CAG: Mkandarasi alichukua tenda kwa 104b akaiuza kwa 40b akapiga cha juu 64b

Namnukuu CAG Kichere

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari iliingia mkataba na “Mkandarasi Mkuu” wa shilingi bilioni 172.36 tarehe 3 Agosti 2019 wa muda wa mwaka mmoja hadi kufikia mwezi Agosti 2020 kwa ajili ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia meli katika bandari ya Tanga, kufanya tathmini ya athari za kimazingira, na kununua vifaa kwa ajili ya shughuli za bandari. Kwa kulingana na mkataba, gharama ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia meli katika Bandari ya Tanga ilikuwa ni shilingi bilioni 104.92 (asilimia 60 ya bei yote ya mkataba).

Hata hivyo, mnamo tarehe 1 Agosti 2019, “Mkandarasi Mkuu” iliingia makubaliano na “Mkandarasi Mbia” kwa ajili ya kazi ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia Meli kwa bei ya mkataba dola
za marekani milioni 18.15 sawa na shilingi bilioni 40.46 kwa kipindi cha miezi 11 bila kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari. Pia “Mkandarasi Mkuu” aliingia mkataba na “Mkandarasi Mbia” hata kabla ya kusaini mkataba wake na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Kuingia mkataba bila kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Bandari ilikuwa ni kinyume na Kifungu Kidogo cha 4.4 cha Masharti ya Jumla ya Mkataba kati ya Mamlaka ya Bandari na Mkandarasi Mkuu ambacho
kinaizuia Mkandarasi Mkuu kutoa sehemu ya kazi kwa Mkandarasi mwingine, na ikiwa kunauhitaji wa kutoa kazi kwa Kampuni nyingine kutekeleza kazi zilizoko kwenye mkataba, Mkandarasi Mkuu anapaswa kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Bandari siku 28 kabla ya kutoa kazi hiyo.

Aidha, nilibaini jumla ya malipo yaliyolipwa kwa kazi ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia Meli yalikuwa dola za
marekeni milioni 18.22 sawa na shilingi bilioni 40.62, kiasi hiki, pia, kinajumuisha malipo ya dola za marekani 73,824 sawa na shilingi milioni 164.55 kwa huduma za wakala wa meli kwa “Mkandarasi mbia”. Ulinganifu wa kiasi kilichotozwa na Mkandarasi Mkuu shillingi bilioni 104.92 na kiasi alicholipwa na “Mkandarasi mbia”
shilingi bilioni 40.62 inaonesha Kiasi kilichotozwa na Mkandarasi Mkuu kimezidi kiasi halisi kilichotumika kufanya malipo ya kazi hiyo kwa shilingi bilioni 64.30.

My Take
Msimamo wangu ni uleule,kwa mwendo huu ni bora nchi ikauzwa kila mtu achukue chake ajue anafanya nini. Inatia uchungu sana
Halafu eti tunamsifia yule Dictator? Na huko si ndiyo aliweka Yule rafiki yake aliyeonyofolewa na Mh. SSH? Yaani Bora alizikwa Tu. Hii nchi ilikuwa inauzwa kimya kimya. By the way hivi asili yake ni nchi gani? Namaanisha babu yake alitoka nchi gani vile? Alijitetea kuwa babu yake alitoka nchi Ile eti akaja kumzalia Joseph Tanzania na John akazaliwa Tz. Mnafiki Sana Yule.
 
Kakoko alikuwa mwizi sana, TPA ilikuwainaendeshwa kama kampuni binafsi na alilindwa na dikteta
 
Ee bana eeh [emoji848][emoji848][emoji848]

Duuh Mbona noma mbaya?!
 
Hospitali dawa hakuna, maji hakuna, maskini wanakufa kwa kukosa vipimo , vifaa tiba, dawa lakini pesa za Umma za zinapigwa kirahisi kiasi hicho jamani [emoji24][emoji24][emoji24]
 
Wakianza kuwekwa ndani mnaanza kupiga kelele wanaonewa yaani watanzania sijui tuna laana gani.
 
Haya anayosema CAG yatakuwa yalifanyika wakati Magufuli yuko Chato, hakuna namna yangetokea akiwa jumba jeupe la magogoni
Magufuri hamwezi kumchafua mkamweza, sanasana ni kujifariji tu, Magufuri amejenga stend za kisasa Tanzania,kajenga barabara mpaka za njia 8 ambazo ilikuwa ni ndoto kutokea Tanzania,kanunua ndege ambazo tawala 3 zilizopita zilikuwa zinatuambia serikali aina uwezo wa kununua ndege kwa cash, kajenga Dodoma kitu ambacho kilishindikana tawala 4 zilizopita, kajenga meli ambazo zilikuwa zimeisha shindikana, Kajengea walalaoi magorofa Sasahivi walalaoi pale magomeni hawaamini kama niwao kitu ambacho kilimshinda hata Nyerere,alafu huyo Magufuri kaiba mabilioni, Tanganyika tungelipata wezi aina ya Magufuri tungelifurahi Sana.
 
Namnukuu CAG Kichere

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari iliingia mkataba na “Mkandarasi Mkuu” wa shilingi bilioni 172.36 tarehe 3 Agosti 2019 wa muda wa mwaka mmoja hadi kufikia mwezi Agosti 2020 kwa ajili ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia meli katika bandari ya Tanga, kufanya tathmini ya athari za kimazingira, na kununua vifaa kwa ajili ya shughuli za bandari. Kwa kulingana na mkataba, gharama ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia meli katika Bandari ya Tanga ilikuwa ni shilingi bilioni 104.92 (asilimia 60 ya bei yote ya mkataba).

Hata hivyo, mnamo tarehe 1 Agosti 2019, “Mkandarasi Mkuu” iliingia makubaliano na “Mkandarasi Mbia” kwa ajili ya kazi ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia Meli kwa bei ya mkataba dola
za marekani milioni 18.15 sawa na shilingi bilioni 40.46 kwa kipindi cha miezi 11 bila kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari. Pia “Mkandarasi Mkuu” aliingia mkataba na “Mkandarasi Mbia” hata kabla ya kusaini mkataba wake na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Kuingia mkataba bila kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Bandari ilikuwa ni kinyume na Kifungu Kidogo cha 4.4 cha Masharti ya Jumla ya Mkataba kati ya Mamlaka ya Bandari na Mkandarasi Mkuu ambacho
kinaizuia Mkandarasi Mkuu kutoa sehemu ya kazi kwa Mkandarasi mwingine, na ikiwa kunauhitaji wa kutoa kazi kwa Kampuni nyingine kutekeleza kazi zilizoko kwenye mkataba, Mkandarasi Mkuu anapaswa kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Bandari siku 28 kabla ya kutoa kazi hiyo.

Aidha, nilibaini jumla ya malipo yaliyolipwa kwa kazi ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia Meli yalikuwa dola za
marekeni milioni 18.22 sawa na shilingi bilioni 40.62, kiasi hiki, pia, kinajumuisha malipo ya dola za marekani 73,824 sawa na shilingi milioni 164.55 kwa huduma za wakala wa meli kwa “Mkandarasi mbia”. Ulinganifu wa kiasi kilichotozwa na Mkandarasi Mkuu shillingi bilioni 104.92 na kiasi alicholipwa na “Mkandarasi mbia”
shilingi bilioni 40.62 inaonesha Kiasi kilichotozwa na Mkandarasi Mkuu kimezidi kiasi halisi kilichotumika kufanya malipo ya kazi hiyo kwa shilingi bilioni 64.30.

My Take
Msimamo wangu ni uleule,kwa mwendo huu ni bora nchi ikauzwa kila mtu achukue chake ajue anafanya nini. Inatia uchungu sana
Kweli, Inatia Uchungu Sana na Hasira! Mpaka nataka kuzimia Kwa Hasira!
 
Mkandarasi wa Bwawa la umeme alipatikana Kwa tenda ipi? Bei iko inflated.

Yapi Merkez Kwa tenda ipi?

Hao wote wakiwamo Mayanga walikuwa ni wakandarasi wa mchongo kuwezesha upigaji..

Nyie sukuma gang mlikuwa mafisadi Sana nguruwe nyie na mlijipanga kila kwenye sekta nyeti.
Hivi hi mayanga ipo bado

Aise waripiga kazi kwerikweri

Ova
 
Hii ndo bongo unapiga pesa za walipa kodi unaenda vulia chupi
 
tutaendelea kupata taarifa fake za CAG hii yote ni propoganda ya kufikisha ujumbe kwa wananchi ili wajue jpm si mzuri. utaona ripoti yote ya cag ikishatolewa na inahusu jpm baadae haifanyiwi kazi wakati mkandarasi yupo na wengine waliorodheshwa kwa upigaji wapo
 
My Take
Msimamo wangu ni uleule,kwa mwendo huu ni bora nchi ikauzwa kila mtu achukue chake ajue anafanya nini. Inatia uchungu sana.

Nchi huwa inauzwa wapi mkuu, namaanisha soko lake liko wapi

YESU NI BWANA

Hakuna cha kuuza hapa. Wapigaji wapelekwe mahakamani, Wahukumiwe na katiba mpya itengenezwe haraka itunusuru.
 
Halafu Kuna mbuzi zinasema JPM aliondoa upigaji, awamu ya JPM ilikuwa na upigaji ambao haijawahi kutokea tangu Tanzania ianze, alikuwa anahadaa watanzania kwa kutembea akitukana mabarabarani as if anapambana na ufisadi, aliowatumbua wote ni wale "waliomruka" kwenye mipango, mkuu wa mamlaka ya bandari alikuja kutimuliwa na mama Samia, JPM alimtunza

tumia akili ya kuzaliwa propoganda ya kumchafua jpm bado ipo. western na america wanafanya kwa putin kila aina ya propoganda
 
C&P kutoka hapa hapa JF

Mafisadi wenzie. Hakuna sheria nchini kwamba wezi wanaporudisha kile walichoiba basi hawafunguliwi mashtaka lakini Mkwere hakuwapandisha wezi wa $133 million za EPA kwa kudai kuwa pesa zile asilimia kubwa wamezirudisha pamoja na kuwa hakutoa uthibitisho wowote wa kurudishwa kwa pesa zile.

Rada walikwapua $42 million na hakuna hata mmoja aliyepandishwa kizimbani. Yule mhindi aliyekuwa rumande aliachwa atoroke katika mazingira ya kutatanisha na wahusika wengine wote waliopata mgao hawakuguswa na mkono wa sheria mpaka leo wanapeta na pesa za wizi uraiani.

Mabilioni ya Uswiss uchunguzi bado unaendelea tangu June 2012 na Mkwere hajatia neno hata siku moja na si ajabu "uchunguzi" utaendelea hata baada ya awamu yake kwisha. Cha ajabu hizo bank accounts zote wenye nazo bado wanaendelea kutoa hizo pesa za wizi na mpaka sasa wameshatoa zaidi ya Tshs 40 billion.

Meremeta walichota $155 million na Kagoda pia walichota mapesa chungu nzima na kudai ni siri kubwa za Serikali hivyo wizi ule hauwezi kujadiliwa Bungeni.

Acheni kutaka kupindisha ukweli ili kuwatetea hawa wezi wakubwa na mafisadi waliojivisha ngozi ya uongozi ambao wanakwapua mapesa chungu nzima ya walipa kodi miaka nenda miaka rudi.

tunataka watu kama nyinyi wenye akili jf sio chadomo
 
Wewe unafanya biz let’s say unaagiza vifaa vya ujenzi kutoka nje ka kontena tuwili unalipa kodi zako zote halafu mtu X anaagiza kontena 200 na analipa kodi kontena 100 tu au zaidi kidogo pale port! Unategemea utakuwa nae sawa kwa kukua? Hutakua sawa katika ushindani wke wa kibiashara n hutakua kamwe utapiga marktime tu.

Kama hujanielewa kwa notis nambie nikupe summary.

imerudi huo upigaji ndio ipo sasa
 
Magufuri hamwezi kumchafua mkamweza, sanasana ni kujifariji tu, Magufuri amejenga stend za kisasa Tanzania,kajenga barabara mpaka za njia 8 ambazo ilikuwa ni ndoto kutokea Tanzania,kanunua ndege ambazo tawala 3 zilizopita zilikuwa zinatuambia serikali aina uwezo wa kununua ndege kwa cash, kajenga Dodoma kitu ambacho kilishindikana tawala 4 zilizopita, kajenga meli ambazo zilikuwa zimeisha shindikana, Kajengea walalaoi magorofa Sasahivi walalaoi pale magomeni hawaamini kama niwao kitu ambacho kilimshinda hata Nyerere,alafu huyo Magufuri kaiba mabilioni, Tanganyika tungelipata wezi aina ya Magufuri tungelifurahi Sana.

hongera unajielewa
 
Back
Top Bottom