CAG Ripoti 22/23: TEMESA inailipa Kampuni ya AZAM Tsh. Milioni 5 kila siku kuendesha Vivuko

Kweli serikali imeshindwa kutengeneza vivuko kama hivyo vya Azam, au bora mradi wote wamuachie Azam Tu.
 
Kuna kitu sijaelewa Wakala wa umeme na vivuko vya magogoni vinahusiana vipi

Alafu hivyo vivuko vya serikali ukarabati wake unachukua miaka mingapi?

2022 Hadi Leo 2024 ukarabati haujakamilika
 
Ni mkataba wa wizi tu. Vigogo wa Temesa huo mkataba wanakula na azam. Ndio ile tunasema vigogo Temesa wamejibinafsishia shirika. Ukiona Temesa inapata hasara sio hasara. Vigogo pamoja na bodi yao ya wakurugenzi wanachukua gawio huku hawajawekeza kitu na huku wanapata mishahara na posho kibao. Ndio sisi tunasema tunataka uongozi wa kimagufuli ndio suluhisho la ubadhirifu na wizi wa mali ya umma.
 
Mikata
Azam anajichukulia milioni 5 zake kila siku huku gharama za matengenezo, mafuta na nyingine ni mzigo wa wajinga..

Hii nchi ipo kama haina serikali, viongozi wake wote hawana akili.
watu wanafaidika kila Azam inapopiga mzigo! Sasa hayo mapantoni ya Temesa yatatiwa ubovu mkubwa ili watu waendelee kubunya.
 
Ni Ujinga sana,Kwa nini Azam marine asiachwe huru kama private service provider na Serikali ikachukua Kodi zake kuliko huu Ujinga?
 
Si wawaachie Azam tu wafanye hii shughuli ya vivuko!?
Maana hivyo vivuko vya Magogoni ni michosho havina ufanisi.
Yani ukisema utegemee kivuko cha MV.Magogoni unaeza kuta anaepitia daraja la nyerere akafika mjini wewe bado.
Vitu vingine waachieni watu wanaoweza kuviendesha kwa ufanisi.
 
Kama Azam wanapata asiliamia 31 ya makusanyo sioni shida ikiwa huduma zimeimarika sana na za uhakika! Sasa CAG alitaka Azam alipwe Tsh ngapi ikiwa anaingiza hela zote hizo? Labda tushauri tuu kuwa pengine Azam apewe kabisa hilo eneo la magogoni kuliendesha halafu serikali ipate kodi na wagawane makusanyo…..

Hiyo Mv Magogoni ipelekwe sehemu nyingine yenye changamoto ya Vivuko….Azam wapewe kuendesha hilo eneo kwa hizo speed boat kuliko kupoteza muda na hiyo MV magogoni!
 
Sasa hawa nao ni wajinga mbona ni hesabu rahisi sana.
Kama unakusanya 5 bill na mbia analipwa bill 1.8. Kwa vivuko 2
Kwann usimwombe mbia (azam) akuletee kivuko kingine cha kuvusha vyombo vya moto then ukabaki kusimamia na ukapata faida maana utakuwa unamlipa 3.5 billion na utabaki na 1.5 billion. Hizo billion kusimamia kivukoni pale zinatosha kabisa maana unakodisha kampuni ya kusimamia machine za Scanner zile, ulizi na za usafi unazipa kwa mwezi basi unabaki na faida kubwa tu.
 
Hizi ni deal za watu. Ndiyo maana hawataki kuachia nchi. Wengine wamegeuza uongozi kuwa club ya usagaji.
Hebu naomba ufafanuzi zaidi eneo hilo la usagaji, hizi story nazisikia sana hebu elaborate tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…