Ulinisoma hadi mwisho, au ulisoma para ya kwanza tu uka-conclude?! Ungenisoma hadi mwisho na kunielewa, ungejua neno stahili kwangu halikuwa msisitizo!Mkuu nafikiri umelivuta sana hilo neno "ku-stahili" nawe umeligeuza kuwa lazima mkataba wake uwe renewed. Maana halisi ni kuwa anaweza akapewa mkataba mwingine au kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Tunaweza kujiuliza kwa nini raisi hakumpa mkataba mwingine lakini kisheria raisi yuko ndani ya sheria (Public Audit Act 2008)
Halafu unashangaza sana unaposema Rais yupo ndani ya sheria na wakati huo huo una-cite Public Act 2008! Hiyo sheria umeisoma?! Na kama umeisoma, umeilewa?!
Kumbuka kwamba, Katiba ya Jamhuri. Ibara ya 144 (1) inasema:-
Kwa tafsiri isiyo rasmi, ATALAZIMIKA kuachia ofisi akifikisha miaka 60, au umri wowote utakaotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge!!Controller and Auditor-General of the United Republic shall be obliged to vacate office upon attaining the age of sixty or any other age which shall be prescribed
by a law enacted by Parliament.
Swali la kwanza: Je, Profesa Assad kafikisha umri wa miaka 60?! Jibu ni HAPANA kwa sababu amezaliwa Oktoba 6, 1961. Kwa maana nyingine, last month kafikisha miaka 58, na atafikisha miaka 60 Oktoba 5, 2021... kwa hiyo ana miaka 2 bado!!
Kuna watu wanadai huwezi kumwongezea muda kwa sababu ukimwongezea muda, hadi miaka 5 inaishia atakuwa amevuka miaka 60.
SWALI: Je, CAG akifika miaka 60 ni LAZIMA aachie ofisi?! Hapa pia jibu ni HAPANA, kwa sababu katiba imesema "...
or any other age which shall be prescribed by a law enacted by Parliament. Kumbe yetu imesema ataachia akifikisha miaka 60 au umri wowote kama utakavyotajwa na Sheria ya Bunge!!
Je, Bunge limetaja huo umri wowote mbali na ile miaka 60?! Jibu ni NDIYO! Public Audit Act 2008 Ibara ya 6(2)(a) inasema
Kumbe Public Audit Act 2008 uliyoweika hapo juu bila kuisoma au kuilewa, inasema CAG ATALAZIMIKA kuachia ofisi akifikisha miaka 65 "....Unless the question of removal becomes the subject of investigation in terms of Article 144(3) of the Constitution."Unless the question of removal becomes the subject of investigation in terms of Article 144(3) of the Constitution, the Controller and Auditor-General shall vacate office upon attaining the age of sixty five years;
Hapo juu tumeona Assad ana miaka 58, wakati Katiba inataka awe amefikisha miaka 60 au umri utakaotajwa na Sheria ya Bunge! Kwa maana nyingine, kuchagua CAG mwingine wakati Assad akiwa na miaka 58, hiyo ni REMOVAL... kwamba, AMETUMBULIWA!!
Ametumbuliwa kwa sababu, mosi, hajafikisha miaka 60, lakini pili, Public Audit Act 2008 Ibara ya 6 (1) inasema:- The Controller and Auditor-General shall hold office for the fixed term of five years and shall be eligible for renewal for one term only.[/QUOTE]Kumbe sio tu hajafikisha miaka 60, lakini pia he's elligible for renewal.
Na kwa muktadha wa sheria ZETU, neno SHALL ni shuruti... passipo na shuruti hutumika neno MAY.
Na ukitaka kuona ni namna gani neno SHALL ni shuruti, Ibara ya 4 (1) ya Public Audit Act 2008 inasema:-
Kwa sababu hamna mwingine anayeweza kumteua CAG zaidi ya rais.(1) The Controller and Auditor-General shall be appointed by the President from among the citizens of the United Republic of Tanzania by birth.
Na kwavile kilichotokea ni KUTUMBULIWA, Public Audit Act 2008 hapo juu inasemat CAG atatumbuliwa:- "... Unless the question of removal becomes the subject of investigation in terms of Article 144(3) of the Constitution."
Je, kuna jambo CAG amefanya na kwahiyo anatumbuliwa ambalo ni subject of investigation kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 144 (3)?!
Unless uweke vifungu vya sheria vinavyosema Rais yupo ndani ya sheria, kinyume chake, Rais sio tu amevunja katiba bali pia amevunja sheria ya Bunge... Public Audit Act 2008!