CAG Mstaafu Prof Mussa Assad: Kuna Waziri Kijana ana ukwasi wa kutisha miaka mitano tu madarakani!!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
18,653
Reaction score
31,010

CAG Mstaafu Profesa Mussa Assad amedai kuna Waziri kijana Awamu hii ya Sita ana ukwasi wa kutish alipoingia tu madarakani.
Prof Assad amesema
"Namjua kijana mmoja Waziri, ana magari matatu ya Shillingi 300 kils mojs,ana gari aina ya Range Rover, ana flats(maghorofa) hapa Dar es salaam chungu nzima.
Unajiuliza hii miaka mitano, umefanya kitu gani cha kukupa hizi Dola Bilioni moja"
Nipashe June 24, 2026.

Je hii ni ile sera ya kula kwa urefu wa kamba?
Wajameni Waziri Kijana ni nani huyo nasi tumuige?
 
Nini veve, TAKUKURU kwisa habari!
 
Professor amechagua mnyonge wake. Otherwise, mawaziri wenye utajiri usio na maelezo yaliyonyooka wapo wa kumwaga nchi hii.
 
Kama ana maanisha yule waziri kijana niliyemtaja hapa Live on TBC: Ridhiwani Kikwete yuko live, anaongea kama Jakaya Kikwete. Like father like son, atatufaa sana in future baada ya zamu yetu! huyu utajiri wake ni wa familia ya kitajiri, hayo majumba, viwanja na magari, vyote alimiliki kabla ya kuteuliwa waziri!, ni mwanasheria na wakili, ikitokea wakili akasaini mkataba mmoja tuu, anaweza kulipwa hadi dola 1.M, sasa nini cha ajabu?!.
P
 
Nayeye hawezi kumuongelea huyo cause anajua ni tajiri kabla hajawa waziri
 
Mkuu umeamua kuwa The Devils Advocate?
 
Mkuu umeamua kuwa The Devils Advocate?
No mimi siku zote ni mkweli, tusikubali watu wasafi wachafuliwe kwa majungu!, dogo nimesoma nae chuo UDSM, tangu chuo yuko njema on family support, kisha kawa wakili, just a single deal wakili anaweza kuvuta mpaka US$1.M, hivyo kama ni huyo namjua anatoka familia bora!.
P
 
Na ameenda Mexico kuangalia WEDI KAPU?
 
Swali liko wazi, alipataje $ 1 BILLION akiwa mtumishi, and in the last 5 years.
Ee bwana dont fool us!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…