CAG Prof. Assad astaafu, Charles Kichere ateuliwa kuwa CAG mpya

Rais ameteua CAG mnyonge, kwaajili ya Serikali ya wanyonge. Hatari sana.
 
In facts he dont know what happen....
 

Attachments

  • 77148205_3454338214578053_1431037782532292608_n.jpg
    21.6 KB · Views: 1
Embu cheki Sheria ya Ofisi ya CAG inasemaje....usijekuta imetoa masharti mengine
 
Rais ameteua CAG mnyonge, kwa ajili ya Serikali ya wanyonge. Hatari sana.
Hakuna CAG wa wanyonge. Kinachotakiwa ni uadilifu. Hata ukitoka kwenye familia maskini, kama wewe ni mwizi utakuwa mwizi tu. Kumbuka hata katika wanyonge kuna waliyo afadhali. Watanzania wengi wanatoka familia za kinyonge kiuchumi. Lakini Nyerere hakutoka familia ya kinyonge kiuchumi. Baba yake alikuwa chifu na kuchumi alikuwa afadhali. Lakini yeye alikuwa raisi wa wanyonge.

Ukiangalia TZ maraisi wengi walitoka kwenye familia zenye hali mbaya kuuchumi, lakini tunajuwa kilichotokea. Kwa hiyo mtu anaweza akatoka kwenye utajiri lakini akawa na moyo wa kuwatetea wanyonge. Anaweza akatokana na wanyonge kiuchumi na akawa mfakamiaji wa mali za walipa kodi, tena anakula bila kunawa.

Kwa hiyo mimi naona Assad alikuwa pia wa wanyonge lakini kulikuwa na mikwaruzano ya kibinadamu, ambayo kiukweli ilikuwa vigumu kuongezewa muda. Hata Assad nadhani aliyaona hayo na hakutaka kuwa chanzo cha migogoro ya mihimili mitatu. Bunge (spika) tayari alikuwa haelewani na CAG lakini hao wawili wanatakiwa kufanya kazi pamoja. Mimi ninamsifu CAG kuyaona hayo na kuamuwa kuondoka. Maana angeomba kuongezewa angemweka raisi pabaya, maana kulikuwa na uwezekano wa kutomuongezea muda maana tayari alikuwa na mkwaruzano na Bunge (spika).
 
Hatimaye uchafu wote kufichwa
Tuna safari ndefu sana awamu hii.
Labda Kwa sababu "NCHI ILIYOPATA MAENDELEO FEDHA HAINA SAMANI" jamaa anamkwanja Sana atakuwa anadharau report Kwa sababu ni story "FEDHA KUINGIA KWENYE MZUNGUKO"
 
Only in Tanzania. Miezi michache tu alimtumbua toka TRA hadi kuwa RAS.
Alisema dhahiri kashindwa kazi TRA. Sasa ataweza kuwa CAG na elimu yake yenye mashaka?
Ndio maana tunasema huyu MtuPori huwa haeleweki au tuseme anaropoka bila kupima maneno. Leo unamshusha cheo mtu kuwa utendaji wake hauridhishi, baada ya muda mfupi unampa madaraka makubwa zaidi hata ya Yale uliyokuwa umemvua.
Shida sana kuwa na mtu wa aina hiyo
 
Ndiyo. Kapandishwa tena cheo baada ya kushushwa kutoka kamishna TRA na kapelekwa kuwa katibu tawala. Leo kapanda tena cheo na kuwa CAG.
hiki kitendo kinaonyesha vile magufuli amekosa INTELLEGENT WAY OF THINKING AND DOING THINGS,but i dont blame magufuli i blame his lack of education
 
Mkuu mbona unachanganya mambo? CAG ameomba kuondoka lini? Huyu amestaafishwa bila hata ya yeye mwenyewe kupewa taarifa, fuatiliana maoni yake baada ya hizi taarifa za CAG mpya.
 
Huyu ametenguliwa ndiyo maana hapo kwenye andiko la mtoa mada amemnukuu mwenyewe Prof Assad kuwa hana taarifa yoyote na huo utenguzi wake kwakuwa yupo nje kikazi.sasa cha kujiuliza mtu kama Pro Assad inakuwaje asielewe kwamba muda wake kukaa ofisini umeisha halafu yeye asafiri tena safari ya kikazi.yeye anachoamini muda wa kustaafu yaani miaka bado haijafika.
 
Kwa kuwa CAG Ni independent office yake ifanye tu hivo kuepuka kuwa unable kujua Nani kakwapua na mwisho kuwa office ya kusema tu hazionekani!
Hicho kitengo cha ujasusi watu wake watatoka sayari gani? Na watakuwa wanafanya kazi chini ya nani? Bajeti yao je? Na recruitment atafanya nani?
 
wasalaam, kuna habari zinasambaa kwa kasi sehemu mbalimbali nchini kwamba CAG mpya mh kichere ni dhaifu kutoka na historia yake ya utendaji huko nyuma. Habari zinasema kwamba bwana kichere ni mtu wa ndio mzee na kuanzia sasa ukaguzi wa hesabu za serekali utafanywa na serikali yenyewe kwa maelekezo kutoka pale nyumba nyeupe.

Tusubiri muda ni rafiki huenda ni majungu tu labda watu wanazusha. Maendeleo yana vyama usipochagua ccm hakuna kuletewa maendeleo.
Ova.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…