Katika mahojiano maalum yaliyorushwa na M&S Podcast, Juni 24, 2026, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Prof. Mussa Juma Assad, amefafanua kuwa kiongozi bora ni yule mwenye uwezo wa kusimamia watu na taasisi kwa ufanisi kupitia mambo makuu matatu: upangaji wa mipango ya muda mrefu (planning), utekelezaji makini unaoshirikisha timu thabiti ya watu, na upimaji wa matokeo (performance measurement).