CAG Prof. Assad astaafu, Charles Kichere ateuliwa kuwa CAG mpya

Ulinisoma hadi mwisho, au ulisoma para ya kwanza tu uka-conclude?! Ungenisoma hadi mwisho na kunielewa, ungejua neno stahili kwangu halikuwa msisitizo!

Halafu unashangaza sana unaposema Rais yupo ndani ya sheria na wakati huo huo una-cite Public Act 2008! Hiyo sheria umeisoma?! Na kama umeisoma, umeilewa?!

Kumbuka kwamba, Katiba ya Jamhuri. Ibara ya 144 (1) inasema:-
Controller and Auditor-General of the United Republic shall be obliged to vacate office upon attaining the age of sixty or any other age which shall be prescribed
by a law enacted by Parliament.
Kwa tafsiri isiyo rasmi, ATALAZIMIKA kuachia ofisi akifikisha miaka 60, au umri wowote utakaotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge!!

Swali la kwanza: Je, Profesa Assad kafikisha umri wa miaka 60?! Jibu ni HAPANA kwa sababu amezaliwa Oktoba 6, 1961. Kwa maana nyingine, last month kafikisha miaka 58, na atafikisha miaka 60 Oktoba 5, 2021... kwa hiyo ana miaka 2 bado!!

Kuna watu wanadai huwezi kumwongezea muda kwa sababu ukimwongezea muda, hadi miaka 5 inaishia atakuwa amevuka miaka 60.

SWALI: Je, CAG akifika miaka 60 ni LAZIMA aachie ofisi?! Hapa pia jibu ni HAPANA, kwa sababu katiba imesema "...
or any other age which shall be prescribed by a law enacted by Parliament. Kumbe yetu imesema ataachia akifikisha miaka 60 au umri wowote kama utakavyotajwa na Sheria ya Bunge!!

Je, Bunge limetaja huo umri wowote mbali na ile miaka 60?! Jibu ni NDIYO! Public Audit Act 2008 Ibara ya 6(2)(a) inasema
Unless the question of removal becomes the subject of investigation in terms of Article 144(3) of the Constitution, the Controller and Auditor-General shall vacate office upon attaining the age of sixty five years;
Kumbe Public Audit Act 2008 uliyoweika hapo juu bila kuisoma au kuilewa, inasema CAG ATALAZIMIKA kuachia ofisi akifikisha miaka 65 "....Unless the question of removal becomes the subject of investigation in terms of Article 144(3) of the Constitution."

Hapo juu tumeona Assad ana miaka 58, wakati Katiba inataka awe amefikisha miaka 60 au umri utakaotajwa na Sheria ya Bunge! Kwa maana nyingine, kuchagua CAG mwingine wakati Assad akiwa na miaka 58, hiyo ni REMOVAL... kwamba, AMETUMBULIWA!!

Ametumbuliwa kwa sababu, mosi, hajafikisha miaka 60, lakini pili, Public Audit Act 2008 Ibara ya 6 (1) inasema:- The Controller and Auditor-General shall hold office for the fixed term of five years and shall be eligible for renewal for one term only.[/QUOTE]Kumbe sio tu hajafikisha miaka 60, lakini pia he's elligible for renewal.

Na kwa muktadha wa sheria ZETU, neno SHALL ni shuruti... passipo na shuruti hutumika neno MAY.

Na ukitaka kuona ni namna gani neno SHALL ni shuruti, Ibara ya 4 (1) ya Public Audit Act 2008 inasema:-
(1) The Controller and Auditor-General shall be appointed by the President from among the citizens of the United Republic of Tanzania by birth.
Kwa sababu hamna mwingine anayeweza kumteua CAG zaidi ya rais.

Na kwavile kilichotokea ni KUTUMBULIWA, Public Audit Act 2008 hapo juu inasemat CAG atatumbuliwa:- "... Unless the question of removal becomes the subject of investigation in terms of Article 144(3) of the Constitution."

Je, kuna jambo CAG amefanya na kwahiyo anatumbuliwa ambalo ni subject of investigation kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 144 (3)?!

Unless uweke vifungu vya sheria vinavyosema Rais yupo ndani ya sheria, kinyume chake, Rais sio tu amevunja katiba bali pia amevunja sheria ya Bunge... Public Audit Act 2008!
 
Unaweza kutoa mfano wa hiyo politicizing yake?! Au kusema Bunge halitekelezi wajibu wake kwako wewe ndio politicizing?!
 
Ukweli na msimamo usioyumba ndicho kilichomponza; historia itaendeelea kumkumbuka vizazi na vizazi.

Mwendo umeumaliza vyema
 
Hongera yake kwa utumishi wake uliotukuka kwenye nchi yetu kipindi akiwa CAG...
 
Ukwel na msimamo ucyoyumba ndicho kilichomponza historia itaendeelea kukumbuka vizazi na vizaz mwendo umeumaliza vyema
Hapa ndipo chadema wanapofeli, huwezi amini mtu mmoja kuwa ndiyo mwenye uwezo pekee kama mbowe, kila mtumishi wa umma anafaa kwa nafasi take, muda umeisha astaafu mbona Kuna walimu manesi na polisi walishastaafu, site tunaona wizi kila Kona mwanri Yuko anahangaika waziri mkuu Yuko anahangaika, takukuru ndio wamekuwa cag kila sehemu tkkr chunguza Kama ofisi ya cag haina mtu, arudi chuo akashike chaki.
 
Ukweli na msimamo usioyumba ndicho kilichomponza; historia itaendeelea kumkumbuka vizazi na vizazi.

Mwendo umeumaliza vyema

Mkuu hawa watu wakiteuliwa kwenye hizi nafasi ..wananchi hatushirikishwi…..iweje wakifukuzwa au mwajiri akiwaondoa tuumize vichwa??

Assad aliwekwa kwa matashi ya mkuu wa nchi..kaondolewa kwa matashi yake. Yes..tunaweza tusikubaliane na hili lakini sidhani kuumiza kichwa itasaidia. Tupambane tupate mifumo sahihi wa kupeana hizi nafasi. Hapo tutakuwa na la kusema watu wakiondolewa kinyume na sheria.

Kwa sasa hata kama sikubaliani na JPM..lakini ni haki yake kufanya maamuzi ya uteuzi!
 
Kumbe sio tu hajafikisha miaka 60, lakini pia he's elligible for renewal.
[/QUOTE]
Na kwa muktadha wa sheria ZETU, neno SHALL ni shuruti... passipo na shuruti hutumika neno MAY.
Sasa mkuu jiulize kama SHALL hapa inaweka shuruti kwa nini wasiseme atakuwa appointed kwa fixed term ya miaka 10? Niisomavyo mimi hapa hii clause inampa RAISI uwezo wa kumchagua tena kwa miaka mingine mitano mtu huyo huyo. Mhusika anakuwa eligible-anaingia kwenye kapu la contenders tu.
 
Sasa kwanini waandike atakuwa appointed kwa fixed miaka 10 wakati CAG sawa na vyeo vingine kadhaa vinaenda kwa renewable terms?!

But on top of that, ukisoma vifungu vya sheria bila kuunganisha vifungu lazima utakosea tu! Pasipo na SHURUTI, Katiba na Sheria zetu zinatumia neno MAY na sio SHALL kama inavyoelezwa kwenye Interpretation of Laws Act Ibara ya 53 (1&2) kwamba:-
 
Kumbe sio tu hajafikisha miaka 60, lakini pia he's elligible for renewal.

Sasa mkuu jiulize kama SHALL hapa inaweka shuruti kwa nini wasiseme atakuwa appointed kwa fixed term ya miaka 10? Niisomavyo mimi hapa hii clause inampa RAISI uwezo wa kumchagua tena kwa miaka mingine mitano mtu huyo huyo. Mhusika anakuwa eligible-anaingia kwenye kapu la contenders tu.
[/QUOTE]
Kama neno shall ndio kizingiti Cha yeye kukaa ofisini mbona hata kipengele Cha uraisi nacho kinasema shall, Sasa tunahangaika Nini kupiga Kura siakae miaka 10.
 
Kazi ipi? Wakati kazi yake ni kwenda kuwasafisha wale waliokula trillion 1:5 kuwalinda wanunuzi wa mdege waliokula 10% na kulinda 10% na ufisadi wote kwenye miradi yote mikubwa
Unaweza kuwa na ushahidi usiokuwa na shaka utuwekee hapa ili hoja yako iwe kweli?
 
Kupanda na kushuka na kupanda tena


Ukiinuliwa na mwanadamu, wanadamu watakushusha chini. Ukiinuliwa na Mungu juu, ni lazima utakua juu. Hongera mkuu na ukafanye kazi kwa haki na weledi.
 
Mungu wangu! Wewe jamaa ni mafia aisee! Wewe ni kichwa! Una akili mingi( sio tena nyingi)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…