo zingetoa ajira milioni 12 nchi nzima.Ndege ugusa wachache,kilimo ugusa wote.Kama Malaysia waliwekeza kwenye michikichi tu ndo wanailisha dunia mafuta ya kula na bado awajalijaza soko. Soko la mazao ya kilimo duniani ni kubwa hata KILA mtu alime tza hatutoweza kulijaza.Hela zilizotupwa kwenye ndege tilioni moja tungepata matreka laki 2 yangeajiri vijana milioni 12 zingemaliza tatizo la ajira nchini kwa kuwekeza kwenye kilimo mkakati na zingesharudi ndani ya miaka 3 tungepata pesa tosha za kigeni kukamilisha miradi yote bila kutegemea kukopa.Kupitia kilimo tu tungekuwa uchumi wa kati.Kama wakoloni wao waliweza maliza tatizo la ajira nchini why tunashindwa?Tangu Uhuru bado atujapata kiongozi sahihi mwenye uchungu anaeguswa na ugumu wa maisha ya watz,zaidi ya kuyafanya maisha yazidi kuwa magumu.Kwann watumishi wasipewe misamaha ya Kodi Ili wajinunulie magari binafsi kuliko kuwa na utitiri wa magari ya serikali ambayo hayazalishi,hayana faida ni hasara kwa mlipa Kodi V8 moja tu ni sawa na matrekta 10 mapya na jembe zake hapo ni sawa na ajira elf 1.
Tuendelee tu kuwalaumu mabeberu juu ya kushindwa kwetu aliyetupa Mali alitunyima akili.
 
marehem ndie aliemchagua. weakness yake kubwa marehem ni ubishi, na hakutaka taarifa mbaya. huyu angempelekea hiyo report kazi yake ingeishia hapo hapo.

get back to CAG aliepita. aliibua mambo kama haya. tena this time jeshi la polisi likapatwa na kashfa kubwa.
CAG prof assad kilimkuta nini?
Marehemu na ukweli ni mbingu na ardhi.Aliwadanganya futureless people ( wanyonge) kwamba anajenga miradi kwa pesa za ndani huku deni la taifa linakua kwa kukopa nje.Alikuwa ni propagandist Mkubwa sana kwa kuitumia vibaya tbc.
 
Afu walikuwa hawatangazwi ndio mbya zaidi,hakuna wapinzani wa kusema tena kama zamani
Wapinzani Ndugai aliwafunga midomo wangesemea wapi ndg yangu wakilalamika anawatoa nje.
 
Hujui chochote!! Nia ya ulichosema huwa ni kutotoa huduma kwa faida. Sio kujiendesha kwa hasara. Hata sijui kama una uwezo wa kutambua tofauti!

Ujinga wa namna hii ndio shida ya nchi. Hizi ndege zinafanya safari za ndani, vipi kama zingekuwa zinafanya safari za kimataifa - ungesema zinatoa huduma???

Mawazo yenu ya “ujamaa na kujitegemea ndio njia PEKEE ya kujiletea maendeleo” ndio yametifikisha hapa. Ingekuwa hivo miaka yote hii ya uhuru si tungekuwa tunazizidi nchi za kibapari?? Ujinga from right, left and center!!

Walau ungejikita kujifunza kuandika kwanza, ndipo ufikirie kuhusu uwezekano wa kujadili nami mambo makubwa... hadi hapo, kwa sasa nachagua kukupuuza tu.
 
Back
Top Bottom